Naomba kujua kuhusu safari ya Dar kwenda Dodoma kwa pikipiki

Habari za leo wakuu, ninafikiria kati ya njia mbili za kusafiri, aidha kwa pikipiki au kuisafirisha chombo yangu used kwa malori ya mizigo.
Kwa wale wenye uzoefu na route hii kwa pikipiki mnaweza kunipa muongozo wa sehemu za kupumzika, kufanya service nikiwa njiani, muda wa safari kwa makadirio na changamoto zilizopo barabara hiyo ya Dar - Dodoma,
Chombo ni mbili moja boxer cc125, na Tvs cc 150 madereva tupo wawili.
Natanguliza shukrani.
Mkuu embu nipe umbali kwa kilometer ili nishauri sawasawa.
 
Mkuu, kama kufika haraka sio issue kwako, piga gear vyombo hivyo. Adventure.

Utatumia siku 2. Pumzika kila baada ya 2 hours au kila baada ya kilometa 100-150. Pumzika kwa saa moja hivi.

Uzuri izo pikipiki ni famous, kwahiyo kila unavyopumzika unaweza enda sehemu penye mafundi wakacheki upepo na vitu vidogo vidogo.

Ukibadirisha oil huku hauna haja ya kubadirisha hadi Dom.

Mi nishaenda na pikipiki Dar to Mbeya, na ilikua air-cooled, TVS apache 180, na ilikua poa sana.

Utachoka kingese ila iyo safari hautakaa ukaisahau maishani mwako.

Narudia tena, kikubwa usiwe na haraka.
 
Dar - Dodoma haina haja ya kupakiza pkpk kwenye Lori, cha msingi jaza mafuta full tank hapa dsm, ukifika Moro jazia tena mafuta full tank na upumzike hata dak 45 hv ili injini ipoe kidogo. Hakikisha pkpk yako umejaza oil mpya na umekaza brek vizur. Ili usiumizwe sana na upepo usiendeshe spidi zaidi ya 85km/saa, vaa koti na kofia ngumu, vaa suluari ya jinsi na viatu vya ngozi. Safari yako anza sa 10 alfajiri toka dar ili usipate usumbufu wa mabasi.
 
Shukrani mkuu, ka adventure mara mojamoja sio mbaya
 
Dar - Dodoma haina haja ya kupakiza pkpk kwenye Lori, cha msingi jaza mafuta full tank hapa dsm, ukifika Moro jazia tena mafuta full tank na upumzike hata dak 45 hv ili injini ipoe kidogo. Hakikisha pkpk yako umejaza oil mpya na umekaza brek vizur. Ili usiumizwe sana na upepo usiendeshe spidi zaidi ya 85km/saa, vaa koti na kofia ngumu, vaa suluari ya jinsi na viatu vya ngozi. Safari yako anza sa 10 alfajiri toka dar ili usipate usumbufu wa mabasi.
Shukrani sana mkuu, hii njia nitaitumia
 
Kwanza tujue.

1. Dar dom km ngapi
2. Unaenda kwa km ngapi kwa saa
3. Lita inakupeleka km ngapi
4. Je una vifaa vya kujikinga, koti, helmet nk
5. Je una tool box
6. Una pesa ya dharura.

Inawezekana kabisa. Wanaokutisha hata pikipiki hawajui kuendesha. Jipange, inawezekana.
Dar Es Salaam ~Dodoma Kilometres 450
CHANGAMOTO Ulizosema Anaweza Kuwa Hana Vifaa Vitakavyolinda Afya Yake
 
Yaani natamani moja ningeendesha mimi. Yaani mnajiondokea jumamos mnafika jumapili, jumatatu upo ndani ya Kimbinyiko umelala mwanzo mwisho hadi Mbezi unakoroma tu.
Hahaha, mkuu
Next time nikija nitakualika unisindikize Dom
 
Dar to Dom ni 450KM.
Hiyo safari igawe siku2 kwa kutembea saa sita sita.

Fanyia service pikipiki, badili oil weka mpya, rekebisha nyororo, kaza kaza nut zote, taa iwake na tube nzima.

Ondoka Dar hadi Moro, lala pumzika.
Kesho yake Moro to Dom.

Ukifika mwisho wa safari mwaga oil.
Asikutishe mtu kama wewe ni dereva mzoefu, tembea 60-80 hadi 100 kmph kutokana na eneo.

Mimi nilikuwa natembea saa6, km300 kwa kutumia rouph road lakini nafika bila tatizo lolote.

Hiyo barabara ya lami wala hautachoka kivile, isipokuwa kama utadunda dunda sana kwenye makorogesheni muda mrefu, makalio mzee, kumbuka zile fimbo ulizokuwa ukitandikwa shule ndivyo yatakavyosoma.

Anzisha safari yako kama saa1 kabla ya muda wa mabasi ya abiria utatembea bila bugudha njiani.

Kama walivyoshauri wengine, spana ni muhimu na pesa ya dharula.

Waweza tembea hadi mwisho wa safari wala usikumbane na kikwazo chochote.

Nikutakie safari njema.
 
Dom karibu sana mkuu, kuna jamaa alisafiri na pikipiki dsm-kyela na baada ya week akarudi dsm boxer 125......zingatia mavazi tu
 
Back
Top Bottom