Maajabu ya mji wa Njombe: Kitimoto kinauzwa bei rahisi kuliko nyama ya ng'ombe

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,694
6,396
Ni hali ya hewa ya ubaridi ndiyo imepelekea hiyo mboga kupatikana kwa wingi Njombe Mjini?

Nimeshangaa kukuta mabucha pamoja na "vijiwe" vya kuchomea kitimoto zaidi ya moja sehemu moja.

Wakati kilo moja ya nyama ya ng'ombe ikiuzwa sh 9,000/=, kitimoto inauzwa sh 6,000/= kwa kilo.

Kwangu, hayo ni maajabu kwa sababu katika mikoa mingi niliyofika, bei ya kitimoto ama ni ghali kuliko nyama ya ng'ombe, au inalingana nayo.
 
Njombe mdudu anafugwa kwa wingi sanaaa kuliko hata ng'ombe, hio ndio sababu, kila nyumba vijijin ina mdudu, ila ni rahisi Kwenda kwenye kijiji njombe wenye ng'ombe ni watu watano tu
 
Njombe Tena Kwa Style Mpya Wakati Muafaka, Watu Wale Washibe Watembee Kifua Mbele
 
Ni hali ya hewa ya ubaridi ndiyo imepelekea hiyo mboga kupatikana kwa wingi Njombe Mjini?

Nimeshangaa kukuta mabucha pamoja na "vijiwe" vya kuchomea kitimoto zaidi ya moja sehemu moja.

Wakati kilo moja ya nyama ya ng'ombe ikiuzwa sh 9,000/=, kitimoto inauzwa sh 6,000/= kwa kilo.

Kwangu, hayo ni maajabu kwa sababu katika mikoa mingi niliyofika, bei ya kitimoto ama ni ghali kuliko nyama ya ng'ombe, au inalingana nayo.
Ukanda huo kuna ndezi wakubwa size ya mbuzi
 
Mimi naona Kuna factor kama mbili zinachangia
1. Ufugaji wa nguruwe ni mkubwa huko. Kwa asilimia kubwa utakuta Kila kaya inafuga huyo mnyama
2. Mkoa kuwa mbali na Dar pia nayo ni sababu. Mikoa iliyopo karibu na Dar inafikiwa na wanunuzi wa kitimoto kutoka Dar kirahisi ukilinganisha na huko Njombe.
 
Back
Top Bottom