Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,892
KUWA NA MZAZI WA NAMNA HII NI ZAIDI YA KERO. "NIMEKUBALI LAANA YA BABA"

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kuna kijana mmoja tumekuwa tuliwasiliana Kwa takribani mwezi sasa. Amekuwa akiniomba msaada wa ushauri wa namna ya kukabiliana na yale yanayomkabili ambayo kwake anayaona kama ni matatizo na kero inayomnyima furaha ya kuishi mpaka kufikia mawazo ya kutaka kujiua.

Anasema, Yeye alilelewa na Mama pekee katika mazingira ya ufukara uliokithiri. Biashara ya kuuza pombe za kienyeji pale nyumbani ndio iliyomkuza, amekua akiona na kusikia matusi kutoka kwa Wateja ambao sisi waja na walimwengu tunawaita Walevi wa mataputapu., Ambao wakishalewa basi huanzisha matusi, fujo na Karaha pale nyumbani.

Kusikia au kuona mama yake akitukanwa au akifanyiwa vitendo vinavyofanana na matusi kwake alihitimu kuizoea baada ya miaka mingi ya kujitahidi kukabiliana na hisia kali za maumivu.

Uliwahi kuona au kusikia Mama yako mzazi akitukanwa. Na ili apate pesa ni lazima atukanwe na wateja wake ambao wapo chakari? Kama uliwahi basi Taikon nakupa pole kama nilivyompa huyu Kijana. Na kama haujawahi basi mshukuru Mungu.

Pombe nyumbani, matusi ndio muziki, nyumba ndio kilabu cha Pombe. Kelele siku zote. Harufu za mikojo ya pombe ndio marashi na manukato yenu.
Hapana nimesahau, sio wewe ni huyu Kijana.

Hakuna ambaye hakumdharau kijana huyu. Kila alipopita walimdhihaki na kumkejeli. Kumsimanga na kumnanga. Sio barabarani sio shuleni kote alikutwa na kejeli. Waalimu ambao wangemfundisha walikuwa wakimfundisha chuki kwani walikuwa wakimchukia kwa maneno na vitendo.
Huko makanisani kila alipojaribu kwenda alisikia mahubiri yanayotukana na kukejeli Pombe. Serikali nayo kupitia polisi na migambô alishazoea purukushani zao wakija kumkamata Mama yàke.

Anasema, hakuwahi kuheshimiwa hata siku moja. Tangu yupo tumboni alidharauliwa tuu. Nikamuuliza ulijuaje kuwa ulidharauliwa ulipokuwa tumboni mwake mama yako. Akasema alipata uzoefu huo kupitia Uzoefu wa kuona Mimba ya Mdogo wake wa mwisho. Anasema aliona jinsi Watu na jamii ilivyomsimanga na kumsema vibaya mama yake. Hiyo ilitosha kuelewa kuwa hata yeye ilikuwa hivyohivyo. Kama hiyo haitoshi akasema, maisha ya utoto wakati anajitambua yanajieleza zaidi.

Hakuna aliyemhakikishia, mthamini isipokuwa mama yake ambaye hata naye kazi yake ilimfanya amjali kwa namna ya kutisha, kwa kumtukana matusi ya nguoni.

Hapo nikamuuliza, Baba yake je?
Akasema baba yake kwa mara ya kwanza alipata kusikia jina lake alipoandikishwa shule ya msingi, hapo ndipo akakua jina na Baba yake ambalo mara kadhaa alikuwa akijiuliza pekeake pasipo kumshirikisha mtu. Anasema alifurahi kujua jina la baba yake. Kuna wakati akiwa pekeake katika tafakuri alikuwa akijaribu kufikiri taswira ya Baba yake mzazi.
Anafananaje?
Ni mweusi au mfupi?
Mrefu au Mweupe?
Yupo wapi na anafanya nini?

Kijana akakua, na bahati nzuri anadai alifika mpaka kidato cha nne, kiugumuugumu, huku kwenye kitabu cha mahudhurio kikionyesha Absent ni robo tatu huku Present ikiwa robo tuu. Akafeli akiwa kapata Sifuri.
Anasema alifurahi kumaliza shule kwa sababu alijua ndio mwisho wa manyanyaso.

Akiwa kidato cha tatu kwa mara ya kwanza akakutana na Baba yake, ni baada ya Mama yake kumpeleka. Mtaa wa sita huko.
Mbele yake alisimama mwanaume mwenye nuru, mtanashati aliyevaa kimaridadi, sura wanafanana ila mwanaume huyo kidogo alikuwa mweusi. Wakati kijana na mweupe akiwa amechukua rangi ya mama yake. Kwani mama yake ni mweupe ingawaje weupe umechakazwa na pombe.

Alifurahi kumuona Baba yake, tena akiwa kapendeza. Tumaini la maisha kubadilika lilikuwa mbioni kuufungua mlango wa moyo wake. Naye asingesita kufungua mlango huo ambao alikuwa akiimba dua tangu na tangu.

Kumbe yule mwanaume hakuwa anaishi pale kijijini. Alitoka mjini huko. Lakini katika hali ya ajabu. Yule mwanaume akawa anamzingua Mamaake na huyu Kijana, wakatukanana hapo, huku Mwanaume yule akimuita yule Mwanamke malaya na matusi mengine ya nguoni.

Kijana aliumia. Anasema, ingawaje mama ndiye alienda kwa Shari kama ilivyo kawaida yake lakini Aliamini Baba yake angeweza kulitatua jambo hilo katika njia salama. Aliamini baba yake ambaye ndio siku ya kwanza anamuona asingeshindwa kukosa hekima na busara za kukabiliana na mzozo ule.

Lakini moyo wake ulikatiliwa mbali. Uligomezwa na kugongelewa misumari. Yule mwanaume alimtukana na kumdhalilisha mama yake. Alimkaripia na nusura ampige.
Anasema;, Akanifukuza mimi na mama yangu"

Hapo akaacha kunisimulia akawa anavuta makamasi mepesi yaliyokuwa tayari yanamtoka huku machozi yakichirizika mashavuni. Alikuwa akilia.
Hisia zangu alizokamatwa ingawaje nilijikaza asinione nimekaribia kushindwa kuzihimili kama yeye.

" Ondoa huyu Mbwa umpeleke kwa Mbwakoko waliokuzalisha"
Akasema kisha kwikwi ikambana kwa nguvu. Sasa alikuwa anapoteza uwezo wake wa kujihimili. Nikamkamata. Alikuwa mwepesi sana huku kwikwi ikiwa na nguvu dhidi yake na mimi niliyekuwa kama mkanizi wa vita yake na hisia zake.

"Baba yangu alijiita Mbwa. Mimi nilimkosea nini? Mimi kosa langu ni nini?" Hapo akanambia huku akijitoa kwangu macho yakiwa tepetepe yamelowana kwa machozi. Akajifuta machozi kisha akanikazia macho yake kwa nguvu na kunitazama, "Taikon niambie kosa langu"

Mimi sikuweza kumjibu. Nikawa namtazama.

Alinitukana mimi na kufukuza pale nyumbani mbele za Watu pasipo aibu yoyote. Hiyo ningevumilia. Lakini kumtukana mama yangu, kumkashifu mbele yangu, na kumsukumasukuma mbele ya macho yangu mama anadondoka chini na vile mama yangu alivyokuwa mwembamba kutokana na ugumu wa maisha. Unafikiri ningejihisi vipi? Ninge-feel vipi wewe Taikon? Wewe si mtaalamu, ningejisikiaje.

Amemtukana mtu aliyekuwa faraja kwangu. Aliyekuwa mlinzi wangu, aliyekuwa mtetezi wangu. Aliyekuwa kila lilojema kwangu. Tena aliyefanya hivyo ni Baba yangu wa kunizaa kabisa.

Au alikuwa akimuonea aibu mama yangu jinsi alivyokuwa anaonekana? Alikuwa hapendezi usoni si ndio? Midomo yake ilikuwa imebabuka kwa pombe si ndio? Nguo alizovaa zilikuwa matambara si ndio eeh? Alikuwa sio wa hadhi yake si ndio ehe? Alikuwa mama Muuza mataputapu si ndio ehe?
Nakuuliza Taikon, si ndio eeh?

Nisikie, huyo ndiye aliyekuwa Mama yangu, kipenzi changu. Hata kama mdomo wake ulikuwa umeharibika na kubabuka kwa pombe na sigara lakini midomo hiyo ndio iliyokuwa ikiniita "mwanangu" ndio hiyohiyo iliyokuwa inaniambia "nakupenda"

Wewe mwenye midomo mizuri na nguo nzuri na makazi mazuri vyote hivyo vilifanya nini kwangu? Nambie vilinisaidia nini mimi?

Huyo mama muuza pombe ndiye aliyenilea, pombe zake zilinikuza na kunisomesha angalau mpaka kidato cha nne. Wewe kazi yako hiyo huko mjini inamaana gani kwangu?

"Taikon! Taikon! Taikon!"
Nakusikiliza kijana endelea.

Nikamaliza kidato cha nne. Nikiwa nimemfuta Baba kwenye akili zangu.
Miaka ikaenda na wala sikutaka irudi. Sikutaka maisha ya kipindi kile yajirudie. Niliamini kusonga mbele kwa siku ndiko ahueni yangu. Niliamini huko mbeleni lipo tumaini. Ipo nuru. Nuru iko mbeleni. Na ili niipate nuru hiyo itanipasa kusonga mbele kama siku zifanyavyo. Bila kujali ugumu na urahisi nitakaokutana nao mbele nitasoma. Mbele ilipo Nuru ya ukombozi.

Nikaondoka pale mjini. Huyo mpaka mjini. Nikiwa nimemuacha mama yangu akiendelea na shughuli zake za pombe ingawaje siku hizi biashara imekwisha, haimpi pesa yoyote kutokana na sheria za serikali kushikiliwa kidete.

Piga kazi! Fanya Kazi! Chapa kazi!
Huku nikiimba, "Mama yangu midomo imebabuka sababu ya pombe na sigara, Muuza pombe na mataputapu wa huko bara, Mwili wake umekonda kauvalisha matambara" Baba yangu alimuita Malaya"

Hapo nikamsimamisha, nikamwambia aache kuimba. Alikuwa akiimba kama mlevi lakini hakuwa amekunywa.
Akaendelea,

Huo ndio ulikuwa wimbo wangu wa Maisha. Wimbo ambao ungenikumbusha wapi nilipotoka na nini kilichonileta Mjini kutafuta maisha.

Miaka ikaenda, nashindwa kusema Mungu ndiye kajaalia kwani maisha niliyoishi sikuamini kama Mungu angekuwepo na aruhusu maisha yetu kuwa vile. Pengine naye nilijikuta namchukia.

Lakini ile nuru niliyoanza kuifuata nilianza kuiona kwa mbali. Maisha yangu yalianza kuchukua mkondo mpya. Nikajenga nyumbani kwetu na kumbadilishia mama makazi yake. Pale nyumbani niliweka bomba la maji ambalo ndilo linamsaidia mama kujipatia kipato kwa kuuza maji yale.
Yale matambara ambayo yalikuwa nguo zake havai tena. Nimemnunulia nguo nzuri na ninahakikisha kila ambacho alitamani kukivaa basi anakivaa kwa wakati huu kulingana na umri wake.

Nami nimenunua gari. Ni IST. Ninaipenda sana. Ingawaje wapo waliosema ni kagari kadogo lakini kwangu ni gari kubwa kwa sababu nilipotoka napajua.

Nimejenga pia kwenye mji niliopo. Ni kajumba kanakonitosha, nakakapenda, ngoja nitakutumia picha na video baada ya kuongea. Nikamjibu; Sawa.

Baba sijui nini alisahau kwangu. Nikashangaa siku moja namba mpya ikanipigia. Kupokea akaongea na kujitambulisha. Nikamuuliza anashida gani. Akaanza kunitolea maneno ya kero na Karaha.

Ati ananilaani. Na kunitolea maneno ya kipuuzi. Ati mzazi ni mzazi na baba ni Baba. Nikamwambia mimi Baba yangu ni Mbwakoko. Na yeye sio baba yangu. Nikirejelea maneno yake. Akasema ati nisiseme hivyo, alafu ati nisiingilie ugomvi wake na Mama.

Nikamjibu kuwa Wakati unaniona Mbwakoko na baba yangu umbwakoko niliingilia ugomvi wenu? Baba yangu anadai ati mama ndiye ananilisha sumu ilhali mimi mwenyewe ile siku kwa masikio yangu nilimsikia. Halafu mama hakuwahi hata siku moja kumtaja Baba yangu tukiwa wote(mimi na Mama).

Sasa Baba yeye kila siku ni kunitumia Watu wananisumbua, mara ndugu zake wanipigie simu. Mara wazee wa Kanisa.

Nimemuambia, yeye keshanipa Laana na mimi nipo tayari kwa hiyo laana. Asinitafute. Nimekubali laana ya Baba yangu. Sitaki anitafute. Nipo tayari kukabiliana na lolote kwenye Maisha yangu lakini sitaki Awe karibu yangu. Sitaki kumuona na sitaki anione.

Kuhusu hayo mambo ya Mungu nimewaambia wazee wa kanisa na wachungaji waniache. Nitajibu maswali mbele za Mungu. Nipo tayari.

Taikon ninachokitaka kwako ni kuandika simulizi inayonihusu Mimi. Kisha uniambie ninawezaje kumzuia Baba asinisumbue kisheria.

Kijana akamaliza.
Nikafungua zile picha na video alizonitumia, nikashangaa kuona katika moja ya kuta zikiwa zimeandikwa ule wimbo;
"Mama yangu midomo imebabuka sababu ya pombe na sigara,
Muuza pombe na mataputapu wa huko bara,
Mwili wake umekonda kauvalisha matambara"
Baba yangu alimuita Malaya"

Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Nami nimewasilisha kama wadau wangu wapendavyo.

Wanasheria watusaidie kumsaidia huyu kijana kuwa ni vipi apate msaada wa kumzuia Baba yake asimsumbue sumbue. Kuhusu kuandika simulizi yake nitaanza kuiandika Februari 2024 panapo majaliwa. Title amesema iwe; NIMEKUBALI LAANA YA BABA"

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kuna aina ya maisha niliyo yapitia hua sipendi kuyasimulia.
Lakini nilimuomba Mungu asimame na mimi ili nisamehe na mwisho niliipata amani.
Yale mapito hakika yalinijenga na leo hii nimeimarika sana, pia nimekua baba bora kwa kiwango changu hasa kwa watoto wangu.
Nimejitahidi kufanya kila niwezalo ili siku moja watoto wangu wasije wakapitia na kujeruhiwa kama nilivyo umizwa mimi.
 
Wanaume tunafeli mengi.
Hapa mwenzetu hajaomba ushauri wa kumsamehe baba yake,tujadili aliloomba asaidiwe.
Baba ujana wako utumie na mbwa koko halafu utegemee watoto ambao ukuwalea waje wakusaidie kwa vitisho kuwa wasipofanya hivyo utawalaani?
Please baba wa aina hiyo kafie mbele mbwa wenzako
 
unanifurahishaga unavyomalizia hapo mwisho
"Taikon wa fasihi" "Kwa sasa ......"
 
Wanaume tunafeli mengi.
Hapa mwenzetu hajaomba ushauri wa kumsamehe baba yake,tujadili aliloomba asaidiwe.
Baba ujana wako utumie na mbwa koko halafu utegemee watoto ambao ukuwalea waje wakusaidie kwa vitisho kuwa wasipofanya hivyo utawalaani?
Please baba wa aina hiyo kafie mbele mbwa wenzako

😀😀
Hasira Mkuu
 
Back
Top Bottom