Wanamgambo (RSF) wachukua Ikulu nchini Sudan

Mributz

Senior Member
Aug 29, 2022
112
388
Kikosi Maalum cha Wanamgambo nchini Sudan cha RSF, kimesema kimechukua udhibiti kamili wa Ikulu ya rais, makazi ya mkuu wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum.

Katika taarifa yake iliyotolewa hii leo Aprili 15, 2023 RSF imesema imechukua pia udhibiti wa viwanja vingine viwili vya ndege, kwenye mji wa kaskazini wa Merowe na mji wa El-Obeid ulioko upande wa kusini mwa nchi.

Kikosi hicho cha RSF kinachoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, maarufu kama Hemedti, kilisema jeshi lilizingira moja ya kambi zake na kufyatua risasi kwa kutumia silaha za kivita huku vyama vya kiraia vya Sudan vikitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano yaliyozuka baina ya vikosi hivyo viwili.

Vyama hivyo ambavyo vimesaini makubaliano ya awali ya kugawana madaraka na jeshi la nchi hiyo pamoja na kikosi cha RSF pia vimetoa wito kwa wadau wa kimataifa na kikanda kuchukua hatua haraka kuzuia umwagaji damu.

IMG_20230415_170054.jpg
 
tusiwapokee kamwe wakimbizi wa sudan. hawa jamaa wana chuki mbaya sana na wakristo.kuna hatari kubwa sana tukiwapokea watatuletea chuki ya kidini ambayo sisi hatjaizoea wala kuiona. niliwahi kusema hawa wasudan waliisha wahi kushangaa kuona watanzania hatuna kubaguwana kidini katika kila minuso tunachanganyana kwa smile kubwa sana! waache wakizipiga wakimbizi wao waishie somalia, saudis na senegal.
 
Wamekuambia wanataka kuja? Mbona hatupakani na Sudan?
 
Back
Top Bottom