Naomba kujuzwa siri za Tausi kufugwa Ikulu

Huko Mbali South Africa wako kibao tu au Botswana au Zambia hapo
Hawa ndege ukienda India na Sri Lanka wapo wengi tu. Huwa najiuliza kama mtu akienda India na kuwanunua, na akawaleta nchini kuwafuga ataruhusiwa au ndiyo yale yale ya ''nyara za Taifa''?
 
I think ni pambo tu. Njoo Moshi maeneo ya SHANT TOWN kuna watu kibao tu wanawafuga. Muasisi wa ufugaji wa tausi katika eneo la Shant Town ni mzungu mmoja almaarufu BUNDI.
Shanty town maeneo gani,karibu na international School au na maghorofa ya bima ?
 
Sijui kwanini watu wanapenda kukuza vitu vidogo kufanya mambo kuwa complicated unnecessarily hivi? Kabla ya Uhuru kulikuwa na tausi Temeke veterinary farm.
Uganda pia walikuwepo Makerere University na sehemu zingine.

Ndege hawa asili yao ni India na wako aina chache tofauti lakini sio rare species kama watu wanavyofikiri. Tanzania na hapa Dar es salaam kulikuwa na aina nyingi za ndege lakini baadhi ya hao wametoweka kutokana na kushambuliwa na kunguru mweusi.

Ingefaa hatua stahiki zichukuliwe kumwondoa kunguru mweusi ili kurudisha vizazi vya ndege wengine kama tetele, kasuku wadogo, shorwe, sparrows, dudumizi, kwasa, hata mwewe na kipanga.

JPM ameonyesha mfano kwa wataalamu wetu wa SUA na vyuo vinginevyo wafanyie kazi kurudisha ndege wa asili wa Tanzania katika miji yetu kwa faida ya vizazi vijavyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua madhara ya kuwaonfoa hao kunguru weusi.

Ujui ni miongoni mwa wafanyausafi wa jiji.
Bila kunguru weusi kuwepo uchafu ungetapakaa kila kona kila eneo la jiji.
 
Tausi wanauzwa mkuu ziko breeds aina mbili kuna weupe na weisi, tausi wanfugwa dana huko Duniani, Kenya hapo ni wengi tu, sisi ndo tuko lockdown tunona ni vitu vya ajabu
Okey, hao waliopo Moshi wanafugwa na wazawa au ni huyo mzungu bado/wazungu wengine au familia yake? Kama ni wazawa waliwapataje? Kuna utaratibu wowote wa kufuata ili kuwapata?

Na kama si wazawa, ni kwa nini iwe hivyo? Lakini pia hata kama ni wazawa wa hayo maeneo ya Shant town, je maeneo mengine kama majengo, Kiborloni, Himo n.k ni kwa nini hawafugwi huko...!?
 
Labda Ndege john au turkey
Hao hapo weupe
images%20-%202020-05-30T173951.209.jpeg
 
Aruhusu kivipi? Arusha kuna watu wanao mbona ? Kwa hiyo unazania Tanzania ni Ikulu pekee ndo kuna Tausi?
Acha wivu huyu kawakuta wachache tena wameterekezwa wajiokotee chakula na kutaga hovyo vichakani na mayai kuliwa na nguchiro na kenge. Muhudumu msukuma akiagizwa na kikwete anunue incubetor azalishe wawe wengi kagoma.

Yeye kafika kamfukuza mtunza tausi kaweka mtunzaji, kaleta incubator, kazalisha na ziada. Wengine ka export, wengine kawagawia watangulizi wake, wengine kajigawia wegine zaidi ya 1400 kapeleka ikulu ya chamwino bado stock ya magogoni ipo ya kutosha.

Ulitakaje?. Acha roho ya kishetani. Mimi huyu JPM namkubali sana. Sasa aruhusu kila anayetaka kufuga na ana eneo afuge tuu shida ni nini kwani?.
 
Kuna Congo peafowl wanapatikana Mto kongo huko,
Sijui kwanini watu wanapenda kukuza vitu vidogo kufanya mambo kuwa complicated unnecessarily hivi? Kabla ya Uhuru kulikuwa na tausi Temeke veterinary farm.
Uganda pia walikuwepo Makerere University na sehemu zingine.

Ndege hawa asili yao ni India na wako aina chache tofauti lakini sio rare species kama watu wanavyofikiri. Tanzania na hapa Dar es salaam kulikuwa na aina nyingi za ndege lakini baadhi ya hao wametoweka kutokana na kushambuliwa na kunguru mweusi.

Ingefaa hatua stahiki zichukuliwe kumwondoa kunguru mweusi ili kurudisha vizazi vya ndege wengine kama tetele, kasuku wadogo, shorwe, sparrows, dudumizi, kwasa, hata mwewe na kipanga.

JPM ameonyesha mfano kwa wataalamu wetu wa SUA na vyuo vinginevyo wafanyie kazi kurudisha ndege wa asili wa Tanzania katika miji yetu kwa faida ya vizazi vijavyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kwanini watu wanapenda kukuza vitu vidogo kufanya mambo kuwa complicated unnecessarily hivi? Kabla ya Uhuru kulikuwa na tausi Temeke veterinary farm.
Uganda pia walikuwepo Makerere University na sehemu zingine.

Ndege hawa asili yao ni India na wako aina chache tofauti lakini sio rare species kama watu wanavyofikiri. Tanzania na hapa Dar es salaam kulikuwa na aina nyingi za ndege lakini baadhi ya hao wametoweka kutokana na kushambuliwa na kunguru mweusi.

Ingefaa hatua stahiki zichukuliwe kumwondoa kunguru mweusi ili kurudisha vizazi vya ndege wengine kama tetele, kasuku wadogo, shorwe, sparrows, dudumizi, kwasa, hata mwewe na kipanga.

JPM ameonyesha mfano kwa wataalamu wetu wa SUA na vyuo vinginevyo wafanyie kazi kurudisha ndege wa asili wa Tanzania katika miji yetu kwa faida ya vizazi vijavyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vizazi vijavyo vitafaidika kwa namna gani? Nieleweshe tafafhali
 
tausi tausi tu hakuna nyuma ya pazia wala mbele ya pazia izo n mila na utamaduni wa kiafrika ambayo wenzetu wa dunia ya kwanza wanatushangaa tunapokaa na kuanza kukabidhiana mambo ambayo hana maana kwa dunia ya sasa
Mbona huko kwao, bustani za wanyama, yaani Zoo.

Hata huku kwetu hifadhi zetu, soko kubwa tunategemea kutoka kwao, iweje leo wanyama wasiwe na maana, mpaka wazungu watushangae kwa kutunza wanyama.
 
Hao Tausi wala sio wa kuwalilia, wakijazana usiku hamtalala, wanapiga sana kelele

Nashangaa wanawapendea nini kama sio kukaribisha vicheche na kelele usiku bila sababu, bora mtu kama JMK angefuga nguchiro ambao wangemsaidia kula nyoka kule porini Msoga
 
Wanajf, bila shaka popote linapotajwa jina la ndege aina ya Tausi, basi bila shaka moja kwa moja zinakuja fikra za kuwaza ikulu! Na hii ni kwa sababu, ndege hawa wamekuwa maarufu zaidi kufugwa kule magogoni,na hivyo si rahisi kuwakuta sehemu nyingine kama majumbani au hata katika mbuga zetu!Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere bila shaka ndiye aliyekuwa muasisi wa kuwafuga hawa ndege aina ya Tausi ikulu, na Marais waliofutia wote waliendeleza utamaduni wa kuwafuga na kuwatunza!

Katika awamu hii, Rais Magufuli amekuwa akiwahusudu sana hawa ndege na inaonyesha anawapenda sana! Alimpa Rais wa Kenya, Mh. Kenyata lakini vile vile alimpa masharti baada ya kumpatia!

Katika ikulu mpya inayotengenezwa Dodoma, amehakikisha hawa ndege wanakuwa katika eneo hilo ili kuenzi utamaduni wa kuwafuga ambao ulianzishwa na Baba wa taifa!

Sasa, je hawa ndege tofauti na umbo lao la kuvutia ni sababu gani hawa ndege inawafanya wawe maarufu hivi, kiasi cha kufikia kufugwa tu ikulu?

Ni kwa nini hawa ndege hugawiwa viongozi wakubwa tu, mfano Rais mstaafu Kikwete ametangaza kupewa na Rais Magufuli, pamoja na familia ya Hayati Mwalimu Nyerere?

Je kuna siri gani juu ya hawa ndege inayowafanya watunzwe kwenye maeneo sensitive kiasi hicho?
Vipi, kuna watu binafsi wanaowafuga kama bata, kuku n.k?

Je, raia wa kawaida akitaka kuwafuga, kuna utaratibu wa kufuata ili awapate, na atawapata wapi zaidi ya ikulu? Wanajf, naamini hiki ni kisiwa cha maarifa, na wapo wajuvi wanaojua kuhusu hili, hebu mtutoe tongotongo tafadhali!
Nyie endeleeni kuwaona kama ndege wa kawaida tu...
 
Back
Top Bottom