Nani anaweza kuwa CDF mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama?

Kikanuni lazima wawe wamepita jkt..
kama wamefika huko na hawakupita jkt hawana sifa ya kua cdf...
Hivyo wa chini yao.aliepita jkt ataweza kupandishwa mfulilizo hadi kwenye levo yao...na atapewa cdf..
Sio lahisi kwa sasa..wangetaka hivyo wangefanya mchezo huo toka mwaka wa jana.
Lazima kwenye hiyo timu ya maluten jeneral yupo aliepita jkt..watapeleka majina ma3 yatachambuliwa...atasimikwa mmoja wao.
Sijawahi kuisikia hii kanuni na sielewi kwanini imewekwa.
 
Kufatia habari ya jana ya kustaafu kwa General Mabeyo ndani ya JWTZ, basi kama kawaida yetu sio mbaya tukafanya bashiri ya nani anaweza akawa CDF mpya.

Kwakuwa JF ni uwanja mpana, ina wadau wengi na wengine ni wa huko huko jikoni, sio mbaya tukapendekeza jina la CDF mpya kwa kuzingatia uweledi wake katika kuchapa kazi.

Mimi nampa nafasi kubwa Luteni Jenerali Mathew Mkingule kuwa CDF mpya.

Lakini pia kwenye korido anatajwa Luteni Jenerali Yakubu Mohamed balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Japo pia mzee wa infantry, Meja Jenerali Mwaisaka anapigiwa chapuo.

Vilevile, Meja Jenerali Rajab Mabele naye anaweza akawa CDF mzuri tu kwa utendaji wake mzuri wa kazi huko JKT.

Japo pia kuna minong'ono kuhusu Meja Jenerali Suleimani Mzee kufatia kazi ya kutukuka huko Magereza.

Ila watu wasimua-underrate Meja Jenerali Mbuge lolote linaweza kutokea. Japo kwasasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Brigedia Jenerali J.J. Mwaseba mkuu wa chuo cha TMA naye anatajwa japo atakuwa yupo nyuma sana kwa rank kulinganisha na hao wenzake.

NB:
Uzi huu haumlengi kumpigia mtu yoyote promo!!

Viva JWTZ
Viva Tanzania
All in all CDF mpya lazima awe muislamu mwenzetu.
 
Humu watu hata protokali za jeshi hawazijui
Yani mtu ni brigedier general au major general awe cdf halafu aachwe lieutenant general?
Enzi za mwendazake ofcourse ingewezekana hata segeant kuwa cdf
Sheria inatamka mmoja wa majenerali. Anaweza kutokea kaunzia Brigedia, Meja, au Luten Jenerali.

Ingekuwa hivyo WANGEUANA SANA kisa hiko cheo, na ndio maana sheria inataka kuteua kati ya hao MAJENERALI, hakusema Lazima awe luten Jenerali.

Usikariri, uchaguzi wa Jenerali unazingatia vitu vingi ikiwemo umri wa kuweza kuhudumu kazi hiyo, mrengo wake kwenye utawala ( Mpole, au Mtu wa kutumia nguvu nk).
Nishani alizonazo, uzoefu katika kuongoza watu.

Sio kama unavyochukulia wewe.
 
Back
Top Bottom