Naomba ushauri kuhusu dini

Naomba ushauri kuhusu dini

Nimekuelewa ila sijasoma shule za katoliki nimekaa hostel tu za wakatoliki ambazo hazitoi mafundisho ya dini labda uwe unaenda kanisani kwao na ukumbuke wakat naenda hiyo hostel tayar nilishabadili jina kuwa la kikristo na kusema baba yangu ni mkristo!
Kweli elimu ya chekechea ndiyo niliyonayo kwenye dini zote mbili
Wewe si umesema umesoma vitabu vyote vya dini ya uislam
 
Wewe siulisema unaijua Qur'an sasa mbona unaanza tena kusema unasali kule unakoielewa lugha?.
Unafikr ukilitadi wewe uislam utakufa?
Kwendlaaaaaaaaaaa.
Anasema anaijua KURUAN halafu hapo hapo haelewi ndio maana ANASALI kule anakoelewa
 
Wewe hukijui kiarabu bali ulijua kusoma maandishi ya kiarabu na si maana ya maandishi au maneno ya kiarabu

Tafautisha kujua kusoma na kujua maana halafu urudi hapa utuambie hio dini yako(uislamu) unayosema unaijua hukuijua bali ulikuwa ukiimba maneno ya kiarabu kama yule ndege Kasuku na hii ndio shida ya wengi
Hata kusoma hayo maandishi ya kiarabu for sure hajui. Huyo ni kafiri tu
 
Lakini kama Yesu ni mwana wa Mungu na sisi ni wana wa Mungu, vipi unakubali hilo ?
Ndiyo.

Yesu ni Mwana wa Mungu na Kristu Yesu yu ndani ya Baba na Baba yu ndani yake.

Ukimuamini Kristu, I mean Yesu unakuwa ndani ya Yesu na Yesu ndani yako. Huoni automatically unakuwa Mwana wa Mungu na ndani ya Baba - kwa kuwa kwako ndani ya Yesu?

Wote walioamini wamefanyika kuwa wana. Na sio kinasaba. Tuseme labda ni ki hadhi au na kiurithi wa ufalme na sio kimali na wala sio kimamlaka na wala sio baada ya Baba kufa mana hana mwanzo wala mwisho!. Maana katika uwanda wa kiroho mambo ni infinity na muda ni eternal/milele.
 
Haki ya watoto wanavyolawitiwa makanisani. Mpaka papa imembidi aombe radhi
Papa kajishusha, Je kuna sheikh yoyote ambaye alisimama kwenye hadhara na kukemea vitendo vinavyofanyika kwenye madrassa?
 
Kwanza nakupa pole sana, umesema umesoma madrasa na unaijua Dini ya kiislamu?kwa mtu anayeijua Dini ya Kiislam hawezi kuja kuomba msaada hapa jukwaani, naamini wewe ungekuwa msaada kwa wengine kuwaingiza kwenye Uisilamu.

Kama kweli ulichokifanya unakijua na malipo yako utakuwa unayajua baada ya kufa kaburini na siku ya kiaama. Kibaya zaidi unadiriki hata kuwapotosha watoto zako wakati wazazi wako wamekupa kheri zote? Nimejaribu kuandika lakini nashindwa kuuendelea, angalia wanaokupotosha wanakwambia Dini zote ni sawa, wapi na wapi? Nenda kwa wazazi wako ukawaambie kuhusu msimamo wako nadhani watakusaidia zaidi
Hivyo ni vitisho tu, nani alitoka kaburini akaja kukusimulia yaliyomkuta huko kaburini, Yesu mwenyewe pamoja na kufufuka lkn hakusema nini alikutanacho kaburini alisepa moja kwa moja mbinguni, mpaka leo tunasubiri lkn haji, tunaambulia vitabu vya injiri navyo ni vya kutunga tu wala YESU hakuviacha.
 
Hana elimu yoyote huyu ni sumbua tu, sema ujinga wake tu hauja kudhihirikia ila ni mjinga sana katika hayo anayoyaandika.

Majibu yako yamenyooka ila kwa Mokiti ni kama unampigia mbuzi gitaa.



Sent using Jamii Forums mobile app
Fuatilia mada ilipo anzia , alisema wazi Allah anapotosha nafsi 😂 ni yeye mwenyewe kasema , nilipo muuliza kama Allah anapotosha nafsi shetani anafanya kazi gani, ndio unaona akaanza kuleta takiya , ila ukweli Allah kasema mwenyewe yeye ndie anae potosha nafsi za watu
 
Hata kusoma hayo maandishi ya kiarabu for sure hajui. Huyo ni kafiri tu
Hayo maandishi ya kiarabu yametafsiriwa? Mimi kafiri nikitaka kusoma naruhusiwa? Ukiwa unaomba unatumia lugha ipi? Je lugha tofauti na hiyo maombi yanasikilizwa?
 
Mimi ni Muislam kwa baba na mama na hatuna historia ya dini nyingine labda huko nyuma kabisa ambapo hata bibi zangu hawakuwepo au hawajui, imetokea mimi tu kuupenda ukiristo kiasi ambacho tangu niko form one miaka zaidi ya ishirini kubadili majina yangu na kuwa ya Kikiristo na nilikua nikisema baba yangu mkristo mama yangu ndiyo Muislam.

Bahati mbaya nikiwa form two nilikaa hostel ya waroma kwahivyo nilikuwa napenda wakati mwingine kwenda kanisani japo nilikua sielewi kitu, kuna wakati napotezea naanza kusali kiislam kwasababu dini ya Kiislam naijua nimesoma madrasa nikiwa mdogo na hakuna kitabu cha dini kina kina kinanishinda kusoma na hapo zamani nilikua nikisia mtu anasoma kuruan nalia bila kujua nalilia nini nikawa namwambia mama mbona nie nalia nikiona au kusikia kuruan inasomwa? Mama ananiambia tu inaitwa midadi hiyo.

Nimejikuta tu wanangu sijawapeleka madrasa na shule nimewapeleka shule za kikiristo na sipendi kabisa za kiislam wala madrasa na huwa nawaambia wanangu nendeni kanisani, na utu uzima huu kuna wakati nilipata majanga makubwa nikaona njia sahihi ni kuombewa kanisani nikaenda roma kuombewa ndani ya siku tatu pepo likatoka na nimeendelea kusali kiroma nikiwa nyumbani na natumia maji ya baraka wakati mwingi nahisi kabisa yananisaidia, halafu nikiwa kanisani nina amani zote nachokisema nakielewa nachokisali nakielewa! Naona mahubiri ya father nayaelewa vizuri na hapa nyumbani redio nasikiliza redio Maria tu na naifurahia.

Sasa wakuu nisaidieni hili ni pepo au nini? Je nibadili dini na utu uzima huu? Au nifanyaje nifute historia hii? Yaan sasa hivi ndiyo nazidi kuzama kwenye ukristo kiasi ambacho hata wanangu natamani waanze mafundisho, au kuna sehemu sijielewi?
Wewe sio muislam au hujui chochote kuhusu uislam wewe umetumwa jitahidi ufe katika mila sahihi ya uislam
 
Hapa nadhani utafurahi kusikia mkristu anatamka hivi.

Tunatofautiana uelewa kiroho kuna watoto na watu wazima. Paul alitumia usomi wake kuwaelekeza watu katika lugha ambayo wataielewa kwa urahisi. Kuna vitu alivilainisha kwa kusudi jema tu kulingana na anaowaandikia. Wasomi wote hufanya hivyo.

Mitume wote na manabii wote walifanya hivyo, kuliwasilisha jambo kwa namna inayoeleweka kwa wanaowaambia. Ndo maana lazima tutumie akili kuelewa maana na muktadha

Mimi tafakari yangu itakuwa: Katika dunia ilokuwa na miungu mingi kwa levo walokuwa nayo wa juu kuliko wote akawaambia ni Yesu. Ukilinganisha na hiyo miungu. Ndiyo maana akasema Mungu mkuu kwa levo yao.

Titus 2:13, CSB: while we wait for the blessed hope, the appearing of the glory of our great God and Savior, Jesus Christ.
Acha niseme tu kwamba,mimi bado sijakuelewa kwa sababu ufafanuzi wako umejikita katika kutumia uwezo wako binafsi bila ya msaada wa andiko.
Lakini wakristo wengi udai kuwa maandiko ya biblia ni vigumu mno kuyaelewa eti mpaka Roho Mtakatifu akuongoze.
 
Acha niseme tu kwamba,mimi bado sijakuelewa kwa sababu ufafanuzi wako umejikita katika kutumia uwezo wako binafsi bila ya msaada wa andiko.
Lakini wakristo wengi udai kuwa maandiko ya biblia ni vigumu mno kuyaelewa eti mpaka Roho Mtakatifu akuongoze.
Maandiko mi wala sijakariri, nikiyasomaga huwa nayajumlisha kichwani napata maana yake natulia.

Siku nyingine nikiulizwa natumia sense tu iliyojijenga na nashkuru Roho wa Mungu huwa ananiongoza kwa kweli.

Kwa hiyo kama unasubiri niquote vifungu huwa sipo vizuri. By the way mimi sio muwakilishi mzuri wa dini yoyote. Ila natamani kuwa na ni mfuasi mzuri wa Kristu🐣
 
Kuna mwalimu wangu aliwahi kujenga hoja yake kuhusu utatu akasema.
" Ujue ni rahisi kumuelewezsha mtoto kuwa Mungu I mmoja, kuliko kumwambia Mungu amegawanyika mara tatu,"

Nilipouona huu mfano wako ndio Nimekumbuka hii, yaani najiuliza kama sisi watu wazima umeona huwenda hatuja uelewa huo mfano wako, sijui watoto wenu huwa mnawaelewesha vipi?

Hivi unajua tofauti ya sifa na dhati?

Gari - dhati
Linakimbia, jeusi - sifa

Tangu nianze kutumia Jf sijawahi kumuona mkristo akifafanua utatu akaeleweka.
ngoja nijaribu kuelezea utatu.

Kwanza ili uelewe utatu lazima ujue utofauti huu

a)1+1+1=3

b)1×1×1= 1

Katika mfano ' b' hapo juu ndio utatu wenyewe .

Ni hivi , baada ya wanadamu kuasi katika kanuni za kiroho ilipaswa lazima uhai utoke ndio wanadamu wapate kusamehewa dhambi zao.

Kumbuka Mungu hajikani neno lake, mshahara wa dhambi ni mauti na yeyote aliyetaka kuondolewa dhambi mauti iliyotokana na kuchinja mnyama au wanyama na kutoa sadaka( utaona kwenye agano la kale ) ilihusika.


Sasa kwa kuwa Mungu ana upendo, na ili asilikane neno lake na sheria yake mwenyewe ilibidi ashuke mwenyewe na itolewe sadaka takatifu ambayo itakomboa watu wote na utumwa wa dhambi ambao uliwahitaji wao kutoa sadaka niliyotaja hapo juu.


Sasa Mungu anashukaje, hapa ndio utatu unaeleweka sasa , Mungu akashuka kwa njia ya mwanadamu ( kumbuka yesu hakuwa mbegu ya mwanadamu ) kama wanadamu wengine, na hakuna mwanadamu wa kawaida ambaye anatokea katika mbegu ambazo sio za mwanadamu.

Mungu huyo huyo akashuka in form of a human kwaajili ya ukombozi wa watu.

Sasa kuna watu huwa wanauliza swali la kijinga kama Mungu alishuka duniani , mbinguni alibaki nani ( watakaouliza hivi na wenyewe tuwaulize Mungu anawezaje kusikia mtu aliyepo singida , mwingine austaralia , Mwingine india?) hivyo basi jibu Mungu ni muweza wa yote na anaweza kuwa kote muda wote. Tusiulimit uwezo wa Mungu kwa uwezo mwanadamu wa kuwepo eneo moja kwa wakati mmoja.

Yesu alipomaliza mission yake akaondoka, alipoondoka akasema Roho mtakatifu atachukua hatamu.

Roho mtakatifu ni roho wa Mungu, anatufundisha na anatuongoza hapa duniani baada ya Mungu kuondoka inform of a human.

Yesu= Mungu alipokuja kama mwanadamu na ndio neno la Mungu

Roho mtakatifu= Roho wa Mungu/Jehovah ambaye hata hapa duniani ukiamua kusali utamsikia kabisa akikuongoza katika mambo mbalimbali

Mungu Baba= Jehovah/Yahweh

hivyo utatu ni simple kuelewa.... 1×1×1=1
 
Nilitaka nikuoneshe ni kweli ulivyo sema Allah anapotosha nafsi , na ulimuomba mwenyewe asikupotoshe nafsi yako

Nilitaka nikuoneshe ni kweli ulivyo sema Allah anapotosha nafsi , na ulimuomba mwenyewe asikupotoshe nafsi yako
Nilirekebisha kwa kuandika nilichokusudia kama in ligi tafuta kwingine maana inaonekana unaujua undani wangu hats baada ya kukuambia kusudi langu lilikua lipi. Usiku mwema
 
Nilirekebisha kwa kuandika nilichokusudia kama in ligi tafuta kwingine maana inaonekana unaujua undani wangu hats baada ya kukuambia kusudi langu lilikua lipi. Usiku mwema
Huyo jamaa ni sumbua tu achana nae.
 
Back
Top Bottom