Tetesi za mjasiriamali aliyejipata miaka ya karibuni na staa wa filamu Tanzania, Jacqueline Masawe Wolper kwamba yeye na watoto wake wapo njiani kubadili dini, ndiyo trendi ya mitandaoni kwa sasa.
Habari kutoka huko mitandaoni zinasema kuwa, Wolper anatamani kutoka kwenye Ukristo ambao ni wa kuzaliwa na kuwa Muislamu huku ikielezwa kuwa, anapendezwa na maadili ya imani hiyo.
Sasa kwa mujibu wa rafiki wa karibu na Wolper mwenyewe ambaye aliomba jina lake lisipandishwe mitandaoni, mchungaji Matheo wa Tanzania Apostles of God (TAG), Tabata-Kimanga, Dar es Salaam alipoisoma taarifa hiyo mitandaoni, alimkalisha chini binti yao huyo na kumuonya aache kuchukua imani pacha na kubaki kwenye imani yake ya kuzaliwa.
Inaelezwa kuwa, mchungaji Matheo alimtaka Wolper kutohangaika kwenye kumtafuta Mungu akimkumbusha hatua kama hiyo akiwahi kuifanya mwaka 2013 na baadaye kurejea kundini pale K.K.K.T Usharika wa Kijitonyama, Dar.
Rafiki huyo akaendelea kusema kuwa, tayari staa huyo ambaye alifunga ndoa na mjasiriamali Richi Mitindo na kuzaa naye 'majamaa' wawili, ameshachagua jina la Jamila ambalo J yake inashikamana na J ya Jacqueline ili aendelee kutumia kitambulisho cha NIDA kwenye 'dokumenti' zake ili kuzugia kuwa, J ni kifupi cha Jack kumbe wakati huohuo ni herufi ya kwanza ya Jamila.
Rafiki huyo aliendelea kusema kuwa, mchungaji huyo alitishia kupiga magoti kwa Mungu ili staa huyo apate adhabu ya kimwili ili ajue makosa ya kutangatanga kiimani.
Mwaka 2013, Wolper alibadili dini kuwa Muislam baada ya kuangukia kwenye uchumba uliyotikisa akiwa na mfanyabiashara aliyeibuka ghafla aitwaye Dallas.
Baadaye Wolper alirejea kwenye Ukristo huku mwenyewe akianika wazi kwamba, wazazi wake walimkemea sana kwa kitendo chake hicho cha kuingia kwenye Uislamu kwa ajili ya mwanaume huyo ambaye hata hivyo, baadaye waliachana kwa 'uhasama'.
Kama vile nia ya Wolper kuwa Muislamu imekuwa ikimea taratibu moyoni mwake, Februari mwaka huu, staa huyo aliandika bandiko mtandaoni akisema:
"Napenda sana kusikia Swala, Kaswida ya Kiislam. Nasisimkwa, nafurahia. Nakumbuka hadi nilitamani wanangu waijue hii dini pia. Ikiwemo na ya kwao (Ukristo). Sijui nakosea. Sijui ni nini?!
"But sometime hadi nalia kwa hisia ya nyimbo au maombi yenu. Mashallah keep praying. Tunapenda na tunaheshimu wengine huku."
Baadhi ya mashabiki zake mitandaoni wamekuwa wakisema kuwa, Wolper ana damu ya Kiislamu ndiyo maana anaingia na kutoka.
Wolper alipotakiwa kukiri au kukanusha maneno ya rafiki yake huyo alisema:
"Hayo mawazo siyo kwa mimi. Natamani watoto wangu ndiyo wajifunze maadili ya imani ya Kiislamu."
Alipoulizwa kama wazazi wake watakubali wajukuu zao wawe Waislamu, alijibu:
"Hawawezi kukataa. Hawa wajukuu siyo watoto wao. Hawana mamlaka nao. Mimi ndiyo mtoto wao."
Alipoulizwa kama baba wa watoto hao anajua matamanio yake kuhusu vijana wake, alisema:
"Mi sipendi kufanya kitu bila baba yake. Hata kama tumegombana, napenda kumuuliza kwanza baba yao maana yeye na mimi ndiyo wenye mamlaka, siyo bibi wala babu yao."