Naomba kufahamu kuhusu ndoa ya aina hii

A teller

JF-Expert Member
Feb 6, 2018
492
687
Wakuu habarini za jioni!

Nafikiria kuanza mchakato wa kufunga ndoa na huyu mchumba wangu wa tangu vidudu Hadi Sasa, kutokana na Mambo kadhaa ambayo yapo nje ya uwezo wetu, naomba kufahamu utaratibu wa kufunga ndoa ya serikali upoje? Nikiwa namaanisha process za kufunga ndoa ya kiserikali upoje, na Hatua zipi nifuate Hadi kukamilika kwake.

Pia faida au hasara za ndoa ya aina hii. Mawazo yenu ni muhimu wakuu

Ahsanteni!
 
Mnaenda na huyo mchumba wako na kila mmoja na mpambe wake mnaandikisha,baadae wanaweka tangazo ubaoni wa kusudio lenu.

Na ndoa itafungwa baada ya siku 21kama kuna pingamizi kwa yoyoyte kuhusu ndoa hiyo.Faida ni kwamba inatambulika kiserikali na baadhi ya madhehebu pia ni uthibitisho wa kwamba ni mume na mke.Hasara ni kwamba mkuachana lazima mgawane mali!
 
mbele za Mungu ni nyinyi mtakua wazinifu mliojihalalishia kuzini hadharani mbele ya serikali na watu wachache.
 
Kama sio mshika dini tatizo hakuna

Lakini kama ni mshika dini kuna baadhi ya mambo hutashiriki,ama kushiriki kwa ukosaji kama kushiriki sakramenti ya meza ya bwana na hata katika mifungo ya ramadhan na kwaresma itakuwa ni ngumu kwa ndoa ya aina hiyo kushiriki
Ok, nimekuelewa.

Sema kuna taratibu zimewekwa lengo kuwafanya watu wawe watumwa wa dini zao.
Sio kama zina mashiko kiimani.
 
Mnaenda na huyo mchumba wako na kila mmoja na mpambe wake mnaandikisha,baadae wanaweka tangazo ubaoni wa kusudio lenu.

Na ndoa itafungwa baada ya siku 21kama kuna pingamizi kwa yoyoyte kuhusu ndoa hiyo.Faida ni kwamba inatambulika kiserikali na baadhi ya madhehebu pia ni uthibitisho wa kwamba ni mume na mke.Hasara ni kwamba mkuachana lazima mgawane mali!
Ahsante Sana Mkuu, na vipi kuhusu gharama
 
Mnaenda na huyo mchumba wako na kila mmoja na mpambe wake mnaandikisha,baadae wanaweka tangazo ubaoni wa kusudio lenu.

Na ndoa itafungwa baada ya siku 21kama kuna pingamizi kwa yoyoyte kuhusu ndoa hiyo.Faida ni kwamba inatambulika kiserikali na baadhi ya madhehebu pia ni uthibitisho wa kwamba ni mume na mke.Hasara ni kwamba mkuachana lazima mgawane mali!
Ok, na vipi kuhusu ndoa ya kikristo huwa hawagawani mali wakiachana?
 
Kama sio mshika dini tatizo hakuna

Lakini kama ni mshika dini kuna baadhi ya mambo hutashiriki,ama kushiriki kwa ukosaji kama kushiriki sakramenti ya meza ya bwana na hata katika mifungo ya ramadhan na kwaresma itakuwa ni ngumu kwa ndoa ya aina hiyo kushiriki
Kwa uislamu inatambulika kwa sababu ndoa inafungishwa kwa kauli sio utukufu wa mfungisha ndoa nina maana mtu yeyote anaweza kufungisha ndoa kikubwa awe na akili timamu .

Kauli itatamkwa kwa yakini ya muoaji na mkewe hii inatamkwa ili watu wasikie wale mashahidi ,la sivyo ingekuwa anatamka moyoni ..Hata kumslimisha mtu anatakiwa kutamka shahada wala hamna kingine dk 4 hazifiki tayar.

Unatamka ili kuonyesha umeridhia mbele ya mashahidi kisheria na mahali popote sio lazima msikitini wala kuvaa kanza hayo mi miongoni mwa sunnah ,ila utavaa mavazi kama nguo ndefu kwa wanaume ili kustiri uchi kisheria na mke kujitanda .

Basi ingekuwa za mahakamani hazifai kweny uislamu pasingekuwa hata na ndoa za mkeka tena hizi hata ukutwe gesi mko uchi mnaweza kufungishwa hivyo hivyo na vichupi vyenu na ndoa ikatambulika.

Ndoa ya serikali lazima patakuwa na mashahidi ndo hivyo hivyo kweny uislamu hata watu watano basi .
 
nyie mnaosema ndoa ya mahakama haitambuliki na Mungu, niwaulize ndoa ni tendo la kiimani au ni matakwa ya kisheria?

Kama ni tendo la kiimani ya dini yako mbona cheti cha ndoa hutolewa na mamlaka za kiserikali na siyo za dini yako?

Mimi kama mkristo hakuna mahali Biblia iketaja neno ndoa, ila muunganiko wa mwaume na mwanamke ambao unatakiwa utambulike na kiongozi wako ili kukutoa kwenye hatia ya uzinzi. Kiongozi wako wa kidini anahusika tu kubariki muungano wa mwanamke na mwanaume.

Unaweza kufunga ndoa ya mahakama na ukaomba ubarikio wa unganiko lenu kutoka kwa kiongozi wako wa kiimani
 
Wakuu habarini za jioni!

Nafikiria kuanza mchakato wa kufunga ndoa na huyu mchumba wangu wa tangu vidudu Hadi Sasa, kutokana na Mambo kadhaa ambayo yapo nje ya uwezo wetu, naomba kufahamu utaratibu wa kufunga ndoa ya serikali upoje? Nikiwa namaanisha process za kufunga ndoa ya kiserikali upoje, na Hatua zipi nifuate Hadi kukamilika kwake.

Pia faida au hasara za ndoa ya aina hii. Mawazo yenu ni muhimu wakuu

Ahsanteni!
Nenda ofisi ya mkuu wa wilaya upate muongozo.
 
Back
Top Bottom