Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Hashimu Ally Phillemon, mkazi wa Babati Mjini anaeleza kwamba alikamatwa eneo lake la kazi, Paleii Lake View Garden, mali ya mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba na kupigwa, kujeruhiwa na kuwekewa chupa katika maeneo ya haja kubwa.

Hashimu Ally anadai, Pauline Gekul alitoa bastola, akamueleza achague kukalia chupa mwenyewe au apigwe risasi na mwili wake wakautupe katika Ziwa Babati. Alipogoma, wakampiga sana, wakamuingizia chupa sehemu ya haja kubwa.

Hashimu Ally anasema alituhumiwa na bosi wake (Pauline Gekul) kutumwa kuweka sumu ili kumuua Pauline Gekul, tuhuma ambazo hazijathibitishwa popote hata na jeshi la polisi, akasulubiwa sana kisha kukabidhiwa polisi Babati na kumpiga kila siku asubuhi na jioni, kwa siku nne.

Hashimu Ally anasema alikana tuhuma zote hizo akiwa kituo cha polisi Babati Mjini na hata chini ya mikono ya mateso ya Pauline Gekul. Baada ya kupigwa kwa siku nne mfululizo akiwa polisi Babati, alidhaminiwa na baba yake mzazi lakini baadaye akaitwa ofisi za Manyara ili kutoa maelezo.

Hata hivyo, Mbunge Pauline kupitia Katibu wake alikanusha taarifa hiyo katika ujumbe uliowekwa kwenye mitandao ya kijamii ukimtuhumu Hashimu kufanya udanganyifu na kushirikiana na washindani wa Pauline wa kibiashara kumfanyia ushirikina na baadaye ujumbe huo kufutwa kwa maelezo kuwa suala hilo liko mikononi mwa Polisi.

Saa chache baada ya tuhuma hizi kusambaa na kupigiwa kelele na wadau mbalimbali ikiwemo wa JamiiForums, Rais Samia Suluhu, jioni ya tarehe 25 Novemba 2023, ametengua uteuzi wa Naibu Waziri huyo wa Wizara ya Katiba na Sheria.

====

Zaidi soma >>

Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji

Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

CCM Manyara yakutana kumjadili Pauline Gekul, kutoa tamko Novemba 27, 2023


Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

Mbunge Pauline Gekul akamatwa na Jeshi la Polisi akijaribu kutoroka nchini kuelekea nchini Kenya

Mbunge Pauline Gekul ahojiwa Polisi na kupewa dhamana, karudi nyumbani kwake

Peter Madeleka kusikiliza kesi ya Gekul mahakama ya Wilaya kwa tuhuma alizonazo dhidi ya Hamis

Mbunge Pauline Gekul atakiwa kufika Mahakamani Disemba 27, 2023 kujibu tuhuma dhidi yake

Nani anamlinda Gekul? DPP asema hana mpango wa kuendelea na kesi

Ya Gekul hayajaisha, Wakili Madeleka kukata rufaa

DPP: Hakukuwa na nia ya kufungua kesi ya Jinai dhidi ya Pauline Gekul

Rufaa ya Pauline Gekul (Mbunge Babati Mjini) yapigwa kalenda

Shauri dhidi ya Mbunge Gekul lasikilizwa Mahakamani, Wakili Madeleka asema DPP hakuwa na Mamlaka ya kufuta kesi

Rufani dhini ya Mbunge Pauline Gekul yatupiliwa mbali, wapanga kufungua kesi ya madai kwa wote waliomchafua
 
Mara nyingi watu wanaofanyiwa unyama wa aina hii unakuta anampanda mtu kichwani kwa kumletea mambo ya ovyo. Hasira zake ndio anamrudishia kwa kutuma watu wafanye unyama wa aina hiyo.

Binafsi I am capable of doing worst if opportunities arises kwa watu kama watatu tu hivi; ipo siku wataingia anga zangu.
 
Mara nyingi watu wanaofanyiwa unyama wa aina hii unakuta anampanda mtu kichwani kwa kumletea mambo ya ovyo. Hasira zake zake ndio anamrudishia kwa kutuma watu wafanye unyama wa aina hiyo.

Binafsi I am capable of doing worst if opportunities arises kwa watu kama watatu tu hivi; ipo siku wataingia anga zangu.
Unapenda sana kuwa opposite wewe
Sasa kitendo alichifanya hyo mb ni
Sawa.....
Kuwafanyia madogo kama hao kuwapiga na kuwaingiza chupa mtkoni ni unyama

Ova
 
Sasa mimi nawauliza?
Mmemuamini vipi huyu kijana huku amefichwa sura?
Chanzo cha taarifa hii ni kipi?
Au ndio team Mbowe inavyowasa wabaya wao?
Ukitazama network inayohusisha huo uhalifu aliofanyiwa huyo kijana, huwezi kupata mashaka juu ya kile alichofanyiwa, na yule aliyemfanyia, kwasababu hao wahusika wameshathibitika miaka mingi mateso kwa watanzania wenzao, ndio tabia zao

- Mbunge / waziri / mtuhumiwa - CCM.

- Polisi - CCM.

Hapo mtuhani unakuja CCM amkamate CCM mwenzie!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom