Naomba kufahamu Madhara ya kupeana talaka baada ya ndoa Kuvunjika

Nimempa ujauzito mwanamke mmoja wa kizungu mimba ina miezi kadhaa sasa ila anaishi nje ya canada mwanzo nilikuwa nataka aitoe tu akagoma lakini kadri muda unavyozidi kwenda naona namhitaji huyo mtoto aliye tumboni si vyema kumtelekeza sasa katika hilo ndio likaibuka suala la kumwambia mkewangu tu ukweli kwamba mwenzie mimi nishaharibu huko nje na natarajia mtoto mwingine sasa hali nayoisikia huku ndani ni tofauti sana.. atalibebaje atalikubali ? na baada ya kumwambia hali ya ndoa yetu itakuwaje ? kama itafikia kupeana talaka hali itakuwaje ndio maswali yanayonisumbua kwasasa mkuu
Kama unaitaji kutua mzigo ulobeba moyoni mwako pasipo kujali madhara yake,Basi mwambie tu ili upate amani.
 
Mimi ni mkristo na nipo kwenye ndoa kwa muda wa miaka 8 na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili sasa ila kuna jambo nililikosea kwa mkewangu na sasa nataka nimwambie ukweli kuhusu hilo sasa kutokana na uzoefu kumhusu kwa kaliba yake naona kabisa ataenda kukiwasha isivyo kawaida na kwa asilimia 89.6% anaweza kudai talaka (namuwazia tu kichwani:().

Sasa kabla sijakubali atakachokidai naomba kufahamu kwa wale ambao mmeshapitia hii situation ya ndoa kuvunjika mpaka kupeana talaka.

Je, kuna madhara yoyote yanaweza kutokea kama mmekaa kwenye ndoa kwa muda mrefu kiasi hiki ukiachana na kugawana mali sijui nini?

Je, haya mambo ya kupeana talaka inaweza kuniletea shida ya kisaikolojia au kiroho nikakengeuka?

Mliopita kwenye hii situation naomba uzoefu wenu, nitashukuru sana kabla sijaaamua ..🙏

Mazara ni makubwa sana kwa viumbe visivyo makosa
 
Kuishi nao kwa akili ni pamoja na kutomwambia hicho kitu
 
Sijui ni dini gani ila kwa Mungu kuna amani. Najua unaitaka amani ila amani ya kweli ipo kwa Mungu pekee. Rudi kwake muombe muobgozo. Hapo kuna maisha ya viumbe wawili. Pia kuna maisha yako hasa nafsi itakavyojutia ikiwa utaachana na mkeo. Mimi nina changu japo sio cha ndoa. Nilienda kwa Mungu nikamuomba nikimaanisha sitarudia tena. Huwa Mungu anahuruma mno. Alinisamehe na kuonesha anakupa amani kuu. Shetani atajaribu kuichukua ila ukisimama na Mungu hawezi. Ndio umekosa ila kuivunja ndoa ni kosa kubwa mno. Maadam hujaua kiri kwa Mungu, utafute uso wake atakupa majibu yake.
 
Siku zote Na Mara nyingi wanawake ndio huanza kuomba talaka. Kama humtaki, tengeneza mazingira aiombe.
Majukumu yako yatakuwa pale pale mf. Kuhudumia watoto Na hata yeye pia kama ambavyo Mahakama itaamua.
Pia jaribu sana kuwa amicable - yaani anza kujitoa pole pole, ukojotoa haraka Na yeye hataki au hayuko tayari- mtiti wake si wa mchezo...
Watoto ndio huathirika zaidi. Na wewe pia itakuathiri Mara tu akiangukua Kwa mkunyenge mwingine halafu unapangiwa masharti ya kuwaona watoto wako...lazima utagundua tu...
 
Iseme hiyo siri, kuna wenye busara zao humu kina Mshana Jr ERoni Watu8 Glenn Heaven Sent watakupa ushauri mzuri wa a way foward.

Niliposoma uzi mwanzo kwa namna alivyoandika kwa vificho nilidhani labda jamaa kaamua kuwa choko...

Kumbe mwamba kaongeza familia na anakuwa muoga muoga...

Kitu pekee naweza muhakikishia ni kwamba ajiandae kumpoteza huyo mke wake wa miaka 8 ya ndoa...
 
Kumbe ni jizi?
 
Back
Top Bottom