Namtafuta Baba yangu aitwaye Peter Matiko

Namtafuta Baba yangu aitwaye Peter Matiko

Status
Not open for further replies.
Mambo Vipi Naitwa Noel Matiko, namtafuta baba yangu aitwaye Peter Matiko, walipotezana na mama yangu aitwaye Omega Macha maeneo ya Njiro Arusha miaka ya 1998

Sikuwahi kumuona ningefurahi sana kupata taarifa zake, kama akipata ujumbe huu au kwa yeyote anayejua alipo anitafute kwa simu namba 0676238390

Natanguliza shukrani!
Anza na Ester Matiko aka Covid 19
 
Kama mama yako aliolewa na mwanaume mwingine akachukua jukumu la kukulea huyo ndie baba yako au mwanaume yoyote aliekulea mpaka kufika hapo huyo ndie baba yako wacha kupoteza nguvu zako kumtafuta biological father maana usitegemee kupata chochote Cha maana zaidi ya salamu hakuna namna unaweza fanya kwa Sasa ukapata ule upendo halisi wa baba na mtoto.

Endelea kumtafuta ila nakusihi usitarajie makubwa baada ya kuonana nae.
Usifate huu ushauri.. Dizaini hizi wengi wana historia mbaya na umimi...
Mtafute baba yako, Achana na yaliopita kwa wazazi wako hayakuhusu...
Kama salamu unatoa na umezipokea lakini sisi binadamu uwepo wetu hapa una siri nzito......
 
Usifare huu ushauri.. Duzaini hizi wengi wana historia mbaya na umimi...
Mtafute baba ako, Achana na yalio piyta kwa wazazi wako hayakuhusu...
Kama salamu unatoa na umezipokea lakini sisi Binadamu uwepo wetu hapa una siri nzito......
Noted, boss!
 
sawa, japokua sijajua jinsi ya kulink na hiyo mifumo ya utambuzi
Acha uvivu na ugoigoi changamka kijana, hapa unapewa pakuanzia sio lazima utafuniwe kila kitu.

Kwa mfano ukiona matokeo ya shule fulani kuna mtu mnafanana majina yote ya mzazi utashindwa pa kuanzia? hiyo mifumo hujui ni ofisi gani zinazoiendesha? Come on
 
noted, boss!
Kama kweli unamtafuta Baba yako basi jua hiyo ndio damu na mzee wako nae hana raha anakuwaza sana...
Huenda uko kuna dada au kaka zako..
Shangazi hata Baba wakubwa kwa wadogo, pia huenda bibi au babu yako wako hai basi furaha ya kukuona itaongeza baraka na amani maishani mwako..
Mwenyezi Mungu akuangazie..
 
pamoja mkuu
Ila tu cha msingi kama ukifanikiwa kupata mawasiliano yake au alipo tafadhali nenda taratibu na kwa hekima kubwa kabisa maana yawezekana ana familia nyingine na hajaiambia chochote kuhusu uwepo wako hivyo itabidi utumie mbinu mbadala kama utakuta hali hiyo ili familia yake ibaki salama.

Lakini pia achana na hao wanaosema usimtafute kwa sababu wanafikiri upande mmoja pekee, wao wame base sana kwa wewe kupata msaada kutoka kwa huyo baba, wewe nenda na yote, maana kwa mfano: ni vipi kama baba yako huyo yupo katika hali ngumu sana sana ya maisha au kiafya kutokana na kuwa na kipato duni ilihali wewe una hali nzuri kifedha? Huoni kumtafuta kwako kutamuokoa?

Nina mfano hapa rafiki yangu naye alimtafuta sana baba yake kwa mda mrefu kumbe yule mzee alikuwa hoi anaumwa kalazwa pale BUGANDO na hana msaada kwani hali yake ngumu na bahati mbaya mke aliye oa hakujaliwa kupata nae mtoto lakini aliishi naye hivyo na yupo anamuuguza pale tatizo ni kukosa pesa laki 7 tu ya upasuaji

Sasa jamaa alipo enda kumtembelea mfanya kazi mwenzie aliye pata ajali ya gari ndio anasikia manesi wana elezana kwenye korido kwa kutaja jina la mgonjwa kwamba wanataka wamruhusu tu aende nyumban maana hata akibaki pale hakuna cha kufanya, ndio jamaa alipo sikia jina linatajwa ndio kuuliza kwa manesi akapewa maelezo alipo ruhusiwa kwenda kumuona huyo mzee na kumdadis maswali kumbe ni baba yake mzazi kabisa

Jamaa akalia sana na hasa akiangalia hali na hadhi yake halafu na hali aliyo nayo baba yake mazazi pale kitandani na hapo ndio ikawa pona ya mzee maana alimsafirisha akaja kutibiwa hapa muhimbili na yupo safi hadi sasa na anazidi kumpa baraka mtoto wake

Na jamaa kiumweli kabisa ananiambia mambo yake yameanza kumyookea na hasa baada ya kufanikiwa kumpata baba na kubwa zaid kumnusuru na kifo cha maradhi ya kukosa pesa

Huo ni mfano dhahir kabisa ulio mtokea rafiki yangu wa karibu kabisa

Lakini pia waweza tumia facebooj, tweeter au mitandao mingine ya kijamii we andika tu majina ya baba huyo kwenye search bar lazima yatakuja majina yanayo fanana anzia hapo
 
Acha uvivu na ugoigoi changamka kijana, apa unapewa pakuanzia cio lazma utafuniwe kila kitu.

Kwa mfano ukiona matokeo ya shule fulan kuna mtu mnafanana majina yote ya mzaz utashindwa pa kuanzia? hiyo mifumo hujui ni ofis gan znazoiendesha?come on
Siku hizi NECTA kwenye matokeo hawaweki majina wanaweka namba tu kiongozi hivyo ni ngumu sana

Njia nyingine ajaribu kutumia facebook andika majina hayo ya baba yako unaweza kuta yanatokea labda watoto wake au yeye mwenyewe
 
Ila tu cha msingi kama ukifanikiwa kupata mawasiliano yake au alipo tafadhari nenda taratibu na kwa hekima kubwa kabisa maan yawezekana anafamilia nyingine na hajaiambia chochote kuhusu uwepo wako hivyo itabidi utumie mbinu mbadala kama utakuta hali hiyo ili familia yake ibaki salamanders

Lakini pia achana na hao wanao sema usimtafute kwa sababu wanafikiri upande mmoja pekee, wao wame base sana kwa wewe kupata msaada kutoka kwa huyo baba , wewe nenda na yote, maana kwa mfano : ni vipi kama baba yako huyo yupo katika hali ngumu sana sana ya maisha au kiafya kutokana na kuwa na kipato duni ilihali wewe una hali nzuri kifedha ? Huoni kumtafuta kwako kutamuokoa ?

Nina mfano hapa rafiki yangu naye alimtafuta sana baba yake kwa mda mrefu kumbe yule mzee alikuwa hoi anaumwa kalazwa pale BUGANDO na hana msaada kwani hali yake ngumu na bahati mbaya mke aliye oa hakujaliwa kupata nae mtoto lakini aliishi naye hivyo na yupo anamuuguza pale tatizo ni kukosa pesa laki 7 tu ya upasuaji

Sasa jamaa alipo enda kumtembelea mfanya kazi mwenzie aliye pata ajali ya gari ndio anasikia manesi wana elezana kwenye korido kwa kutaja jina la mgonjwa kwamba wanataka wamruhusu tu aende nyumban maana hata akibaki pale hakuna cha kufanya, ndio jamaa alipo sikia jina linatajwa ndio kuuliza kwa manesi akapewa maelezo alipo ruhusiwa kwenda kumuona huyo mzee na kumdadis maswali kumbe ni baba yake mzazi kabisa

Jamaa akalia sana na hasa akiangalia hali na hadhi yake halafu na hali aliyo nayo baba yake mazazi pale kitandani na hapo ndio ikawa pona ya mzee maana alimsafirisha akaja kutibiwa hapa muhimbili na yupo safi hadi sasa na anazidi kumpa baraka mtoto wake

Na jamaa kiumweli kabisa ananiambia mambo yake yameanza kumyookea na hasa baada ya kufanikiwa kumpata baba na kubwa zaid kumnusuru na kifo cha maradhi ya kukosa pesa

Huo ni mfano dhahir kabisa ulio mtokea rafiki yangu wa karibu kabisa
Nashkuru sana boss
 
Kama alikuwa mwanajeshi hao jamaa wana Taarifa za watu wao, vyema uende kambi iliyo Karibu nawe watakupa msaada utaratibu gani huwa unafuatwa unapomtafuta Ndugu au mzazi wako.

Jitahidi nawe uwe na maelezo yaliyonyooka
 
Kama alikuwa mwanajeshi hao jamaa Wana Taarifa za watu wao vyema uende kambi iliyo Karibu nawe watakupa msaada utaratibu gani huwa unafuatwa unapomtafuta Ndugu au mzazi wako

Jitahidi nawe uwe na maelezo yaliyonyooka
Shukrani sana mkuu
 
shukrani sana mkuu
Pata taarifa zake kambi alizofanyia kazi ikibidi cheo chake wakati huo asili yake

Nina hakika utampata maana hata kama amestaafu Taarifa zao zinakuwepo........wakati mwingine hata wa depo yake inawezekana bado wapo kazini
 
Mkuu acha kabisa kuna watanzania ni mbumbumbu sana aisee.
Yaani wamekariri kwamba mtu akimtafuta ndugu yake labda lengo ni kwenda kuomba msaada tu kumbe wengine hufanya hivyo just kwa ajili ya upendo tu.
Mimi nina uzoefu wa kesi kama hizi jinsi gani watu waliolelewa na mzazi mmoja mateso wanayoyapata hasa ya kisaikolojia hata kama wanapata huduma zote.
Nilishawahi kuwa na rafiki yangu mmoja nilisoma naye alikuwa analelewa na mama yake tu na baba yake alikuwa hamjui.
Yule jamaa alikuwa anapewa kila kitu na mama yake yaani huduma zote muhimu alikuwa anazipata na alisomeshwa kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu.
Licha yule rafiki yangu kupata huduma zote muhimu lakini kuna kipindi alikuwa anakosa amani kwa kutomjua baba yake yaani ilikuwa inamkwaza,alitamani kumjua tu huyo baba yake yupoje na anafananaje hata kama hatopewa huduma yoyote.
Hii hali huwa inatokea kibinadamu.
Sasa huwa nashangaa mtu anapojitokeza kuomba msaada wa kumtafuta mzazi wake watu wanaanza kuuliza maswali ya kejeli na comments za ajabu ajabu.
Duh, kwahio unamtishia au vipi, sasa kama sio kutaja jina angepataje msaada wa haraka zaidi ? Nawe ulivyo mjinga kwanini usingeenda tu inbox kwake ukampa taarifa ambazo zingemsaidia kumuona baba yake,? Na mbona unamtuhumu kua hana shukrani? Yani mtoto apoteze muda kumlea mama yake mzazi aliyemzaa na kumbeba miezi 9,? Au nyie mmezaliwa na mbuzi hadi kufikia kuona MTU anayetunza au kutafuta mzazi wake anaonekana mjinga, wewe kumfichia habari na kumtishia imekusaidia nini au itakusaidia nini wewe binafsi? Yani hapa ndipo ambapo naona watanzania wengi ni BOGUS kabisa...ukitafuta mzazi unaonekana labda unataka Mali za urithi, wengine wanataka tu maongezi na kumfahamu mzazi wake halisi, au wewe una share katika hio familia yake mpya unayojitapa nayo ..jitathmini na jifikirie kijana.
 
Mkuu kwanza nikupe pongezi kwa kukumbuka hilo.
Damu ni nzito kuliko maji.
Mimi nitakusaidia kutuma meseji yako kwenye magroup mbalimbali, nina rafiki zangu wakurya watasaidia kumtafuta.
Usijali penye nia pana njia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom