Elimu bure bado ghali kwa badhi ya wazazi, baadhi ya Wazazi Washindwa kupeleka watoto shule

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
Baadhi ya wazazi katika wilaya Ya Hai, mkoani Kilimanjaro, wameshindwa kuwapeleka watoto wao kuanza kidato cha kwanza kwa mwaka 2023 kutokana na Kukosekana kwa fedha za michango mbalimbali inayofikia kiasi cha shilingi laki na sabini kwa kila mwanafunzi.

Aidha Baadhi ya wazazi Wengine ambao watoto wao wamefaulu kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka huu wa masomo 2023 nao wamedai kushindwa kutimiza malengo ya watoto wao waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2024 kwa kile kinachodaiwa kuwa pesa anayotakiwa kulipa mzazi kwa mwaka ni karibu laki mbili kwa mwanafunzi mmoja ambayo ni jumla ya michango yote ndani ya kipindi cha mwaka wa kwanza wa masomo.

Daniel Inyasi Moja ya mzazi toka kijiji cha Kimashuku amesema yeye watoto wake wawili wamefaulu kwenda kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2024 lakini kulingana na hali yake ya uchumi kuwa mbaya hatoweza kuwagharamia watoto wawili kutokana na wingi wa michango kuwa mingi huko shuleni hivyo watabaki nyumbani.

Aidha amedai kuwa pia kuna baadhi ya wazazi kijijini hapo ambao wameshindwa kuwapeleka watoto wao shule kutokana na Kukosekana kwa pesa za kulipia utitiri wa michango shuleni. Baadhi ya wazazi wameomba serikali kuangalia namna ya kusaidia zile familia zisizojiweza kumudu gharama za michango mbalimbali huko shuleni ili watoto wao wapate elimu.
 
Serikali sikivu ingesikia kilio cha wananchi wake
 
Wanasemaga mkoani Kilimanjaro hakuna masikini.
Hao masikini wa Hai wametoka wapi wakati huko wote ni matajiri, wachapakazi na watafutaji?
 
Back
Top Bottom