Naomba kujuzwa C.V ya Mwalimu Christopher Mwakasege

Naomba kujuzwa C.V ya Mwalimu Christopher Mwakasege

Shy land

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
6,245
Reaction score
2,856
Ndugu wanaJF husukieni na kichwa cha habari hapo juu. Naomba mtu anayefahamu vizuri curriculum vitae ya mwalimu Christopher Mwakasege anijuze, nasema hivyo maana leo nimejitahidi kuhudhuria semina yake pale viwanja vya jangwani vinavyojaa mafuriko wakati wa masika, kwa kweli sijawahi kukutana na mtumishi wa Mungu anayejua kuhubiri na kufundisha kama yeye.

Lakini pia namshukuru MUNGU Ameniepusha kuniharibia siku yangu kwa sababu ya washabiki wenzangu wa yanga pale makao makuu.

Kosa nimechomekea shati langu jekundu nikitoka kwenye semina nikielekea Kariakoo kwenye hoteli (kwa sababu za kibashara sitaitaja, nilipofika wanayanga nikawakuta wamekusanyika nikaona nipite nisikilize matokeo na uchambuzi, niliposimama tu wakanitaka nipotee yale mazingira nikakataa ndio walipotaka wanipige.

Nikiwa namsubiri atakayeaza kunipiga huku wakinitusi, mara gari ya police ikiwa kwenye patrol wakanitaka niondoke tu.

Namshukuru sana Mungu maana leo washabiki wezengu wa yanga wagenijua mimi ndiye mchunga ng'ombe.
 
Hii thread ni kuhusu mwakasege au heka heka ulizokumbana nazo siku ya leo mfugaji.

Back to topic na mimi ningependa kujua kwa nini wanamwita mwalimu...

Nimeeleza hivyo ili uone njisi nilivyopokea upako kwa mumishi wa Mungu, na mungu kanisaidia kaepusha shari yakuwaduga makonde washabiki wezangu wa yanga.
 
Hii thread ni kuhusu mwakasege au heka heka ulizokumbana nazo siku ya leo mfugaji.

Back to topic na mimi ningependa kujua kwa nini wanamwita mwalimu...

Mtoa mada.
Mwalimu Mwakasege ni mchumi wa daraja la juu na amehudhuria makongamano mengi ya kitaifa na kimataifa. Na kutoa mchango wake kama mchumi.

Kwa H.O.E
Anaitwa mwalimu kwasababu huduma yake ni ualimu na sio uchungaji. Ndio maana hana kanisa na hata mikutano mingi hualikwa ili akafanye huduma ya ualimu kupitia huduma yake ya MANA.
 
Professionally ni mwanauchumi ila pia ni mwalimu wa neno la Mungu ndo maana anaitwa mwalimu!
Sio mchungaji wala mwinjilisti ila ni Mwalimu!

Mkuu kama unamjua vizuri tueleze na Heaven on Earth, kwamba alizaliwa wapi? alikulia wapi? pamoja na elimu alivyosoma hadi alipo,? tutashukuru mkuu
 
Last edited by a moderator:
Haya mwalimu Mwakasege amesoma chuo cha Mipango Dodoma wakati kikianzishwa kutoka Chuo cha Mzumbe na ni miongoni mwa wahitimu wa mwanzo wa chuo hicho ambapo walimaliza kozi yao ya Regional Planning miaka ya 80 na wakafanya Post Graduate ya kozi hiyo mipango hapo hapo wakati huo kikihama kwenda Dodoma Area C kikitokea Morogoro, darasa lao wengi wamestaafu wakiwa Ma-DED na makatibu wakuu kwenye wizara, lakini amejiimarisha kwenye taaluma ya uchumi kwa kozi mbalimbali nje ya nchi na niliambiwa wakati fulani alikuwa ni miongoni mwa washauri wa masuala ya uchumi kwa Mkulu enzi zile za Benny na yupo vizuri kwenye maeneo ya mipango ya maendeleo na uchumi
 
Niliwahi kusikia huyo Mwakasege ni Mchumi by professional, alisomea uchumi na kufanyakazi za kushauri
Mambo ya uchumi mkubwa na mdogo(Macro&Micro Economy), Mwenyeji wa Mbeya lakini Anaishi mkoani Arusha.
Anaitwa Mwalimu kulingana na kipawa chake ulichopewa na Mwenyezi Mungu, na pia ukimsiliza anapoongea utagundua anafundisha na sio kuhubiri. Jamaa nasikia ni muumini wa kawaida sana kwenye ukristo.
 
shy land kumbe ndo ww uliekua unasumvuliwa na wanayanga pale au ni mwingine?
 
Haya mwalimu Mwakasege amesoma chuo cha Mipango Dodoma wakati kikianzishwa kutoka Chuo cha Mzumbe na ni miongoni mwa wahitimu wa mwanzo wa chuo hicho ambapo walimaliza kozi yao ya Regional Planning miaka ya 80 na wakafanya Post Graduate ya kozi hiyo mipango hapo hapo wakati huo kikihama kwenda Dodoma Area C kikitokea Morogoro, darasa lao wengi wamestaafu wakiwa Ma-DED na makatibu wakuu kwenye wizara, lakini amejiimarisha kwenye taaluma ya uchumi kwa kozi mbalimbali nje ya nchi na niliambiwa wakati fulani alikuwa ni miongoni mwa washauri wa masuala ya uchumi kwa Mkulu enzi zile za Benny na yupo vizuri kwenye maeneo ya mipango ya maendeleo na uchumi
Chuo cha mipango alisoma lini? Mwakasege mzaliwa wa Mkoa wa Mbeya, ambaye ndoa yake imefikisha miaka 30 leo, alisoma University of Dar es salaam lakini kwa Faculty of Agriculture ambayo sasa tunaiita SUA. Mwakasege ni mtaalamu wa Agrieconomy.
Amewahi kuwa Mshauri wa Rais kwenye masuala ya Uchumi wakati wa kipindi cha Benjamin Mkapa. Ana ofisi zake Arusha zinazojihusisha na utafiti na masuala ya Uchumi pamoja na huduma yake ya MANA.
 
Ndugu wanaJF husukieni na kichwa cha habari hapo juu. naomba mtu anayefahamu vizuri curriculum vitae ya mwalimu Christopher Mwakasege anijuze, nasema hivyo maana leo nimejitahidi kuhudhuria semina yake pale viwanja vya jagwani vinavyojaa mafuruko wakati wa masika, kwa kweli sijawahi kukutana na mtumishi wa Mungu anajejua kuhubiri na kufundisha kama yeye.

Lakini pia namshukuru MUNGU Ameniepusha kuniharibia siku yangu kwa sababu ya washabiki wezangu wa yanga pale makao makuu. kosa nimechomekea shati langu jekundu nikitoka kwenye semina nikierekea nilpofikia kariakoo kwenye hoteli (kwa sababu za kibashara sitaitaja nilipofika wanayanga nikawakuta wamekusanyika nikaona nipite nisikilize matokeo na uchambuzi, niliposimama tu wakanitaka nipotee yale mazingira nikakataa ndio walipotaka wanipinge. nikiwa namsubiri atakaye aza kunipinga huku wakinitusi, mara gari ya police ikiwa kwenye patrol wakanitaka niondoke tu. namshukuru sana Mungu maana leo washabiki wezengu wa yanga wagenijua mimi ndiye mchunga ng'ombe

sasa CV ya nini hapo??

What will the CV add to hii story yako?
 
Professionally ni mwanauchumi ila pia ni mwalimu wa neno la Mungu ndo maana anaitwa mwalimu!
Sio mchungaji wala mwinjilisti ila ni Mwalimu!

Nasikia pia aliwahi kuwa banker hapo zamani.
 
ndio ni mwalimu wa neno la MUNGU. na vilevile ni mtu aliyesoma chuo cha mipango kozi ya REGIONAL PLANNING. MOJA YA KOZI NZURI KATIKA WATAALAM KWA NCHI KAMA YETU. NAFAHAMU CONTENTS YAKE KOZI HIYO MTU ANAKUWA NI MCHUMI,planner n.k n.k planner na wachumi wa kweli ni waliosoma hiyo kozi
 
Chuo cha mipango alisoma lini? Mwakasege mzaliwa wa Mkoa wa Mbeya, ambaye ndoa yake imefikisha miaka 30 leo, alisoma University of Dar es salaam lakini kwa Faculty of Agriculture ambayo sasa tunaiita SUA. Mwakasege ni mtaalamu wa Agrieconomy.
Amewahi kuwa Mshauri wa Rais kwenye masuala ya Uchumi wakati wa kipindi cha Benjamin Mkapa. Ana ofisi zake Arusha zinazojihusisha na utafiti na masuala ya Uchumi pamoja na huduma yake ya MANA.

Mkuu kilichofikisha miaka 30 ni ndoa yake au huduma yake?
Naona kama umechanganya!
Aliamua tu kumshukuru mke wake kwa kumsaidia kwenye huduma kwa hiyo miaka 30 ya huduma yao ila sina uhakika kama amesema ni ndoa ndo ina miaka 30!
 
Cv yake ina msaada gani kwa maisha yako ya kiroho,shika neno tenda neno,full stop,
 
kuna kitu sielewi kwa mwakasege je yeye anasali wapi jpili kkkt au makanisa ya pentekoste na je najua ana elimu ya uchumi je hii ya neno la Mungu anayo hata certificate?maana hata kama una kipaje elimu ina umuhimu kupunguza makosa flaniflani ktk kutafsiri neno la Mungu.
 
sasa CV ya nini hapo??

What will the CV add to hii story yako?

Unapochaganya kiswahili na kingereza unataka nikijibuje? mimi nataka kujuzwa maisha na historia ya mwl mwakasege kwa sababu nilizozitaja kuwa sijawahi kuona mtumishi wa Mungu anayejua kufundisha kama yeye.
kuweka maelezo nimeyaweka makusudi ili oune njisi nilivyopokea upako wa Mungu, na kwa sababu ile ameniepusha kuharibu siku.
 
Back
Top Bottom