Utatendewa namna ambavyo na wewe unamtendea mwenzi wako

mkushiOg

Member
Feb 17, 2024
52
122
Habari wana jamii, me nmekuwaga msomaji wa humu muda mrefu tu na mm sasa nimeamua kuwa member.


Moja kwa moja kwenye mada eewe mume mjali na mpende mkeo hata kwa 60% then endelea na mambo yako ya nje huko.

Sasa wewe huonyeshi mahaba kwa mkeo michepuko imekuzidiaa tendo la ndoa ni lakutafuta kwa tochi kweli jamani? Anza kwanza kumpa hiyo haki ya tendo mkeo then toka nje kaendeleze kwa michepx jamani siyo unaenda malizwa hamu yote huko ukirudi nyumban upo hoi humgusi mwenzako unadhan yeye anaishi vipi?

Charity begins at home jamani. Mjali mpe vizawadi suprise za hapa na pale mtoe hata dinner mara moja kwa miezi mitatu yaan mfanyie vile tuvitu vitu vya kipindi unamtongoza hapo kama ulimpata mke utainjoy ndoa yako na kazi zako za nje (michepuko)itaenda bila makelele kinyume na hapoo haya malalamishi ya ndoa hivi ndoa vile hayataisha.

Ila sasa ww unamsahau mkeo kweli jamani then akianza chat na x kamzozo akitoka out kelele mnatakaje jamani? Kwani ni mfungwa huyo? Na hao wanawake ni binadamu pia so tujitahidii kutendeana mema katika hizi ndoa na tutaziinjoy.

NB: hapa siongelei wale wanawake makurumbembe yale ambao wamezaliwa na nature ya umalaya hata wapate mume mwema wenyewe hawatulii na pale wanapompata mwanaume mbayaa ndo kabisaa wanafanya usaliti kama maji yakunywa.
 
Sasa wewe huonyeshi mahaba kwa mkeo michepuko imekuzidiaa tendo la ndoa ni lakutafuta kwa tochi kweli jamani?
Wanaume wengi wameoa wanawake wasio wapenda. Vigezo walivyozingatia ni heshima, ukarimu na uaminifu wa mwanamke na siyo sexual chemistry na sexual magnetic attraction iliyopo kati yao.
 
Back
Top Bottom