Namna ya kumkamata mwanaume!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namna ya kumkamata mwanaume!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mama Ashrat, Apr 29, 2012.

 1. M

  Mama Ashrat Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I was single once, but now i'm a wife and a mother. Nimekaa nikaona sio vibaya iwapo nta-share tips kadhaa zilizonisaidia kumuweka baba Ashrat sawa na mpaka leo hii sijawahi kuhisi wala kugundua kwamba anatoka nje ya ndoa yetu, japo matatizo ya hapa na pale hayakosekani ila tumedumu na bado tunaendelea na safari.

  Unapokutana na mwanaume akakutongoza/mwanamke akakukubalia kuna uwezekano mkubwa kuwa amevutiwa na wewe kweli au kakutamani tu. Kitu ambacho watu hua wanasahau ni kwamba hata mtu aliyekutamani tu unaweza ukampa mwongozo/sababu mpaka mwenyewe akajikuta anakupenda kuliko ambavyo angeweza kutarajia kwamba angewahi kupenda. Ndio maana hata wale waitwao 'bad girls/boys' hua wanajikuta wamenaswa na kunasika at some point.

  1. Usiigize.
  Maigizo waachie wasanii wetu, kuwa vile ulivyo kweli kimaisha/kitabia (isiwe mbaya)/mazoea n.k

  2. Don't move too fast/act desperate.
  Usitumie ule muda wa mwanzo kabisa wa mahusiano yenu kutaka kujua "una malengo gani na mie?" "utanioa?" "Kanitambulishe/nataka nikakutambulishe." n.k Mpe nafasi ya kukusoma na kupata kujua wewe ni mtu wa aina gani, je unafanania na mwanamke ambae angependa kuwa nae kwa muda mrefu, possibly hata ndoani? Na wewe nawe tumia muda huo kufanya kitu hicho hicho.

  3.Don't be too demanding.
  Huyo sio baba yako wala sio mume just yet, hivyo chochote atakachokufanyia kinatokana na yeye kutaka/kupenda kufanya hivyo na sio kwakulazimika. Haki hiyo hauna.

  4. Kuwa na shukurani.
  Learn to appreciate all that he does for you, that way ataona umuhimu wa hayo anayokufanyia, yawe makubwa au madogo.

  5. Be real.
  Badala ya kufika kwake na kuanza kushangaa anaishije bila ya mfanyakazi wa ndani huku ukitamba kuwa wewe huwezi, shangaa anawezaje weka nyumba yake katika hali nzuri mwenyewe bila ya msaada. Hii itaonyesha fika wewe utakua mke wa aina gani hapo baadae, kama ni wale wakukaa miguu juu huku wakiagiza hata maji waliyoombwa na mume au la.

  6. Learn to cook if you don't know how to.
  Waliosema "the way to a man's heart is through his stomach" hawakukosea. Ukiachilia mbali wale watu wachache wanaokula ili kushiba wengi hua wanajali ladha. Hiyo ndio hua inawaongezea hamu ya kula na kuwarudisha nyumbani mapema pia kuwafanya wakumiss pale inaposhindikana kula chakula chako . Kwakumwonyesha mwanaume kwamba hata tumbo lake unaweza kuliridhisha unamwongezea sababu za kukuweka kwenye maisha yake.

  7. Mheshimu.
  Mpe heshima yake kama mwanaume wako ila usimwogope. Wengine wote usiwape nafasi kumfanya ajisikie kwamba haheshimiki.

  8. Kuwa ngao yake.
  Inapotokea anakumbwa na matatizo yoyote yale onyesha utayari wa wewe kuwa pamoja naye kwa hali na mali mpaka yatakapoisha. Pia usikose kumjali kumpa moyo pale unapoona inahitajika.

  9. Kuwa muwazi.
  Kama kuna mambo ambayo unajua moja kwa moja yatakuwa sehemu ya mahusiano yenu (watoto/X mkorofi .nk) mweleze mapema ili aamue kama yuko tayari kudeal nayo au la.

  10. Usiwe na chuki.
  Kikifika kipindi cha yeye kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake onyesha ushirikiano. Usionyeshe chuki wala kujiona kana kwamba wewe ndio wewe.

  11. Give your all.
  Kama na nyie mtaamua kuonjeshana tunda kabla (kama ambavyo wengi wanafanya karne hii) basi kuwa mbunifu, mtundu na usiwe mvivu.

  12.Pendeza.
  Vaa/onekana vizuri unapokuwa nje hata ndani pia. Usisahau kuzingatia/jali hisia zake kuhusu mavazi yako.

  13. Onyesha interest kwa yale ayapendayo yeye.
  Usiwe mbinafsi kila siku unataka kusikilizwa wewe tu na story/mambo utakayo wewe. Uliza/jua kuhusu yale anayopenda yeye mf. mpira/siasa.

  14.Kuwa mtulivu.
  Usiwe mtu ambae kila saa simu yako inapigwa pigwa na wanaume wasio ndugu wala marafiki wakaribu na wanaoeleweka. Discpline ni muhimu sana.

  15.Usimzonge.
  Usiwe mmoja wa wale watu wanaofuatilia wenzi wao masaa yote wanapokuwa hawapo pamoja. Mpe nafasi ya kuwa na marafiki zake bila kuhitaji kuzima simu ama ku-ignore simu/text zako.

  16. Mfurahishe/chekeshe.
  Joke around sio muda wote yeye ndio awe wakukufurahisha wewe.

  17. Jifunze kusamehe.
  Mambo madogo madogo yanapoombewa msamaha samehe na uache yapite.

  18. Mshirikishe Mungu wako.
  Ukishaona kwamba huyo ndie basi mshirikishe yule unayemwamini ili upate mwongozo wa kiroho.

  Mama Ashrat.
   
 2. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Karibu Mama Ashrat, kuku mgeni hakosi kamba mguuni
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana ingawa hilo la mwisho nahisi linafaa kuambatana na kila unachofanya.
   
 4. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Mama Ashraf nimekusoma!
   
 5. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Safi sana mama ashrat, tatizo wake wa karne hii wanapenda waonekane wao ndio wao, mume kama pambo tu ndani ya nyumba la kumuwezesha nae aonekane ameolewa. Maadili ya wake kwa waume zao yameporomoka sana

  Mke unakuta yeye kazi yake kubwa ni kukuwinda tu aone wapi umeteleza hata kama ni kwa ishu ndogo ndogo ambazo sometimes na yeye anakuwa amechangia. Baada ya hapo ni ugomvi kwa kwenda mbele na kumjibu mume kwa maneno machafu.

  Inasikitisha sana.
   
 6. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  mh we naeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 7. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana; ila yote hiyo ni kutokuwa na maadili ya Kimungu!
   
 8. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  1. Usiigize.
  Maigizo waachie wasanii wetu, kuwa vile ulivyo kweli kimaisha/kitabia (isiwe mbaya)/mazoea n.k
  2. Don't move too fast/act desperate.
  Usitumie ule muda wa mwanzo kabisa wa mahusiano yenu kutaka kujua "una malengo gani na mie?" "utanioa?" "Kanitambulishe/nataka nikakutambulishe." n.k Mpe nafasi ya kukusoma na kupata kujua wewe ni mtu wa aina gani, je unafanania na mwanamke ambae angependa kuwa nae kwa muda mrefu, possibly hata ndoani? Na wewe nawe tumia muda huo kufanya kitu hicho hicho.madogo.

  Hapo kwenye red, hapo ndipo kinachowaponza wanawake wengi. Mpo tu mwanzo wa mahusiano hata hamjajuana vizuri anatumbukiza maneno kama hayo
   
 9. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  asante mamaaa
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Nimekukubali. Problem yetu ni desperado! Nna dadangu akiambiwa na mkaka ntakutoa jioni, anaulizia pa kupata gauni la harusi!
  Kila la kheri mama
   
 11. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Mke anashinda kwa mashosti na kufwata ushauri wa mashosti zaidi ya mme wake unategemea kutakuwa na maadili ya kimungu? haiwezekani kabisa.
   
 12. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hayo mambo ni mimi tu? yeye haitakiwi anifanyie hivo?
   
 13. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Mke mwema hutoka kwa Bwana; kwa akili zetu si rahisi kumtambua mke mwema
   
 14. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Niliachana na binti kwa kung'angania nimpangishie chumba nimfanye mke mdogo; mazuri yote nilokuwa namfanyia hakuyaona!
   
 15. m

  manasa Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waoh! nimeipenda hii topiac lakini na swali what if yeye ndo anakufatilia unapokuwa mbali?
   
 16. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Good topic but umesahu kuwa it takes two to tango. kwa upande wa wadada umetufundisha vyema. sijui pia tukusubiri uje na somo la wakaka?
   
 17. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Ukiona unafuatiliwa ujue unapendwa!
   
 18. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Wakaka huwa ni mateka kwenye mapenzi. Aliyeniteka sijawahi kumsaliti hata siku 1, kuna kipindi nahisi labda kanipa dawa.
   
 19. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  unafaa sana kua lecturer nikifungua chuo cha kitchen party university college of tanzania.
   
 20. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ....hehe...huyo 'ataolewa' na wengi.
   
Loading...