Niliwahi kuwa na g/friend kipindi cha nyuma alikuwa na tatizo kama lako, akikasirika anaweza akakuua kama hauko makini na ilikuwa anakwambia kabisa kwamba natamani nikuue ili niwe na amani, nilikuja kufaulu kuondoa tatizo lake kwa kumweka karibu nami hasa pale anapokuwa kacharuka. Mwanzoni ilikuwa tabu kidogo vile nililazimika kutumia nguvu nyingi sana kumkamata na kumbembeleza kwa maneno ya kufanya hasira yake ishuke, nilikuja kugundua anapokuwa hasira zake zinamkamata kichwani~ basi ikawa nikimkamata nampet pet kichwa chake na maneno ya kumfariji haichukui muda analala usingizi. Nilifanya hivyo mara kadhaa pasi na kuchoka na Mungu ni muweza wa yote tatizo lake likapungua saana na baadae kwisha. Sasa hivi akikasirika anapuuza tu kisha anasamehe maisha yanasonga. Pole sana miss. chaga