Namna ya kumkamata mwanaume!!

Mke anashinda kwa mashosti na kufwata ushauri wa mashosti zaidi ya mme wake unategemea kutakuwa na maadili ya kimungu? haiwezekani kabisa.

na waume wanashinda baa wanapata ushauri wa marafiki yaan ni tabu tupu ndoa za siku hizi,
 
Sijakataa kama utakuwa katika point zingine sio kwa mke na mme....Tukizungumzia point ya mke kama hamuogopi mme wake, lazima kuna ukosefu tu waheshima hapo....Mana anaweza kwenda popote bila ya kumuaga mme wake, na mengi tu anaweza kufanya sababu hamuogopi mme wake.

sio kweli,ukimuaga mumeo/mkeo uendapo mahali ni heshima na sio uoga
 
...Niliyoyaandika hapa ni maneno ambayo nimeyasikia kwa akina mama ambao wanapata vipigo ndani ya ndoa zao wengine ni ndugu wa karibu kabisa kwamba wanawaogopa waume zao kutokana na vipigo na wanapokuwa hawapo nyumbani wanajiona wako huru zaidi lakini waume wakirudi tu basi uoga huwajaa kwa kujua kosa dogo linaweza kusababisha kipigo.

Kutofautiana hakuna tatizo lolote au vinginevyo tungekuwa tunakubaliana kila kitu basi hili jamvi lingekuwa halina mvuto kabisa. Bado msimamo wangu ni ule ule kwamba hakuna sababu yoyote ya mke kumuogopa mumewe bali anatakiwa kumuheshimu. Ukiona mke anamuogopa mumewe basi ujue kuna walakini wa namna moja au nyingine.
Hao wanawake wanao pigwa na wanaume zao ni wehu/walevi tu kama wanaume zao, kuna sheria zipo zinaweza kuwakinga hao lazima ni wehu/walevi kama wanaume zao ndo mana wanavumiliana mana kuna kasoro kwenye ndoa zao.

Narudia tena mwanaume ambaye akili yake iko sawa sawa hapigi mke wake, hata siku moja.

Kuhusu kipishana mawazo niko na wewe hapo :A S shade:
 
Well said Mama Ashrat lakini waweza fanya mambo yote hayo na mwisho wa siku ukaambulia carbondioxide,hawa watu hawatabiriki at all..
 
Last edited by a moderator:
fazaa
Wewe ndio msemaji wa Mungu? Hayo unayoongea umeyapata wapi? Kama ni maoni yako tu basi yabaki kama yalivyo, ila kama una uhakika kwamba Mungu ndivyo anavyofanya kazi naomba vilelezo vya uhakika.
.
Sa hamaki ya nini tena, si unajua kwenye ukweli lazima ulize watu...kasome vitabu vya dini vyote vinapinga sex before marriage.
 
Nimekubali point nyingi hasa za wale wanaotaka kuolewa; ila kwa wenye ndoa maisha ni more complicated na wengi tu wenye heshima kwa waume zao ndoa zao ziko ndivyo sivyo. Na huwezi sema kuwa mumeo achiti ni siri ya moyo wake; ila ni vizuri ku think positive na kujipa moyo.

Inategemea na mume ulo nae; wengine hata walambwe hawakamatiki. Hence it takes two.

nyumba kubwa
Wanaoanza na waliomo lazima watofautiane kiutendaji. Mtu anapokuwa kwenye ndoa anatakiwa afanye kazi haswa maana majukumu yanaongezeka, familia inaongezeka na mengine mengi tu.

Swala la kuwa amechiti au la ndio maana niliishia kusema kwamba sijawahi kuhisi wala kugundua, hivyo kama amewahi basi atakua amefanya kazi ya ziada kitoruhusu ilete mabadiliko yoyote kati yetu. Mwisho wa siku tabia binafsi inahusu zaidi kuliko matendo ya mwenzi, mhuni ni mhuni tu na mtulivu ni mtulivu tu, hivyo la muhimu ni mke/mume kufanya yale awezayo yeye na yasipomtosheleza huyo mwenzi basi hafai tu.
 
Last edited by a moderator:
Sa hamaki ya nini tena, si unajua kwenye ukweli lazima ulize watu...kasome vitabu vya dini vyote vinapinga sex before marriage.

Sijahamaki ila nimeuliza maswali ambayo ni dhahiri huna majibu yake, mpaka hapo ulichosema mwanzo hakina basis hivyo ni vizuri tukafunga huo mjadala na kuendelea na mingine kama ipo.
 
Well said Mama Ashrat lakini waweza fanya mambo yote hayo na mwisho wa siku ukaambulia carbondioxide,hawa watu hawatabiriki at all..

Purple
Kweli tupu, ila huwezi kuwa acha fanya your best kwa woga wa kutomtosheleza huyo ulonae. Fanya ili akishindikana ujue alishindikana yeye na sio kwamba wewe hukufanya yale uliyopaswa kufanya kuendeleza na kuimarisha mahusiano yako.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo ni ngumu kujua kama hizo point zinafanya kazi kama huna uhakika kama kwa kuzitumia hizo njia wako amekamatika au hapana. Labda tu define "kumkamata" kuna maana gani. Kama ni kuendelea kuwa mwenye ndoa no matter what hapo poa na mimi nakubali kabisa. Kwa maana ya kuwa na uhakika mumeo hawezi tamka hata siku moja kuwa ndoa na wewe basi. Hiyo wanawake wengi tuko assured. Lakini kama atu shei na wengine mh; ngumu kuamini.

nyumba kubwa
Wanaoanza na waliomo lazima watofautiane kiutendaji. Mtu anapokuwa kwenye ndoa anatakiwa afanye kazi haswa maana majukumu yanaongezeka, familia inaongezeka na mengine mengi tu.

Swala la kuwa amechiti au la ndio maana niliishia kusema kwamba sijawahi kuhisi wala kugundua, hivyo kama amewahi basi atakua amefanya kazi ya ziada kitoruhusu ilete mabadiliko yoyote kati yetu. Mwisho wa siku tabia binafsi inahusu zaidi kuliko matendo ya mwenzi, mhuni ni mhuni tu na mtulivu ni mtulivu tu, hivyo la muhimu ni mke/mume kufanya yale awezayo yeye na yasipomtosheleza huyo mwenzi basi hafai tu.
 
Hao wanawake wanao pigwa na wanaume zao ni wehu/walevi tu kama wanaume zao, kuna sheria zipo zinaweza kuwakinga hao lazima ni wehu/walevi kama wanaume zao ndo mana wanavumiliana mana kuna kasoro kwenye ndoa zao.

Narudia tena mwanaume ambaye akili yake iko sawa sawa hapigi mke wake, hata siku moja.

Kuhusu kipishana mawazo niko na wewe hapo :A S shade:

....Hapo kwenye bold nakubalina nawe kabisa. Unamuuliza mtu kwanini unaendelea kuwemo kwenye ndoa ya mateso kiasi hiki? majibu yake ni kwamba naogopa kwenda kuanza 1, lakini huwa akinipiga anagundua kama amenikosea hivyo huwa ananinunulia zawadi za bei mbaya sana kama kunibembeleza!!:nono: ni ulevi tu ndio unamsababisha ananipiga kama hajalewa huwa hanipigi, ukimuuliza huko anakozinywea pombe zake kishawapiga wangapi? hajawahi kumpiga mtu huko anakokuwa na marafiki zake, nahofia kumshtaki maana anaweza kufungwa na watoto wetu wakanichukia kwa kusababisha baba yao afungwe na majibu mengine mengi ambayo yanakuacha mdomo wazi.
 
Kwa hiyo ni ngumu kujua kama hizo point zinafanya kazi kama huna uhakika kama kwa kuzitumia hizo njia wako amekamatika au hapana. Labda tu define "kumkamata" kuna maana gani. Kama ni kuendelea kuwa mwenye ndoa no matter what hapo poa na mimi nakubali kabisa. Kwa maana ya kuwa na uhakika mumeo hawezi tamka hata siku moja kuwa ndoa na wewe basi. Hiyo wanawake wengi tuko assured. Lakini kama atu shei na wengine mh; ngumu kuamini.
Kama sijaona tatizo basi nachukulia kwamba hamna tatizo. Kama lipo litakua acknowledged wakati huo litakapokuwa wazi, but untill then we are good.

Kukaa kwenye ndoa tu no matter what wala haihitaji kazi, ni kiasi tu cha kumwacha afanye mambo yake bila kumuuliza/taka maelezo toka kwake. Hapo huhitaji kumheshimu, wala kumjali na mengineyo maana tayari anayapata kwingine. Hii ni kwaajili ya kumuweka mtu ambae tayari anakupenda 'wewe' na sio 'nyie' maana kama ijulikanavyo mahusiano/ndoa is about giving and taking, not just taking. Huwezi ukabweteka tu ukategemea mwenzio ataendelea kuwepo hata kama anakupenda sana, itafika mahali atachoka na kwenda kutafuta mapumziko kwingine.
 
Sijahamaki ila nimeuliza maswali ambayo ni dhahiri huna majibu yake, mpaka hapo ulichosema mwanzo hakina basis hivyo ni vizuri tukafunga huo mjadala na kuendelea na mingine kama ipo.
Vizuri kama hujahamaki...

Swali gani ulilo niuliza nikakosa jibu.

Endelae tu na thread yako, lakini usiwapoteze wanaume/wanawake wengine wakaja zama kwenye dhambi.

Eti wanawake watoe matunda kama ambavyo wengi wanafanya katika karne hi..sikujua kama kuna dhambi tofouti kati ya karne hii na iilio pita...Sijui vitabu vya dini vipya viko njiani vitakuwa na picture za sex au zitasema tufanye sex kabla ya ndoa, ili mungu azibariki sana ndoa zetu :bounce:
 
BAK umeongea kitu muhimu sana. Sio ex tu ama watoto, kuna issue ya wanafamilia wakorofi pia. Hii tabia (hasa ya wadada) ya kujifanya unatokea familia takatifu is really disgusting. Hata kama babako mchawi muambie mwenzio, ajue u don't side with mambo yake. Ili hata huko mbele ya safari akikusakama nao umuambie the loss is his asiwacheke ndugu zako manake nao ni sehemu yenu.
Asante rafiki.

King'asti,

Nakubalina na wewe ila timing ya kuongea hayo mambo ni muhimu sana. Kuna mambo ya kuongea mwanzoni mwa mahusiano especially yale ambayo yanahusu maisha yenu binafsi. Ila mambo ya familia zenu ni vizuri yakaja baadaye sana kama mnaona kuwa mahusiano yenu yana dire na mwelekeo. Na bado, kuna mambo ya familia ambayo si lazima mwenzi wako ajue..!!

Katika hili, watu wanatakiwa kuwa makini ili asijeuza silaha za maangamizi!!

Babu DC!!
 
Hao wanawake wanao pigwa na wanaume zao ni wehu/walevi tu kama wanaume zao, kuna sheria zipo zinaweza kuwakinga hao lazima ni wehu/walevi kama wanaume zao ndo mana wanavumiliana mana kuna kasoro kwenye ndoa zao.

Narudia tena mwanaume ambaye akili yake iko sawa sawa hapigi mke wake, hata siku moja.

Kuhusu kipishana mawazo niko na wewe hapo :A S shade:

Mkuu fazaa

This is too much...kama huamini kwamba wapo wanawake wenye akili, hekima, busara na utaalamu wao lakini wanakuwa absued basi nakuomba ukae kimya. Tumeshuhudia mama zetu, dada zatu, watoto wetu na sasa wajukuu wanapigwa na wanaume na bado wana akili nzuri. Labda kama mwenzetu ni mgeni katika tamaduni zetu!

Naomba pia kukujuvya kwamba kuna wanaume nao wanapigwa na wake zao na hawako tayari kuchukua hatua za kisheria.

Si unajua mtu aliye ona mwezi anaweza kusema unamulika kuliko jua.

Kukosa kujua, ni swa sawa na usiku wa giza.

Hao wanawake wote mara nyingi sana wanaonewa kwa kutaka wao...wawe ma bibi zetu, mama zetu, dada zetu hakuna sheria inayo sema mwanaume amtukane mke wake.
 
Mama A, All men ought to commit the wisdom displayed in this article for as long as they live.
100% ACCURATE!

Women become dissatisfied when their men neglect them EMOTIONALLY AND MENTALLY!
 
sure!ni jambo jema kutimiza wajibu wako kuepuka majuto pindi mambo yaendapo mrama..

Purple,

Pia mimi naamini kwamba endapo utatimiza wajibu wakao halafu mwenzi wako akashindwa kutambua hilo, hata ukiamua kumpiga chini hutajiona mwenye makosa siku zote.

Tatizo ni kwamba watu wanafanya vitu kwa kutegeana kiasi kwamba inapotokea wakashindwa kuendelea, kila mtu anabaki kumlaumu mwenzake na wengine kujilaumu wenyewe na kujiona wenye hatia!

Babu DC!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom