Nani awe 'JF Miss Chit-Chat' mwaka 2012?

Nani unampa kura yako kama Miss Chit Chat 2012?

 • Cacico

  Votes: 27 11.2%
 • Remmy

  Votes: 7 2.9%
 • Madame B

  Votes: 40 16.5%
 • Ciello

  Votes: 5 2.1%
 • Charminglady

  Votes: 115 47.5%
 • Arabela

  Votes: 48 19.8%

 • Total voters
  242
 • Poll closed .
Status
Not open for further replies.

Ruhazwe JR

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
3,403
2,000
Wasalam,

Ni mara nyingine tena kama ilivyokuwa inasubiliwa sasa ndio imetimia.

Kwanza niwaombe radhi kwa kutokufanya mashindano ya mwezi Dec 2012, hii ilitokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wangu licha ya jitihada nilizozifanya za kuwatafuta ambao wangeweza kuendesha mashindano lakini kwa bahati mbaya haikuwezekana. Niombe radhi sana na samahani kama kuna mtu alikwazika anisamehe bure.

Bila kuwachosha, tunamtafuta MISS CHIT CHAT 2012 ambaye atapeperusha bendera kwa mwaka wote. Washiriki ni kama ifuatavyo:

1. cacico - miss aug 2012
2. Remmy - miss Sept 2012
3. Madame B - miss oct 2012
4. Ciello - miss nov 2012
5. charminglady - Nafasi ya upendeleo
6. Arabela- Nafasi ya upendeleo

ZAWADI
Zawadi zitakuwa kama ifuatavyo:
a/ Mshindi wa kwanza atajipatia Muda wa maongezi kwa mtandao atakao kuwa anatumia wenye thamani ya TSH 16,000/= pamoja na kulipiwa JF Bronze(mchango wa jf wa thamani ya THS 20,000)
b/mshindi wa pili atajipatia muda wa maongezi kwa mtandao atakao kuwa anatumia wa thamani ya Tsh 12,000/=
c/ mshindi wa tatu atajishindia muda wa maongezi wa mtandao atakao kuwa anatumia wa Tsh 8,000/=
d/ mshindi wa nne atajipatia muda wa maongezi kwa mtandao anaotumia wa thamani ya Tsh 6,000/=

Masharti

- Washiriki wanaruhusiwa kujipigia kura na kufanya kampeni za kuomba kura
- One member one vote
- Mwisho wa kupiga kura ni tarehe 31 dec saa 6 usiku kamili.
- Zawadi zitatolewa siku ya tarehe moja asubuh.

Wadhamini
- masopakyindi - Tshs 60,000/=
- Ruhazwe JR - Tshs 42,000/=
- Samaritan Tshs 11,000/=
- kitalolo - 10,000/=
- Mu-sir -Tsh 10,000/=
- Chimbuvu -Tsh 5,000/=
- Jiwe Linaloishi- Tsh 3,000/
- Slave - Tshs 2,000/=
JUMLA 143,000/=

- Akijitokeza mdhamini mwingine basi zawadi itaongezeka!

Nawasilisha..

===========

UPDATE
Tumepata mdhamini mwingine anayejulikana Jiwe Linaloishi yeye anadhamini muda wa maongezi wenye thamani ya Tsh 3000 kwa mshindi atakaye shika nafasi ya nne. Tunaomba wadhamini wengine wazidi kujitokeza ili washiriki wetu wapate zawadi iliyo nona

MORE UPDATE
Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kuwa,wamejitokeza wadhamini wengine wawili kama ifuatao;-

1. Chimbuvu (udhamini wa Tshs 5,000/=) na Slave (udhamini wa Tshs 2000/=).kwa sababu hiyo zawadi za washindi zimeongezeka.Tunazidi kuwaomba wadhamini wajitokeze zaidi.

MORE UPDATE
Napenda kuwa taarifu kwa heshima na furaha kuwa,tumepata mdhamini mwingine anaitwa Mu-sir ambaye amedhamini kiasi cha Tshs 10,000/= ilikuongezea katika zawadi kwa washindi watakao patikana.kwa niaba ya wanachitchat nakupa shukrani mkuu Mu-sir. Tunaomba wdhamini wengine wasisite kujitokeza ili washiriki wetu wapate zawadi iliyo nona.

MORE UPDATE
Nikiwa nafuraha tele napenda kuwapa taarifa wadau wote kuwa tumepata wadhamini wengine wa aina yake. naye ni 1. masopakyindi amedhamini tshs 60,000/=. 2. Samaritan amedhamin tshs 11,000/= kwa niaba ya wanachitchat nitoe shukrani za pekee kwa wadhamini hawa hasa kwa mdhamini masopakyindi kwa kuvunja record ya udhamini.udhamini huu ni wa aina yake,endapo kama atajitokeza mdhamini mwingine wa kiwango kizuri basi tutaongeza mchango kwenye kuchangia jf kwa mshindi wa kwanza.tunaomba wadhamini wengine wajitokeze zaidi.

Hivyo basi zawadi hizi zilizo ongezeka zenye jumla ya 71,000/= zitasubili endapo akijitokeza mdhamini mwingine wa kuanzia Tshs 10,000/= ili tukiongeza na Tshs 20,000/= iwe jumla ya zaidi ya laki moja na kumchangia kifurushi kingine cha JF Gold bronze.

Ahsanteni..

PIGA KURA SASA!
 
Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,379
1,500
Huu ni ubaguzi wa wazi na dhahiri.
Kwanza ni vigezo gani ulivyotumia kupata hao warembo hapo juu, na kwa nini jina langu na la lara 1 halipo kwenye hicho ulichoita 'NAFASI YA UPENDELEO'?

Hapa lazima nipige kampeni ya kususia huu mtanange, mpaka utupe majibu ya kina.

Hii haikubaliki kabisa kijana.
 
Last edited by a moderator:

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,794
2,000
Shosti ukiwekwa wewe itakuwa unfair competition. Wewe wa chuo chikuu ushindanishwe na watoto wa P4? Aaah, kashindane na magwiji wenzio banaa!
Huu ni ubaguzi wa wazi na dhahiri.
Kwanza ni vigezo gani ulivyotumia kupata hao warembo hapo juu, na kwa nini jina langu na la lara 1 halipo kwenye hicho ulichoita 'NAFASI YA UPENDELEO'?

Hapa lazima nipige kampeni ya kususia huu mtanange, mpaka utupe majibu ya kina.

Hii haikubaliki kabisa kijana.
 
Last edited by a moderator:

Ruhazwe JR

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
3,403
2,000
Huu ni ubaguzi wa wazi na dhahiri.
Kwanza ni vigezo gani ulivyotumia kupata hao warembo hapo juu, na kwa nini jina langu na la lara 1 halipo kwenye hicho ulichoita 'NAFASI YA UPENDELEO'?

Hapa lazima nipige kampeni ya kususia huu mtanange, mpaka utupe majibu ya kina.

Hii haikubaliki kabisa kijana.
mkuu Zinduna....
Nafasi ya upendeleo imetokana na hatua yangu binafsi ya kuweka washiri angalau wawe sita badala ya wa nne na kigezo nilichotumia kuwachagua kuwapa nafasi ya upendeleo nimeangalia wale amabo waliwahi kushika nafasi ya pili kwa kura nyingi,rejea mashinda ya miss october charminglady alikuwa wa pili, rejea mashindano ya miss chitchat mwezi wa Nove Arabela alikuwa wa pili na hawa wote walivunja record katika wote walio wahi kushika nafasi ya pili.

unazungumzia lara 1, kwanza ajawahi kufikia nafasi ya pili,na mara zote amekua akinisihi kuondolewa kuwania taji hata kama amependekezwa.Je unaswali? kila la khel katika kampen zako
 
Last edited by a moderator:

Loy MX

JF-Expert Member
Mar 26, 2012
1,253

naomba nikupendekeze au we wasemaje
 
unaa akili wewe!...dah!.... nahisi wewe ni mtu wa haki full.kazi nzuri aisee
 
Ruhazwe JR

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
3,403
2,000
Huu ni ubaguzi wa wazi na dhahiri.
Kwanza ni vigezo gani ulivyotumia kupata hao warembo hapo juu, na kwa nini jina langu na la lara 1 halipo kwenye hicho ulichoita 'NAFASI YA UPENDELEO'?

Hapa lazima nipige kampeni ya kususia huu mtanange, mpaka utupe majibu ya kina.

Hii haikubaliki kabisa kijana.

haya maneno inaonesha kabisa roho inakuuma kwa kukosa kushiriki,unalo dada weye!
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,794
2,000
Wifi huko gym usiniache... Alafu tuweke taratibu Ms na Miss ziwe equivalent na sie tugombee mwakani baada ya kuwa portables. Lol

Nakusalimu with Love. :mwaaah:
love you more wifi. Nimesalimika.
Na kweli kuwe na kategori ya wazee. Na hiyo tuchanganywe na wanaume manake wanawake wazee twataka usawa. Nakupa na viwalo vya gyn vya kuanzia ila kama unataka hijab utajitegemea hiyo.
 
AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,221
1,500
love you more wifi. Nimesalimika.
Na kweli kuwe na kategori ya wazee. Na hiyo tuchanganywe na wanaume manake wanawake wazee twataka usawa. Nakupa na viwalo vya gyn vya kuanzia ila kama unataka hijab utajitegemea hiyo.

ha ha ha! Hapo umenena! naomba viwalo basi viwe vya kunitosha isije ikawa kama nimevaa soksi... Naogopa wateja wa gym kuwavunja mbavu! Lol. Hijabu nitakuja nayo spesheli kwa gym.

Hivi inaruhusiwa kusema umempigia kura nan uniambie uliempigia? Lol
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom