Hata mie sielewi mkuu,
Uanze kusema kuwa, unajua sweetie, baba yangu ni mchawi, kaurithi uchawi kwa bibi yake mzaa mama. Na mama yangu ni mwizi namba moja pale mtaani....Halafu, dada yetu mkubwa ni changudoa.....
Huyo GF/BF naamini atakuona kama nati fulani za kichwa zimelegea!!
BAK,
Haina tija kueleza negatives za familia yako, labda kama kuna sababu ya msingi au zitaingia katika equation ya maisha yenu huko mbele ya safari.
Na umri wangu huu, kuna mambo kibao ya familia yetu ambayo sijawahi kumweleza Bibi DC na wala sitamwambia. Naamini hata yeye akija kuyajua hataniuliza kwa sababu yajaadhiri ndoa yetu kwa namna yoyote ile.
Babu DC!!