Naomba kujuzwa C.V ya Mwalimu Christopher Mwakasege

Naomba kujuzwa C.V ya Mwalimu Christopher Mwakasege

Ukisoma Biblia kwa kukariri kila kitakachofundishwa huwezi kuelewa, Biblia ni MUNGU mwenyewe katika roho mtakatifi we baki na dini yako(Theology) waache wanaotafuta ufalme wa MUNGU.

Jamani mtumishi hivi kweli unaweza kukariri biblia?
Hebu tafuta maana ya theology na usikariri
 
Na wakati anaanza kazi ya ualimu miaka 30 iliyopita alikuwa hana hela ya kutosha hata kabati yao ya kwanza waliokota yeye na mkewe wakati hoteli walipoitupa kwa ajili ya ukarabati
 
Niliwahi kusikia huyo Mwakasege ni Mchumi by professional, alisomea uchumi na kufanyakazi za kushauri
Mambo ya uchumi mkubwa na mdogo(Macro&Micro Economy), Mwenyeji wa Mbeya lakini Anaishi mkoani Arusha.
Anaitwa Mwalimu kulingana na kipawa chake ulichopewa na Mwenyezi Mungu, na pia ukimsiliza anapoongea utagundua anafundisha na sio kuhubiri. Jamaa nasikia ni muumini wa kawaida sana kwenye ukristo.

Hivi hatuwezi mshawishi akawa na darasa huru huku kwa muda fulani manake kina vitu akifundisha katika ulimwengu wa kiroho huwa vinafungua sana.
 
kuna kitu sielewi kwa mwakasege je yeye anasali wapi jpili kkkt au makanisa ya pentekoste na je najua ana elimu ya uchumi je hii ya neno la Mungu anayo hata certificate?maana hata kama una kipaje elimu ina umuhimu kupunguza makosa flaniflani ktk kutafsiri neno la Mungu.

Mwakasege yeye jpili huwa anasali K.K.K.T na sio makanisa ya Pentekoste labda kwa mwaliko maalumu.. ila yeye ana sali K.K.K.T
 
Hyo Siyo Hoja! hata enzi zile Yesi anafundisha aliitwa Rabi(Mwalimu) na hapo ndio mafarisayo, waandishi n wanasheria wa enzi walipohoji kuwa kwa nini anafundisha Neno la Mungu mtu ambaye amekuwa wakimuona hajaenda chuo chochote cha sheria za dini zaidi ya Uselemala aliokuwa akifanya na baba ya Yusufu (ndio maana walimuita Mtoto Wa Selemala).
 
Mwakasege yeye jpili huwa anasali K.K.K.T na sio makanisa ya Pentekoste labda kwa mwaliko maalumu.. ila yeye ana sali K.K.K.T

Huyo anataka wazungu! mimi na weusi wangu wa kuchomwa najua nachuga ng'ombe nitamuweza kweli.?CC Mtoto halali na hela
 
Last edited by a moderator:
Because he teaches the word of God not preaching.
Hii thread ni kuhusu mwakasege au heka heka ulizokumbana nazo siku ya leo mfugaji.

Back to topic na mimi ningependa kujua kwa nini wanamwita mwalimu...
 
Jamani mtumishi hivi kweli unaweza kukariri biblia?
Hebu tafuta maana ya theology na usikariri
Si umemsikia amesema mwenyewe hapo. Ndiyo maana hata vifungu vinavyofundishwa na Mwl Mwakasege havielewi( kwa maana nyingine kama vile Mwalimu ametunga Biblia yake).
 
Professionally ni mwanauchumi ila pia ni mwalimu wa neno la Mungu ndo maana anaitwa mwalimu!
Sio mchungaji wala mwinjilisti ila ni Mwalimu!

Mungu amegawa vipawa mbalimbali moja wapo ni kufundisha,Mwalimu Mwakasege amepewa kazi ya kufundisha au kiingereza tunaita WORD!kuna watumishi wa Mungu ambao kwa kweli wamepewa unabii kufundisha siyo kazi yao lakini nashangaa wanalazimisha sana kufundisha nafikiri huko ni kuharibu kazi ya Mungu,ebu fikiria Mwalimu aanze kutabiri tatizo ni kwamba siyo kazi au kipawa alichopewa,hongera sana kwa kujifunza neno maana ndiyo wajibu wa Mkristo safi
 
mijitu mingine mipuuzi sana, mnamuabudi mwakasege au yesu, yaani kika kukicha mwaksege, sijui gwajima, huo ndio udogmatism, ni sawa na mbwa kumfwata master wake popote anapoenda mbwa hufuata. Rekebikeji jishughulisheni acheni, kupoteza muda, mnampa gwajima na lwakatare ulaji. Waumini mnakuwa mitaji wa watu

Muabudu Mungu achaneni na binadamu wenzenu.

wapagani utawajua kwenye mada kama hizi wanatokwa na povu jingi
 
Ukristo wako unahojika kwa kutukana watu wajinga,ukilazimisha watu wakubali mtazamo wako!!! Tabia mbaya kutukana watu
Kajifunze lugha. Mjinga ni mtu asiyejua. Siyo tusi labda kwa mtu mpumbavu ambaye hajui na hajui kuwa hajui. Ukichukua kioo utamuona
 
Hivi hatuwezi mshawishi akawa na darasa huru huku kwa muda fulani manake kina vitu akifundisha katika ulimwengu wa kiroho huwa vinafungua sana.

Unamaanisha humu humu jf ama? Labda akina khatan & co wapigwe ban ya maisha
 
Hivi hatuwezi mshawishi akawa na darasa huru huku kwa muda fulani manake kina vitu akifundisha katika ulimwengu wa kiroho huwa vinafungua sana.

Kwani hupajui kanisani kwake. Mnataka kutuletea ukafiri huku Jukwaanin
 
hakika huyu n mtumishi wa Mungu aliyehaii,,, Mungu atamvisha taji yake,, Natoa wito kwa Wanazuoni,, wasomi na vyuo vikuu nche na ndani ya nchi hiii kumtunuku phd ya heshima hakika huyu n Dr mwakasege...
 
Back
Top Bottom