Nani anahitaji mapokezi makubwa ya heshima, ni Rais Samia ambaye siku zote anapambana kujenga uchumi au Tundu Lissu anayekirudia kivuli chake?

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Ni swali tu ndugu zangu ambalo limekuwa likininitatanisha sana na leo nimeona nishiriki nanyi kulijadili.

Nimeona Tundu Lissu akiomba watu wakahudhurie mkutano wa hadhara uliotishwa na chama chake, ni jambo jema kama kiongozi wa kisiasa.

Pia, nimeona watu wakihimizana wakampokee Lissu akitua uwanja wa ndege hapa ndipo kwenye ukakasi na kupelekea kuuliza swali hili: Je, ni nani anayestahili mapokezi ya heshima kati ya Dkt.Samia ambaye siku zote ameshiriki pamoja nasi kupambana kujenga uchumi wetu au ni Tundu Lissu ambaye alikikimbia kivuli chake mwenyewe na sasa anakirudia?

N.B: Hata mwana mpotevu alipokelewa kwa shangwe na sherehe kubwa lakini mtoto aliyekuwepo siku zote nyumbani na babaye ndiye aliyeahidiwa urithi wa kila kitu.
 
Wananchi ndiyo wanaamua nani wampokee .... Hata Maza alipochukua cheo alipokelewa na kufanya sherehe Airport. Naona CCM wamechoka.

Waachie Chadema nao wafanye mambo yao. Sijui wewe inakuuma nini. Kama mapoketu tu basi nenda ukampokee Maza akirudi toka Davoz....!!
 
ELIAH_NGASE%F0%9F%85%B0_on_Instagram%3A_%E2%80%9CNiyeye!!!!%E2%80%9D%22_.jpg
 
Mwambie mama ajitegeshe apigwe risasi angalau tatu, apelekwe pahali atibiwe atoroshwe kiaina nchini halafu aje tumpokee.Wacheni wivu kwa vitu vya kijinga.Tundu lissu hata apokewe na watanzania wakenya na waganda hatakuwa mkubwa kama mama.KUMBUKA MAMA NI RAISI.
 
Mnampokea mtu ambae ameshawaambia fika kuwa anakuja kudai hela zake. Mbona sijamsikia akisema alichojipanga nacho. Wapumbavu ndo wanamsapoti
 
Jibu hapa ni kwamba Rais ana watu wake maalum ambao huwa ( protocol ) wanaoenda kumpokea. Si lazima wananchi waende sababu wapo watu wanalipwa kazi hiyo.

Mapokezi ya Lissu ni mapenzi binafsi, unaweza uende ama ukauchubua.
 
Back
Top Bottom