Nansio Ukerewe: Kijana aponda mbwa na jiwe kwa mkono wake na kubaki umenyooka

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
3,871
8,381
Kijana huyo ambae hajafahamika majina alimponda mbwa na jiwe jana usiku majira ya saa 2 usiku.

Tukio hilo la kustaajabisha liliyokea/limetokea Ukerewe Nansio maeneo ya Bakwata (Musoma road) mwisho wa lami.

Picha kukujia punde
 
Tukio hilo nimelishuhudia mwenyewe na mhanga nimemuona kwa macho yangu. Sikuweza kumpiga picha
 
Attachments

  • IMG_20221119_84649.jpg
    IMG_20221119_84649.jpg
    20.5 KB · Views: 17
Mhanga alipatwa na zahama hilo sana 2 jana, amelala hivo na leo asubuhi ndo kubweka wazi. Watu ndo wakaanza kujaa.

Kama kuna mtu yeyote humu ana ndugu, RAFIKI au jamaa anaeishi Nansio Ukerewe basi awasiliane nae amuulize
Ngoja nimcheki jamaa yangu yupo town hapo
----
Jamaa kathibitisha, ni kweli jamaa mkono umegoma kujikunja yani umenyooka tangu alivyo rusha jiwe.

Ila la kubweka sio kweli

Pia jamaa anasema anahisi ni mchezo tu ili atokee mganga ajifanye kamtibu alafu raia waanze kupigwa pesa na mganga.
 
Huwa nadikia kihistoria hawa wakerewe waliokuwa ni sehemu ya makabila yaliyokuwa yanaoatikana Mkoa wa Kagera lakini kutokana na vimbwanga vyao na teknolojia ya miziziology, mazigaumbweology na ulogirism walifukuzwa kagera na kwenda kuanzisha himaya Yao kwenye hicho kisiwa ambacho kilikuwa hakimilikiwi na mtu ( TERA NULLIUS)
 
Tusipoondokana na huu ujinga tusahau kabisa kuhusu maendeleo.

Maendeleo ya karne hii ni sayansi na teknolojia, hivyo kama tumeshajikatia tamaa na kujiona ni wa kubaki kusindikiza wengine hapa Duniani basi hayo ndio ya kushadadia.

Huyo Majeruhi mpelekeni Hospitali na x ray itawapa majibu huenda ame "strech' mkono wakati anarusha jiwe...au hata huenda alizaliwa na ulemavu huo na ameamua kuwaokota maana anajua huwa hamna ziada ya kufikiria zaidi ya kile mnachoambiwa.
 
Ngoja nimcheki jamaa yangu yupo town hapo
----
Jamaa kathibitisha, ni kweli jamaa mkono umegoma kujikunja yani umenyooka tangu alivyo rusha jiwe.

Ila la kubweka sio kweli

Pia jamaa anasema anahisi ni mchezo tu ili atokee mganga ajifanye kamtibu alafu raia waanze kupigwa pesa na mganga.

Sahamani mkuu, hapo kwenye kubweka sijamaanisha jamaa alibweka au alikuwa anabweka wazi.

Hiyo ni typing error, nililenga ALIWEKA WAZI ndo watu wakajua wakaanza kujaa
 
Tusipoondokana na huu ujinga tusahau kabisa kuhusu maendeleo.

Maendeleo ya karne hii ni sayansi na teknolojia, hivyo kama tumeshajikatia tamaa na kujiona ni wa kubaki kusindikiza wengine hapa Duniani basi hayo ndio ya kushadadia.

Huyo Majeruhi mpelekeni Hospitali na x ray itawapa majibu huenda ame "strech' mkono wakati anarusha jiwe...au hata huenda alizaliwa na ulemavu huo na ameamua kuwaokota maana anajua huwa hamna ziada ya kufikiria zaidi ya kile mnachoambiwa.

Mkuu ni kijana wa hapa hapa anaefahamika. Mimi nimeleta habari kama nilivyoishuhudia, swala la KUAMINI ni kweli au si kweli linabaki kwa mtu binafsi.

Hata mimi sijaweza KUAMINI kama mkono umenyooka kutokana na kumponda mbwa.

What if ni mchezo?? (Japo nilipomuona tayari alikuwa ameshalimwa chale za kutosha kwenye huo mkono. Maana awali nilipoenda nilikuta wamemfungia ndani, baadae nikarudi zangu kazini, baada ya dakika kama 5 jamaa yangu akanipigia simu kuwa wamemtoa nje, ndo nikaenda kushuhudia)

Unaweza ukawa ni mchezo kweli, LAKINI TUKIO HILO LIMETOKEA
 
Kuna dada mmoja nae ilimtokea,katoka zake kunywa huko kajilewea....arudi home...sasa njia aliyopita mbele kuna uwanja wa Mpira wa miguu,,naona akaona isiwe shida sana kuzunguka usiku huu wakati hakuna mechi uwanjani...akaamua kupita katikati ya uwanja....si ndo akaona kundi la mbwa....yeye anasema hawakumbwekea wala kumkimbiza ila kitendo cha kuona kundi kubwa la mbwa akaingiwa uoga akaokota jiwe kuwabonda....anasema alisikia kilio cha mbwa mmoja tu nadhani ndo jiwe Iilimpata....then mbwa wale wakasambaratika...na yeye akapita salama salmini....kafika home kalala,Mara kaanza kusikia maumivu ya mkono,akavumilia mpaka asubuhi ....kuamka akakuta mkono umeumuka na umeota magamba ya nyoka.Wakati anasimulia alikuwa tayari kazunguka kote bila kupona....nasikia alikufa baadae yule dada
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom