Naomba kujuzwa C.V ya Mwalimu Christopher Mwakasege

Naomba kujuzwa C.V ya Mwalimu Christopher Mwakasege

Haya mwalimu Mwakasege amesoma chuo cha Mipango Dodoma wakati kikianzishwa kutoka Chuo cha Mzumbe na ni miongoni mwa wahitimu wa mwanzo wa chuo hicho ambapo walimaliza kozi yao ya Regional Planning miaka ya 80 na wakafanya Post Graduate ya kozi hiyo mipango hapo hapo wakati huo kikihama kwenda Dodoma Area C kikitokea Morogoro, darasa lao wengi wamestaafu wakiwa Ma-DED na makatibu wakuu kwenye wizara, lakini amejiimarisha kwenye taaluma ya uchumi kwa kozi mbalimbali nje ya nchi na niliambiwa wakati fulani alikuwa ni miongoni mwa washauri wa masuala ya uchumi kwa Mkulu enzi zile za Benny na yupo vizuri kwenye maeneo ya mipango ya maendeleo na uchumi
hajawahi kusoma SUA huyu? niliwahi kumsikia kwenye mikutano yake ya semina kuwa amemaliza SUA, sina uhakika na course ila nahisi ni Agricultural economics and agribussines
 
mijitu mingine mipuuzi sana, mnamuabudi mwakasege au yesu, yaani kika kukicha mwaksege, sijui gwajima, huo ndio udogmatism, ni sawa na mbwa kumfwata master wake popote anapoenda mbwa hufuata. Rekebikeji jishughulisheni acheni, kupoteza muda, mnampa gwajima na lwakatare ulaji. Waumini mnakuwa mitaji wa watu

Muabudu Mungu achaneni na binadamu wenzenu.

Kunamtu hapa umeona ameandika kwamba yeye anamwabudu mwakasege..??
 
Tatizo kubwa katika semina ya Leo alifundisha kitabu cha ufunuo 13 kuhusu mnyama, joka na viti vya enzi. Kwa ujumla na kwa sababu watu wengi hawajui. Alitafsiri neno out of context. Mie nimesoma theology. Mengi ya maneno yake yalikuwa siyo biblical centred. Ndiyo ule ujanjaujanja wa kutumia vifungu vya biblia kujineemesha. It is bible and bible alone(sola Scripture )
Some serve God by SPIRIT, some by Profession!
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Karibuni kwenye semina ya MWAKASEGE inayoanza leo Mbeya kwenye viwanja vya ottu
 
Tukimaliza ya Mwakasege... Wengine tunaomba cv ya Mshenga wa Dr. Slaa...... Mzee wa kufufua wafu J. Gwajima....
 
Chuo cha mipango alisoma lini? Mwakasege mzaliwa wa Mkoa wa Mbeya, ambaye ndoa yake imefikisha miaka 30 leo, alisoma University of Dar es salaam lakini kwa Faculty of Agriculture ambayo sasa tunaiita SUA. Mwakasege ni mtaalamu wa Agrieconomy.
Amewahi kuwa Mshauri wa Rais kwenye masuala ya Uchumi wakati wa kipindi cha Benjamin Mkapa. Ana ofisi zake Arusha zinazojihusisha na utafiti na masuala ya Uchumi pamoja na huduma yake ya MANA.
Ni kweli alisoma SUA bythen akafanya post graduate diploma chuo cha mipango ndo walioanzisha post graduate ya regional planning ya Irdp nimeona kwenye orodha ya disertation zao
 
Acha kuclem Yesu alisoma Theology?
Weka alichhongea na weka chako tuchambue apa.
Roho wa Mungu anatenda kazi na kumpa iyo talanta Mwakasege kama mwalimu no wonder haubiri kanisa wala dini.
 
maze nimekuelewa tatizo la mwakasege anaubili kwa mtazamo wake anavyoona sio jinsi neno lilivyo.
Kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu not otherwise.
Inabidi siku nije wapa watu dose ya kazi za roho mtakatifu
 
Hyo Siyo Hoja! hata enzi zile Yesi anafundisha aliitwa Rabi(Mwalimu) na hapo ndio mafarisayo, waandishi n wanasheria wa enzi walipohoji kuwa kwa nini anafundisha Neno la Mungu mtu ambaye amekuwa wakimuona hajaenda chuo chochote cha sheria za dini zaidi ya Uselemala aliokuwa akifanya na baba ya Yusufu (ndio maana walimuita Mtoto Wa Selemala).
Theologians wa enzi zile pharisees na masadukayo walimdis Yesu kwa kuwa hakuwa theologian kama wao ingawa alikuwa anatema madini kuliko wao.
No wonder wakapanga njama za kumuua
 
Leo 08 Sept 21, Mwalimu wa NENO LA MUNGU, C.Mwakasege anaendesha semina ya Neno La Mungu Huko jijini Mwanza.

SIIJUI CV YAKE, Lakini nitaeleza machache kumuhusu yeye.
1.Anaitwa Christopher Angumbwike Mwakasege, Mzaliwa wa mkoa wa mbeya mwishoni mwa miaka ya 1950. Kwao watoto wote ni wanaume.

2.Kwa sasa anaishi jijini Arusha, ameoa na pia ana watoto, Yeye na familia yake wanasali K.K.K.T usharika wa kijenge.

3.Kitaaluma Mwalimu C.Mwakasege ni mbobezi katika masuala ya uchumi, amekwisha wahi fanya kazi serikalini na kwenye mashirika binafsi kama Mwanauchumi.

4.Licha ya kuwa mwana uchumi kitaaluma, Kiroho Mungu amempa kazi ya kulea kundi lake kwa KUFUNDISHA NENO LAKE (Neno la Biblia) na ndio maana huitwa Mwalimu, moja ya utambulisho wake ukiachilia mbali sauti yake yenye mamlaka juu ya mapepo na mashetani, Mwalimu mwakasege utamfahamu pale anaposema "Wengine wanasema Mwakasege Unaongea kitu gani?" Kisha hujijibu kwa kusema "Kasome Biblia yako".

5.Mwisho, tumuombee kwa Mungu ili aendelee kumtumia kusudi tupate yaliyo matakatifu kwaajili ya roho zetu.
 
Back
Top Bottom