Naomba kujuzwa siri za Tausi kufugwa Ikulu

Mimi uwa naona hakuna jingine zaidi ya ubinafsi wa kundi dogo la watu wanaotaka siku zote wao waonekane kama ni tabaka teule linalostahili kuwa na kila kitu na wengine wasiwe na haki ya kuwa navyo hata kama uwezo wa kuvimiliki wako nao.
 
Nasubiri kwa hamu sana majibu kutoka kwa wahusika wa nyara za taifa kwani mimi nawatamani sana tangu nikiwa mtoto kuna wakati nilitamani kukamata vifaranga waliokuwa wanazagaa kwenye bustani ya maua pale shabani robert lakini wahudumu wa pale miaka hiyo ya 70s wakanionya kuwa ningesababisha wazazi wangu wafungwe kama ningepeleka vifaranga hao nyumbani.
Duu
 
Sasa wewe kumkubali ndio kunanifanya mie Nina roho ya kishetani? Sikiliza hii clip hapo chini ndio utajua roho ya kishetani anayo nani.

Msikilize JPM kisha sikiliza majibu ya JK kuhusu huyo mtumishi ambaye alikuwa na familia na ndugu wanao mtegemea. Kama una akili utaelewa kitu, lakini kama unatokea kundi lile la kusukumwa na hisia huwezi elewa

View attachment 1464004
Kama alijua anafamilia kwanini hakufanya kazi yake ipasavyo? Au ndiyo mazoea unasikilia sikio hili lingine linatoa nje maagizo? Uzembe wake atafanya kazi anayo iweza
 
Tausi wanauzwa mkuu ziko breeds aina mbili kuna weupe na weisi, tausi wanfugwa dana huko Duniani, Kenya hapo ni wengi tu, sisi ndo tuko lockdown tunona ni vitu vya ajabu
Kaka wapo Kenya hao aliopewa na Mzee MAGU walikuwa wanini!?
 
Nasubiri kwa hamu sana majibu kutoka kwa wahusika wa nyara za taifa kwani mimi nawatamani sana tangu nikiwa mtoto kuna wakati nilitamani kukamata vifaranga waliokuwa wanazagaa kwenye bustani ya maua pale shabani robert lakini wahudumu wa pale miaka hiyo ya 70s wakanionya kuwa ningesababisha wazazi wangu wafungwe kama ningepeleka vifaranga hao nyumbani.
Tausi ni watamu Sana kuliko ndege wa aina yoyote. Ndio maana ni special meal kwa ajili ya marais tu. Nyie wengine kuleni bundi🦉🦉
 
Kuna mama mmoja wa kizungu nlikuwa namuzia manyoya ya tausi alinambia, tausi jikee anavutiwa na tausi dume mwenye manyoya mengi
Kingine nlichoki expirience ni tausi hamuogopi mwanadamu unaweza msogelea fresh tu
Kingine hakuna wanyama watata kama tausi inapotekea mipaka shume inataka kuwazinguaaa
Mtiti wao si wa kitoto wakouanzisha

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kwani Kiongozi mfano akija Tanzania akapewa zawadi ya Kinyago, ni kwamba nchini mwale hakuna mwenye kinyago cha aina hiyo?

Uhuru kapewa kama Zawadi ya heshima, si kwamba au Uhuru hana uwezo wa kuwaagiza India hao tausi, kuna wafugaji Mombasa wanawauzaga sana facebook, milion 2 unapata dume na jike
Kaka wapo Kenya hao aliopewa na Mzee MAGU walikuwa wanini!?
 
Wasomi wa hivyo vyuo ni kujigamba tu hawana ubunifu hahah
Sijui kwanini watu wanapenda kukuza vitu vidogo kufanya mambo kuwa complicated unnecessarily hivi? Kabla ya Uhuru kulikuwa na tausi Temeke veterinary farm.
Uganda pia walikuwepo Makerere University na sehemu zingine.

Ndege hawa asili yao ni India na wako aina chache tofauti lakini sio rare species kama watu wanavyofikiri. Tanzania na hapa Dar es salaam kulikuwa na aina nyingi za ndege lakini baadhi ya hao wametoweka kutokana na kushambuliwa na kunguru mweusi.

Ingefaa hatua stahiki zichukuliwe kumwondoa kunguru mweusi ili kurudisha vizazi vya ndege wengine kama tetele, kasuku wadogo, shorwe, sparrows, dudumizi, kwasa, hata mwewe na kipanga.

JPM ameonyesha mfano kwa wataalamu wetu wa SUA na vyuo vinginevyo wafanyie kazi kurudisha ndege wa asili wa Tanzania katika miji yetu kwa faida ya vizazi vijavyo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom