Nategemea kwenda Shinyanga kwa pikipiki aina ya Boxer, CC 125

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,679
12,249
Ndugu wanajamvi nategemea kwenda Shinyanga nikitokea Dar es salaam kwa Piki piki boxer cc125 mwenye uzoefu itakuwa vyema ukanisaidia.

Nataka kujua mafuta naweza kutumia kiasi gani. Je, nijiandae kwa changamoto gani barabarani pikipiki hii ninayotaka kuitumia ni mpya. na nina tegea kwenda na kurudi....

1695546957011.jpeg
.mrejesho,
Nilibadili safari nikaenda Tanga, muda huu saa 11:30 nipo Mkata. Nilitoka dar es salaam saa 7:30 asubuhi nilikuwa naendesha speed 70 Hadi 80 kwakweli tunaogopa TU.

Ila Kwa boxa IPO vizuri sana barabarani imetulia japo ukizidi speed 90 inayumba nadhani ni kutokana na kuwa sikuwa nimebeba mzigo.

Usafiri wa piki piki ni hatari sana kwani Kuna baadhi ya madereva awazingatii sana Sheria za barabarani.

Nilinusurika kugongwa nikasukumiwa Kando ya barabara baada ya dereva kuovatake bila kujali kuwa nilikuwa mwendo Kasi nakuja Kwa mbele yake...nisingetoka nje ya barabara ninge gongana uso Kwa uso na gari iliyokuwa inaovertake.😭😭😭

Ila Kwa ufupi ukiacha uchovu kidogo barabara haipo busy. Hivyo haikuwa hatarishi sana. Mliokuwa mnaogopa kusafiria pikipiki ndugu zangu msiogope PIKI piki ni usafiri mzuri TU na WA haraka sana.
IMG_20230411_115549_887.jpg

Hapa nilikuwa nimefika chalinze, ubao wa speedometer ikawa unasoma kama picha inavyooneka. Nilikuwa natembea sehemu inayo ruhusu nilikuwa nafika Hadi speed 95 kama picha invyoonesha
Screenshot_20230925-092453.jpg

nilienda na nikarudi zaidi nilidondosha tu number plates ila siku haribikiwa wala kuishiwa mafuta🤣🤣🤣🤣​
 
ndugu wanajamvi nategemea kwenda Singida kwa Piki piki boxer cc125 mwenye uzoefu itakuwa vyema ukanisaidia, nataka kujua mafuta naweza kutumia kiasi gani. je nijiandae kwa changamoto gani barabarani. piki piki hii ninayotaka kuitumia ni mpya. na nina tegea kwenda na kurudi....

View attachment 2760635.​
Tatizo umeandika kwa Kkukurupuka kama unakimbizwa hujasema unatokea wapi Dar au Nairobi
 
Sijui kama uwezo wa injini utahimili umbali huo, wajuvi watatuambia
ila kwa dar es salaam hii pikipiki naizurulia siku nzima kuanzia asubuhi saa 11 hadi usiku saa 6 bila kupumzika, hivyo nadhani itahimili, japo natamani nipate wazoefu ambao walishawahi kwenda longtrip kwa usafiri kama huu
 
Safari ya pikipiki masafa marefu ni nzuri kama unapenda kuenjoy mandhari ya njiani kama milima, misitu nk.. lakini changamoto kubwa iko kwenye mafuta.
Nilishawahi kufanya safari mara kadhaa kutoka hapa Dodoma kwenda mikoa ya jirani kwa pikipiki changamoto kubwa ni mafuta ujipange
Niliwahi kusafiri umbali wa zaidi ya km650 kwa siku moja cha msingi hakikisha una kofia ngumu, koti zito, miwani inayofunika macho kuzuia upepo, gloves, na viatu hasa buti pia hakikisha umefanya service ya pikipiki yako na kukagua kila kitu kuanzia tires, chain,engine oil nk.
Andaa budget ya mafuta maana kwa kawaida pikipiki haili mafuta sana ila unaposafiri masafa marefu lazima utakimbia speed kubwa muda mrefu hivyo mafuta yanatumika sana usishangae unajaza full tank hata mara tatu au zaidi mpaka kufika unakoenda.
 
Back
Top Bottom