Namna ulivyoyaanza maisha na mkeo unakuja pata mali (kufanikiwa) unaongeza mke wa pili hii si sawa

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Feb 9, 2019
859
1,012
Hii ni kwa waislamu,

Mlioruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja.

Yaani unayaanza maisha ukiwa hauna lolote vile unapambana na msichana wa watu (mkeo), vile anakupa njia wapi pa kuanzia wapi pa kumalizia, vile unaanguka anakusaidia kusimama tena. Mdada wa watu (mke mkubwa) mara achome vitumbua mara uende nae shamba.

Life linaanza kuwa sawa mara kwa genge mara ka pikipiki mara mashamba makubwa life hilooo mara nyumba mzuri, life limeongoza na kitambi juu.

DINI yako inakuja kukushawishi uongeze MKE wa pili.

Sawa ushapata mke wa pili.
Bado DINI YAKO inakushawishi eti ugawe haki sawa kwa sawa. Yaani huku nyama na kule nyama.

Kwa bi mdogo siku 2 na kule kwa ukikoanza naye maisha siku 2.

Ndugu yangu wacha nikushauri kitu.

Hiyo unayoifanya ni dhurma.
Haumtendei haki mdada wa watu.

Kumbuka maisha ya shida mlioyapitia, kumbuka ulivyokuwa unamshindisha na njaa mdada wa watu.

Kama wewe ni wakufata sana misingi ya dini si ungeongeza mke kipindi kile unavaa suruali imetoboka kati?

Si ungeongeza mke kipindi kile unakaanga samaki pale sokoni.

Si ungeongeza mke kipindi kile unacharanga kuni na kuuza kwa mzee Kimaro.

HIYO NI DHURMA.
Kumbuka ulipotoka.
 
Sheria ya kuongeza mke au kuwa na mke zaidi ya mmoja inasemaje? Au utaratibu ukoje?
 
Siulijua sheria ya ndoa ya dini yako tangu mapema? Sa unalalama nini? Ungetafuta wa dini tofauti. Na bado mwenzio wakifa pepo I anapewa bikra 72, we upo tu unakodoa..... 😁 😁.. Tukiwambieni njoo kwa Yesu mantuita kafiri... Sa sijui anedaiwa kufanya dhurma nae sio kafiri.... Pole we Dada.. Tulia tu udhulumiwe😁😁
 
Rudi shule kwanza kajifunze kuandika kwa usahihi. Dhurma ndio nini?
Halafu, turudi kwenye mada, unaposaini cheti cha ndoa kimeandikwa NDOA HII IMEFUNGWA KWA MISINGI/MADHEHEBU YA KIISLAM.
Kwamba wafunga ndoa wanafahamu mume anaweza kufunga ndoa nyingine wakati wowote ule.
Uzuri wa ndoa si jambo la kulazimishana.

Abeid A Karume aliwahi kusema, Muungano (wa Tanganyika na Zanzibar) ni kama koti, likikubana unalivua tu. Nawe ndoa ikikubana ivue.

KATAA NDOA, NDOA NI UTAPELI
 
Mke wangu aliniambia kama nataka kuongeza mke wa pili basi Mali zote tulizozonazo tuwaandikishe watoto wetu, halafu nikaanze moja na huyo mke mwingine.

Mfano tuna nyumba mbili lkn anasema nikioa mke mwingine asiende kukaa kwenye nyumba zetu bali nikampangie. Anasema kama yeye alivyoanza sifuri na mimi basi bi mdogo nae pia aanze hivyo hivyo.

Hii imekaaje jamani, ni kweli ukioa mke mwingine wakati mambo yameshakua safi inakua ni dhuluma kwa mke mkubwa?
 
Usiwasahau na wale wanawake wanaokimbia waume zao Kwa kudai talaka kisa wamefilisika ilhali wakati wa neema ni wao ndio walikuwa mstari wa Mbele kula Mali.
 
Mke wangu mimi kazi yake kubwa ni kula, kudinywa, kulea na kulala.

Kupika na kazi za ndani yupo mdada wa kazi.

Mke hajui naingiza kiasi gani kwa mwezi, anajua kuomba pesa ya kununua mahitaji yake na pesa ya kupeleka kwao.

Nikioa mke wa pili, nitakuwa nimefanya dhulma..?
 
Back
Top Bottom