Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,845
Mwezi uliopita kulitokea wizi wa ng'ombe wa Bw.Said Bafiki mkazi wa Nyamakala, wilayani Kasuku. Wakaletwa waganga (maarufu kama lambalamba) ili kubaini wahalifu. Ramli ilionesha vijana 6 wamehusika.
Vijana hao walikamatwa na polisi kwa tuhuma za wizi na walikaa wiki moja rumande wakipigwa na kuteswa bila kupelekwa mahakamani. Wananchi wakaandamana kushinikiza wapelekwe mahakamani. Polisi wakaahidi kuwapeleka tar.11/12 /2023 lakini hawakuwapeleka.
Kufuatia hali hiyo waananchi wakaamua kukata mti na kufunga barabara kuu ya kuingia mjini Kasulu kama njia ya kushinikiza vijana hao wapelekwe mahakamani au waachiwe huru. DC akaagiza vijana hao wasakwe.
Polisi wakaingia mtaani usiku wa manane kuwasaka. Wakaingia nyumba ya Bibi Tausi Ntaburugwa (65) ambaye ni mjane na mgonjwa wa sukari na presha. Bibi huyo anaishi na mabinti zake watatu ambao ndio wanaomuuguza. Polisi walipofika waliuvunja mlango na kuingia ndani, hali ambayo ilizua taharuki.
Walidai wanasaka vijana waliofunga barabara. Bi Tausi akasema nyumbani kwake hakuna vijana, anaishi na mabinti zake watatu. Polisi wakapita vyumbani na kusachi. Hata hivyo hawakumpata mtu yeyote wala kitu chochote chenye kuashiria uhalifu.
Polisi wakaanza kufanya uharibifu katika nyumba hiyo. Wakapiga risasi za moto juu na kuharibu paa la nyumba. Wakavunja TV, vioo vya madirisha, mambomba ya maji etc.
Kisha wakawapiga wale mabinti. Mama yao alipojaribu kuwatetea walimchania nguo na kumjeruhi na kitako cha bunduki mgongoni. Inadaiwa pia walipora vitu mbalimbali katika nyumba hiyo ikiwemo simu za mkononi na pesa taslimu.
#MyTake:
1. Je Polisi wameishiwa mbinu mpaka wanatumia waganga wa kienyeji kubaini wahalifu? Pale CCP wanafundishwa pia ulozi?
2. Polisi kwa "ujinga wao" wameangalia matokeo badala ya chanzo. Barabara ilifungwa ili kushinikiza watuhumiwa watendewe HAKI. Either wapelekwe mahakamani au waachiwe huru. Sio kuwashikilia tu.
3. Halafu TV, madirisha na mabomba ya maji vinahusikaje na kufunga barabara? Yani watu wamekata mti wakafunga barabara nyie mnaenda kuvunja TV? Askari kabisa wenye mafunzo? Tafadhali @hamadmasauni shughulika na hawa wanaotuharibia jeshi letu "tukufu" la Polisi. Anza na Kasulu.!
Sent using Jamii Forums mobile app