Naomba kujuzwa siri za Tausi kufugwa Ikulu

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,410
2,000
Wanajf, bila shaka popote linapotajwa jina la ndege aina ya Tausi, basi bila shaka moja kwa moja zinakuja fikra za kuwaza ikulu! Na hii ni kwa sababu, ndege hawa wamekuwa maarufu zaidi kufugwa kule magogoni,na hivyo si rahisi kuwakuta sehemu nyingine kama majumbani au hata katika mbuga zetu!Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere bila shaka ndiye aliyekuwa muasisi wa kuwafuga hawa ndege aina ya Tausi ikulu, na Marais waliofutia wote waliendeleza utamaduni wa kuwafuga na kuwatunza!

Katika awamu hii, Rais Magufuli amekuwa akiwahusudu sana hawa ndege na inaonyesha anawapenda sana! Alimpa Rais wa Kenya, Mh. Kenyata lakini vile vile alimpa masharti baada ya kumpatia!

Katika ikulu mpya inayotengenezwa Dodoma, amehakikisha hawa ndege wanakuwa katika eneo hilo ili kuenzi utamaduni wa kuwafuga ambao ulianzishwa na Baba wa taifa!

Sasa, je hawa ndege tofauti na umbo lao la kuvutia ni sababu gani hawa ndege inawafanya wawe maarufu hivi, kiasi cha kufikia kufugwa tu ikulu?

Ni kwa nini hawa ndege hugawiwa viongozi wakubwa tu, mfano Rais mstaafu Kikwete ametangaza kupewa na Rais Magufuli, pamoja na familia ya Hayati Mwalimu Nyerere?

Je kuna siri gani juu ya hawa ndege inayowafanya watunzwe kwenye maeneo sensitive kiasi hicho?
Vipi, kuna watu binafsi wanaowafuga kama bata, kuku n.k?

Je, raia wa kawaida akitaka kuwafuga, kuna utaratibu wa kufuata ili awapate, na atawapata wapi zaidi ya ikulu? Wanajf, naamini hiki ni kisiwa cha maarifa, na wapo wajuvi wanaojua kuhusu hili, hebu mtutoe tongotongo tafadhali!
 

Ngararimu

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
235
500
Nasubiri kwa hamu sana majibu kutoka kwa wahusika wa nyara za taifa kwani mimi nawatamani sana tangu nikiwa mtoto kuna wakati nilitamani kukamata vifaranga waliokuwa wanazagaa kwenye bustani ya maua pale shabani robert lakini wahudumu wa pale miaka hiyo ya 70s wakanionya kuwa ningesababisha wazazi wangu wafungwe kama ningepeleka vifaranga hao nyumbani.
 

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,410
2,000
Nasubiri kwa hamu sana majibu kutoka kwa wahusika wa nyara za taifa kwani mimi nawatamani sana tangu nikiwa mtoto kuna wakati nilitamani kukamata vifaranga waliokuwa wanazagaa kwenye bustani ya maua pale shabani robert lakini wahudumu wa pale miaka hiyo ya 70s wakanionya kuwa ningesababisha wazazi wangu wafungwe kama ningepeleka vifaranga hao nyumbani.

Duh, ina maana kuna siri nyuma ya pazia kuwahusu hawa ndege?

... wanatofauti gani na kasuku au kanga, maana hawa unaweza kuwakuta majumbani mwa watu wa kawaida!
Naamini majibu humu tutayapata!
 

MANIAJE

Senior Member
Aug 18, 2019
142
500
Duh, ina maana kuna siri nyuma ya pazia kuwahusu hawa ndege?
... wanatofauti gani na kasuku au kanga, maana hawa unaweza kuwakuta majumbani mwa watu wa kawaida!
Naamini majibu humu tutayapata!
think ni pambo tuu. Njoo moshi maeneo ya SHANT TOWN kuna watu kibao tuu wanawafuga. Muasisi wa ufugaji wa tausi katika eneo la shant town ni mzungu mmoja almaarufu BUNDI.
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
50,137
2,000
Kitambo sana nlipata mchongo wa kutafuta manyoya ya tausi, Enzi hizo ocean road jengo ni pagale watu walikuwa wanaogopa Kuingia Ndani mule tausi walikuwa wanaacha manyoya yao.

Nikikusanya nlikuwa nawapelekea wazungu Kuwauzia, Kuna siku nkaingia kwenye 18 za walinzi wa NIMR walinzi Walibana Mara Akaja boss wao namkumbka Jina profesa kilama wakawa wanatuhoji.

Nkampa mchakato akaingia line maana tulikuwa machali akasema waachienii Hawa, mbona Watoto wadogo lkn masharp shooter, tukaachiwa.

Ila manyoya yke kwa decoration si mchezo

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,410
2,000
think ni pambo tu. Njoo Moshi maeneo ya SHANT TOWN kuna watu kibao tuu wanawafuga. Muasisi wa ufugaji wa tausi katika eneo la shant town ni mzungu mmoja almaarufu BUNDI.

Okey, hao waliopo Moshi wanafugwa na wazawa au ni huyo mzungu bado/wazungu wengine au familia yake? Kama ni wazawa waliwapataje? Kuna utaratibu wowote wa kufuata ili kuwapata?

Na kama si wazawa, ni kwa nini iwe hivyo? Lakini pia hata kama ni wazawa wa hayo maeneo ya Shant town, je maeneo mengine kama majengo, Kiborloni, Himo n.k ni kwa nini hawafugwi huko...!?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom