Dah ni hatari, kumbe hawa walimu walikaa muda mrefu pale, Mi nimepiga advance pale 2010-2012 na hao wote nimewakuta, ila hostel alikua Nwl Maijo (ana matusi balaa). Mtefu(R.i.p) nilimwacha pale. Na akina Landi, Mwakyububu, pia Mng'ong'o (R.i.p) nilimuacha. Mageta na Njegite. Mageta akiwa 2nd master na Njegite akiwa Head Master. Hadi naondoka 2012 Mtindo wa Gate pass ulikuepo kama kawa na kufyatua tofali, kung'oa visiki, kuzibua vyoo hizo ziliendelea kuwa adhabu za muda wote pale.
Simwaba na Language yake pia nilimuacha, chips za califonià kama kawa walaji waliendelea kujigongea.
Wale wa Hostel Idi simba kubwa iliendelea kuwa nyumba ya burudani siku za welcome form 5, na weekend days kwa ajili ya movie.
Bwalo la chakula liliendelea kuwa shida badala yake watu walilia chakula mabwenini au kwenye viunga pale kwenye masanamu ya wanyama.