Mtoto wa kiume wa mwl. Christopher Mwakasege afariki dunia hospitali ya Agha Khan

Veyron

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
572
373
Mtoto wa kiume wa mwalimu wa neno la mungu kutoka Arusha, Christopher Mwakasege aitwaye Joshua Mwakasege amefariki katika hospital ya Agha Khan baada ya kuugua ghafla akitokea kazini kwake.

Habari za awali zinasema alijisikia vibaya ghafla na kukimbizwa hospitalin hapo ambapo madaktari walijaribu kupigania uhai wake lakini ilishindikana hivyo kupelekea umauti!

Taarifa kutoka msemaji wa familia zinasema mazishi yatafanyika Alhamisi tarehe 18 Oktoba 2018 Tukuyu Mbeya.


''"Alhamisi usiku tulifiwa na Mtoto wetu Joshua, alifariki ghafla, halikuwa jambo lepesi kwamba tuendelee na semina au tusiendelee, kwa jinsi ya binadamu halikuwa jambo rahisi kuendelea na semina. Biblia inatuambia tuwe tayari wakati unaofaa na usiofaa''. Mwakasege


RATIBA YA MAZISHI

Ratiba rasmi ya safari ya mwisho ya Joshua Christopher Mwakasege kama ilivyotangazwa msibani na ibadani Mbezi Beach, Dar

Mwalimu Christopher Mwakasege amemaliza semina leo Jumapili Mbeya na kesho Jumatatu tarehe 15 Oct 2018 atasafiri kuja Dar kwenye msiba wa mwanae Joshua.

_NB: Mbali ya kufiwa na mwanae mpendwa lakini Mwalimu Mwakasege ameiheshimu na kuikamilisha ratiba ya Mungu ya semina._

Mahali ulipo msiba
Msiba uko Dar kwa mdogo wake Mwalimu Mwakasege anaitwa Eng. Mwakasingila (Mzee wa kanisa wa KKKT Mbezi Beach)

Jinsi ya kufika msibani
Fika hadi Mbezi Beach Jogoo, unaingia barabara ya Karibu Art Gallery kuelekea _TAG Mbezi beach_ kisha utaona vibao vinavyoelekeza msiba ulipo.

Ratiba ya Jumatatu
Kutakuwa na sara ya pamoja na Mwalimu Mwakasege na familia yeke yote itakayofanyikia hapa msibani itakayoanza saa moja jioni, 7pm itakayoongozwa na Askofu , Mchungaji kiongozi na watumishi wengine

Kuaga Mwili wa marehemu utaagwa Jumanne 16 Oct kanisani _KKKT Mbezi Beach Dar_, kuanzia saa nane mchana (2pm)
Baada ya kuaga mwili utapelekwa airport kwa ajili ya maandalizi ya safari.

Kusafirisha: Mwili utasafirishwa _Jumatano_ 17 Oct kwa ndege

Mazishi: Yatafanyika alhamisi, Tukuyu, Mbeya 18 Oct

Muhtasari:
Joshua amefariki ghafla baada ya kudondoka alhamisi tarehe 11 Oct 2018 akiwa kazini kwake World Bank Dar. Alikimbizwa Aga Khan hospital ila alifariki siku hiyo hiyo usiku.

Amefariki akiwa na miaka 25 na ni mtoto pekee wa kiume na wa mwisho wa Mtumishi wa Mungu Mwakasege.

Twendelee kumwombea Mwalimu Mwakasege na familia yake
d64d6b75-915d-4ab7-aaba-da361cec486e.jpeg

====

Mwalimu Mwakasege athibitisha kifo cha Mtoto wake Joshua rasmi Mazishi kufanyika Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya Siku ya Alhamisi October 18 “Nikweli siku ya Alhamisi tulipata taarifa ya Kifo cha mtoto wetu nadhani wengine mtakuwa mlipata taarifa kupitia mitandao ya Kijamii na Msio fahamu mtoto wetu huyo Anaitwa Joshua alifariki ghafla ,kwa jinsi ya Kibinadamu haikuwa rahisi kuendelea na semina hii lakini Bibilia inasema uwe tayari kwa wakati unao faa na usio faa na kwa jinsi ya kibinadamu haikuwa rahisi kuendelea na huduma hii na jambo hili hatukulitaka kulitangaza hili mapema tusiangushe roho ya Huzuni wakati kuna kitu Mungu anataka kuendelea Kuachia katikati ya wote ,mazishi ya msiba huu yatakuwa alhamisi mjini Tukuyu Wilayani Rungwe”Alisema Mwalimu Mwakasege. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN
 

Tumia akili

Member
Apr 1, 2013
66
987
Shalom all.
Mwenzetu Joshua Mwakasege aliugua ghafla jana wakati akitoka kazini Na alipelekwa Agha Khan hospital Emergency Na doctors walijitahidi kufanya resuscitation haikuwezekana na akafariki.
Tuiombee familia na kukiwa na taarifa zozote tutawajulisha. Mwalimu Mwakasege amefiwa na Yule kijana wake wa kiume wa pekee.
 

ThaGreatman

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
709
1,451
Shalom all.
Mwenzetu Joshua Mwakasege aliugua ghafla jana wakati akitoka kazini Na alipelekwa Agha Khan hospital Emergency Na doctors walijitahidi kufanya resuscitation haikuwezekana na akafariki.
Tuiombee familia na kukiwa na taarifa zozote tutawajulisha. Mwalimu Mwakasege amefiwa na Yule kijana wake wa kiume wa pekee.
Fafanua vizuri mkuu,mzee mwakasege alikuwa na mtoto mmoja pekee??
 

Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,493
1,841
Nasikitika kuwafahamisheni msiba wa mtoto wa Mwl Christopher Mwakasege ( Joshua) amefariki.

Alidondoka jana akitoka kazini, alipoteza fahamu na leo amefariki muda mfupi uliopita.
Mwalimu ana semina mkoa wa Mbeya na ndiyo mtoto pekee wa kiume. Hakika sio pito jepesi.
Tuwakumbuke kwenye maombi. RIP JOSHUA CHRISTOPHER MWAKASEGE.
 
27 Reactions
Reply
Top Bottom