Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,756
Kwa mujibu wa yanayoendelea nchini sasa ni kwamba wananchi wengi hawaamini kauli nyingi za serikali hususani zinazotolewa na Jeshi la Polisi kuhusu masuala ama matukio ya kinyama waliyofanyiwa upinzani.
TUndu Antipas Lisu ni Mtanzania anayestahili haki zote za kikatiba na kisheria. Haki yake ya kuishi iliingia majaribuni baada ya tukio la kinyama dhidi yake lililomlazimu kukimbia nchi huku akiwa anapatiwa matibabu.
Tumemsikia akisema waziwazi kuwa mkuu wa awamu ya Tano ndiye aliyeamuru kushambuliwa kwake kwa lengo la kutoa uhai wake. Mpaka sasa ninavyoandika hapa hakuna mtuhumiwa yeyote aliyehojiwa wala kushtakiwa kwa tukio hilo la unyama wa mchana kweupe.
IGP mstaafu alisema kuwa mwenye ushahidi tosha ni mtendewa yaani Lisu. Hivyo anatuaminisha kuwa endapo Lissu angekufa basi case ingekuwa closed kitambo. Tumejulishwa na wasamaria wema kuwa CCTV kamera zilizorekodi tukio ziliondolewa mara baada ya tukio.
Ni jambo gani linaloipa serikali kigugumizi kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya walioitia doa baya sana nchi kwa tukio lile?
JPM ni mwaka wa pili sasa hayupo na hana amri ya kuzuia uchunguzi. Je tunapaswa kuendelea kuamini kuwa aliamrisha yale yaliyotokea? Kuna uzito gani kumpatia Tundu Lisu haki yake kwa kuwahoji na kuwashtaki waliohusika na shambulizi lile?