Habari wana MMU?
Naomba kuelimishwa. Mimi nimekuwa na mpenzi wangu ila simuelewi, Kila kukicha salamu nianze mie, nikiwa kimya hata hadi jioni naye atakuwa kimya. Nikimtumia sms za love labda I love you, anajibu ME TOO.
Nikimimuuliza kama ananipenda wakati tunaongea anasema ananipenda. Sielewi, Me nahisi sote twatakiwa kukumbukana si lazima me tu kila kukicha nianze kutamka neno au kusalimu. Na wakati mwingine nikimtumia meseji ya love hajibu ila nikituma meseji ya kitu kingine kisichohusu Love anajibu haraka.
Nikimuumiza meseji yangu ya mwanzo hukuiona ataweza sema nilikuwa buzy sana. Yaani napata wakati mgumu kumuwaza.
Nampenda ila ye simuelewi upendo wake.