SoC02 Namna ya kukidhi matakwa ya wateja na kufanikiwa katika biashara

Stories of Change - 2022 Competition

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,852
18,261
Utangulizi
Ili uweze kufanikiwa katika jambo lolote lile, ni lazima ufuate kanuni na taratibu zitakazokuwezesha kufika kwenye kilele cha mafanikio. Hakuna mafanikio yasiyokuwa na utaratibu au kanuni. Wafanyabiashara na wajasiriamali wengi mnaowaona wamefanikiwa katika biashara wamepitia njia ngumu hadi kufikia hapo walipo. Biashara ni sayansi. Kufanya biashara na kufanikiwa kunahitaji mambo ya msingi ambayo kila mfanyabiashara anapaswa kuyafuata kikamilifu ili kufikia ufanisi. Jambo lolote unalofanya katika biashara linalenga kukidhi matakwa ya wateja.

Mbinu mbalimbali katika kukidhi matakwa ya wateja
Biashara yoyote ile ili ifanikiwe ni lazima ikidhi matakwa ya wateja. Unapobuni wazo la biashara ni lazima ujiulize biashara unayoibuni itakidhi matakwa gani ya wateja. Sote tunafahamu kwamba wateja wanahitaji bidhaa au huduma. Sasa kabla ya kuanza biashara jiulize swali hili: je, huduma au bidhaa nitakayouza itakidhi matakwa gani ya wateja wangu? Na si hilo tu bali unatakiwa ujiulize kama hiyo huduma au bidhaa ina naksi sokoni.

Ikiwa bidhaa tayari inatolewa na wafanyabishara au wajasiriamali wengine, hebu jaribu kufanya utafiti uone pengo ambalo bado halijazibwa. Kwa mfano, tuchukulie biashara unayotamani kuanzisha ni ya kuuza chai, jiulize ni nini kinachokosekana kwenye chai iliyopo sokoni ili ukiongeze. Ikiwa wauzaji wengine wanauza chai ya rangi ya kawaida, wewe jikite kuuza chai iliyotiwa viungo au chai ya maziwa ili uweze kukidhi mahitaji ya soko (matakwa ya wateja).

Pamoja na kuziba pengo la bidhaa au huduma, unapaswa kujiuliza iwapo wateja wako wana uwezo wa kulipia bidhaa yako baada ya kuiboresha. Kumbuka uboreshaji pia unaambatana na gharama za ziada kwani utapaswa kuzingatia gharama hizi unapopanga bei ya bidhaa. Usiingie tu kichwakichwa kuboresha bidhaa bila kusoma kwanza uwezo wa wateja kununua bidhaa hiyo.

Wakati marehemu mzee Mengi anaanzisha biashara ya maji ya chupa sio kwamba maji hayo yalikuwa hayauziki mitaani. Zamani wauzaji walikuwa wanajaza maji kwenye ndoo na kuwauzia wapita njia kwenye kikombe. Mzee Mengi alifanya uchunguzi akaona kuna pengo halijazibwa katika biashara hii kama vile usafi na usalama wa maji, ufungishaji na ubebaji (potability). Ndipo akaja na wazo la kufungua kiwanda cha maji ya kunywa. Mwanzoni watu walimbeza na kumsema kwamba “huyu mchanga anapenda hela, tazama anauza hadi maji”! Taratibu, kadri siku zilivyosonga mbele, walaji walianza kumuelewa. Biashara ilipofamikiwa, wafanyabiashara wengine wakamuiga na kuanza kuzalisha maji ya chupa.

Mfano mwingine ni kuanzishwa kwa mitandao ya kijamii kama vile facebook, WhatsApp, instagram, telegram, tiktok, nk. Watu walioanzisha majukwaa haya waligundua kwamba watu wanahitaji kuunganika na wengine. Waligundua watu wengi wamepotezana baada ya kumaliza shule na vyuo, kustaafu kazi nk, hivyo kuna haja ya kuwaunganisha pamoja. Hata mwanzilishi wa JamiiForums alilenga kuwaunganisha watu pamoja kupitia mijadala mbalimbali mtandaoni, ndipo akaja na wazo la kuanzisha jukwaa hili muhimu kwa ajili ya watu kutoa mawazo na maoni yao kwa uhuru.

Wafanyabishara wengi hawazingatii suala la huduma nzuri kwa wateja. Hili ni kosa kubwa sana. Uliwahi kufikiria kwanini, kwa mfano, kule Kariakoo watu wengi wanauza bidhaa zinazofanana lakini baadhi yao wana wateja wengi kuliko wenzao? Jibu ni huduma nzuri kwa wateja. Jamaa yangu mmoja aliwahi kufungua duka la pembejeo za kilimo na biashara yake ikastawi sana lakini baada ya kubadilisha muuzaji, biashara iliyumba hadi ikafa jumla. Tatizo aliondoa huduma nzuri kwa wateja na kuleta huduma mbovu. Baadhi ya wafanyabishara wanadhani wakiajiri wasichana warembo kuuza biashara zao watauza sana. Kwani wateja wanakuja kuwachumbia hao wasichana hadi wavutike kuja kununua? La hasha. Wateja hawaangalii sura bali wanataka huduma nzuri. Ikitokea msichana akawa mrembo na huduma nzuri kwa wateja, hiyo ni sawa lakini urembo tu haujawahi kuwavutia wateja hata siku moja.

Waanzishaji wa magazeti na blogu za udaku waligundua watu wanapenda kupata habari nyepesinyepesi za umbeya na uwongo ili kufurahisha nafsi zao. Wanadamu wanapenda kufahamu taarifa za wengine hata kama haziwasaidii kitu chochote ilmradi tu wapate la kujadili. Wanapenda kujua nani kafumaniwa, staa gani kaachia koneksheni au nani kaachika, nk. Ndio maana mtu akipata skandali au akiongea jambo la ajabu linavuma sana. Hii tayari ni biashara. Wamiliki wa magazeti ya udaku hutumia tabia hizi za binadamu kuuza huduma na kufanikiwa kibiashara kwa kuwa soko lipo tele. Usishangae kukuta magazeti ya udaku yanauza zaidi kuliko magazeti yanayoandika taarifa zenye maarifa.

Shauku ya mtu kutaka kujilinda nalo ni takwa ambalo wafanyabiashara hulitumia kuanzisha biashara. Wauzaji wa dawa za tiba mbadala, wenye makampuni ya ulinzi na bima wapo kwenye kundi hili. Waganga wa tiba mbadala watakuambia ili kuondoa sumu mwilini, kujikinga na kisukari, kuondoa lehemu mwilini, nk, tumia dawa hii. Wanachokifanya ni kukujengea hofu ili utamani kujilinda zaidi. Hapa mtu unaweza kufanya biashara nyingi sana kuanzia kwenye ulinzi wa afya na mali. Kuna kampuni nyingi zinazotoa huduma za afya na zina wateja wa kutosha. Wajasiriamali walioanzisha kampuni hizi walilenga kukidhi haja za wateja kujilinda.

Mwisho, kuna shauku ya hisia. Hapa ndipo panaingia sekta ya burudani ya muziki, mpira, nk. Kwa mfano, wamiliki wengi wa magazeti wamegundua kwamba kuandika juu ya habari nyingine ambazo hazihusu mpira, hawauzi magazeti yao. Siku hizi magazeti ya michezo yapo mengi na mengine yanazidi kuzaliwa kila kukicha. Huwezi kukatiza mtaa mmoja hujawasikia watu wakibishana kuhusu Yanga na Simba. Wamiliki wa magazeti wamejizatiti kuanzisha magazeti ya michezo ili kukidhi kiu ya watu. Kuna gazeti moja la michezo lilikuwa linatoka kila Jumamosi na Alhamisi lakini walipoona soko ni kubwa wakaanza kutoa gazeti kila siku na linauzika hadi nakala ya mwisho.

Aidha, timu moja ya mpira iliamua kubuni tamasha la mpira. Baadaye, timu nyingine nayo iliiga na kunzisha tamasha kama hilo. Hatimaye timu ya tatu nayo ikafuata. Kwa sasa nchini Tanzania kuna jumla ya timu 3 zinazofanya matamasha ya namna hiyo. Waligundua kuna soko ndipo wakaamua kuanzisha matamasha, vinginevyo yasingeshamiri na kuendelezwa kwa kipindi chote hiki.

Hitimisho
Kama nilivyosema awali, biashara ni sayansi, sio sanaa. Ili uweze kufanikiwa lazima ukidhi matakwa ya wateja na katika kukidhi matakwa hayo lazima ufuate kanuni ambazo kama ukizikosea biashara yako haiwezi kufanikiwa kamwe. Jambo la kwanza na la muhimu kabisa ni kuziba pengo la bidhaa na huduma. Hii ni chachu ya kuwatunza wateja waliopo na kuwavutia wateja wapya.

Nawasilisha.​
 
Well noted
 
Back
Top Bottom