Nani aliagiza na waliohusika kumshambulia Tundu Lisu? Serikali itoe kauli au ifunge jalada

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,339
29,137
Kwa mujibu wa yanayoendelea nchini sasa ni kwamba wananchi wengi hawaamini kauli nyingi za serikali hususani zinazotolewa na Jeshi la Polisi kuhusu masuala ama matukio ya kinyama waliyofanyiwa upinzani.

TUndu Antipas Lisu ni Mtanzania anayestahili haki zote za kikatiba na kisheria. Haki yake ya kuishi iliingia majaribuni baada ya tukio la kinyama dhidi yake lililomlazimu kukimbia nchi huku akiwa anapatiwa matibabu.

Tumemsikia akisema waziwazi kuwa mkuu wa awamu ya Tano ndiye aliyeamuru kushambuliwa kwake kwa lengo la kutoa uhai wake. Mpaka sasa ninavyoandika hapa hakuna mtuhumiwa yeyote aliyehojiwa wala kushtakiwa kwa tukio hilo la unyama wa mchana kweupe.

IGP mstaafu alisema kuwa mwenye ushahidi tosha ni mtendewa yaani Lisu. Hivyo anatuaminisha kuwa endapo Lissu angekufa basi case ingekuwa closed kitambo. Tumejulishwa na wasamaria wema kuwa CCTV kamera zilizorekodi tukio ziliondolewa mara baada ya tukio.

Ni jambo gani linaloipa serikali kigugumizi kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya walioitia doa baya sana nchi kwa tukio lile?

JPM ni mwaka wa pili sasa hayupo na hana amri ya kuzuia uchunguzi. Je tunapaswa kuendelea kuamini kuwa aliamrisha yale yaliyotokea? Kuna uzito gani kumpatia Tundu Lisu haki yake kwa kuwahoji na kuwashtaki waliohusika na shambulizi lile?
 
Kuna shahidi yoyote wa hilo tukio mkuu aliyekueleza alichokiona hadi sasa?
Inawezekana ndio maana wanasema muhusika wa ushahidi ni tundu mwenyewe na associates wake. Hii kesi haina hata mpita njia anayefahamu kilichotokea.
Au mimi ndio sijui?
 
Hivi Ben saanane ndo walishaua eti?
Aliyeamrisha alikwisha kufa lakini Bashite aliyesimamia zoezi bado yupo hai, na wala haguswi.

Ndiyo maana nakubaliana na wake wanaosema kwamba Sabaya anakomolewa, siyo kwa sababu ya uovu dhidi ya wananchi bali kwa sababu ya kuwadharau wakubwa.

Japo Sabaya ni mwovu lakini uovu wake, siamini kama unauzidi ule wa Bashite.
 
Bashite ni mtu mbad....ila Kila jambo Lina mwisho wake
 
Kuna shahidi yoyote wa hilo tukio mkuu aliyekueleza alichokiona hadi sasa?
Inawezekana ndio maana wanasema muhusika wa ushahidi ni tundu mwenyewe na associates wake. Hii kesi haina hata mpita njia anayefahamu kilichotokea.
Au mimi ndio sijui?
Camera za CCTV eneo la tukio ndiyo msema kweli.

Kuna nini hadi zitolewe baada ya tukio?
 
Ben Saanane
Azorry Gwanda
Lwajabe
N.K.

Majibu yanahitajika kwa sababu kama walikuwa wahaini, nani aliwasomea hukumu kwa kesi ipi?
Watu wakiamua kuwa wabaya wanakuwa wabaya aisee,wote hao walipitiwa?....daaa
 
Aliyeamrisha alikwisha kufa lakini Bashite aliyesimamia zoezi bado yupo hai, na wala haguswi.

Ndiyo maana nakubaliana na wake wanaosema kwamba Sabaya anakomolewa, siyo kwa sababu ya uovu dhidi ya wananchi bali kwa sababu ya kuwadharau wakubwa.

Japo Sabaya ni mwovu lakini uovu wake, siamini kama unauzidi ule wa Bashite.
Bashite atakamatwa tu
 
Chinjachinja alisha chinjwa. Ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga
Alishika bunduki na kumshambulia Lisu?

Au kuna jambo linafunikwa kwa kumtajataja yeye pekee?
Nani aliruhusu ama kutoa silaha zilizoenda kwenye tukio?
Nani alifyatua risasi?
Nani aliendesha gari?
Nani aliondoa CCTV camera?
Majibu ya jumla yanaashiria kuna jambo linafunikwa. Sheria inyooshe hata kama alitoa amri marehemu nani alitekeleza na wahukumiwe au wawekwe huru
 
Watu wakiamua kuwa wabaya wanakuwa wabaya aisee,wote hao walipitiwa?....daaa
Na kumbuka.mchezo wa kuchezea katiba na chaguzi vimegharimu maisha ya wengi. Akwilina aliuawa akiwa siyo mshiriki wa maandamano.

Aliyesababisha maandamano sasa ndo boss Tume ya Uchaguzi. Je unadhani haya ni bahati mbaya?
 
Bashite atakamatwa tu
Labda wamkamate kumtumia.kama turufu ya uchaguzi 2025.

Lakini kuna projects nyingi chafu amezifanya na dola ilitoa sapoti kwake. Alifikia hata kumdharau Waziri Mkuu kuwa anawalea wanaofanyabiashara ya shisha....

Watu wengi wamebambikiziwa kesi za unga.

Roma Mkatoliki kakimbia nchi kwa sababu ya....

Amenyimwa visa ya kuingia Marekani. Na hakuna taarifa yeyote ya Tume ya Haki za Binadamu inayomtaja kwenye kushiriki kwa matukio ya uvunjivu wa haki hizo.....

Mkuu. Huyo ni dawa ya nyumba, haguswi.

Tuingize madarakani chama kitakachoheshimu utawala wa sheria ili tuanze upya
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom