Makonde plateu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,466
- 3,516
Wakuukwanza niseme nakushukuru sana kwa JamiiForums haswa inaleta exposure watu tunapona kimya kimya kwa maana siku niliyojiunga sikulala ni kama nilikesha natafuta hizi parts nasoma mpaka nikajikuta najiahidi kujileta kwako
Kitu niligundua tangu nikufatilie ni uko very so down to earth not judgemental at all unajitahidi sana kuufanya ukurasa wako kuwa sehemu salama ya mtu kuzungumza bila kuwa attacked kwa matusi, na wewe unajua uongee nini bila kuacha kovu, sijui kama unafaidika na haya unayofanya ila unafanya,
Kuna sehemu unaongelea vitu muhimu sana kwa njia nyepesi ili tu mtu aelewe hadi nahisi nje ya humu ni wale watu wenye upendo sanaaa watu wako wa karibu ndio wanaweza kututhibitishia hili
Sijawahi kukaa chini nikamsimulia mtu maisha yangu na hata kiasili mi si muongeaji sana lakini kwako niulize chochote nitakwambia that is how umefanya nikuamini, na kama nilivyokwambia na mimi niko hapa kuelezea safari yangu
Nilizaliwa mwaka ** kiasili ni ila nimekulia mkoani **. Tangu napata ufahamu mpaka nabelehe nimelelewa umamani sikuwahi kumjua baba yangu mpaka nilipofikisha miaka 18.
Mama yetu alizaa watoto watatu na mimi ndiye mkubwa. Nilianza kulelewa kwa bibi mzaa mama. Wakati watu wengine wana drug addicts (Wanaotumia dawa za kulevya) ambao ni labda kaka, dada sijui binamu mimi drug addict alikuwa mama yangu mzazi kabisa. Yaani huyo dada yako anayetumia madawa azae mtoto, ndio mimi sasa
Hakuna kitu kinauma kama kupata ufahamu na kumuona mama yako stendi au kwenye vibaraza vya maduka akiwa kama kichaa.
Nimekuwa bullied sana shuleni sana sana sana, sikuwahi kufurahia shule sababu ya matani na matusi niliyokuwa napewa na wanafunzi wenzangu na baadhi ya walimu kwa sababu mama yangu alikuwa kama drug addict na kuna wakati alipita karibu na shule.
Laura mama yangu alikuwa ananijua kwa sababu kuna kipindi alifungiwa ndani hatukuruhusiwa kumsogolea lakini nilijitahidi kumsogelea kwa kujificha, she was my mom, sikuwa na mama mwingine ni huyo huyo kichaa nilihitaji anikumbatie nilitaka kuita mama nae aitike nilimpenda sana, alikuwa anakuja shule ananiulizia watu wanacheka anafukuzwa na kutishiwa kupigwa nami naambiwa nisilete vichaa shuleni kuna siku alipigwa na mlinzi wa shule maskini akaacha kuja
Alipofungiwa ndani hali yake ilikuwa mbaya kiasi aliachiwa akazurure tu mwisho wakaanza kusema amelogezewa kulala mtaani lakini nahisi mtaani alipata hizo dawa akifungiwa ndani alikuwa anapata arosto mpaka wanamhurumia, kama kuna mtu amewahi kuishi na drug addict anajua naongelea nini
Basi hayo ndo maisha nilioishi mwanzoni kabisa, pale kwa bibi palikuwa na wajukuu wengine nilipofika darasa la tano aliletwa mtoto ambaye mama alimzaa mtaani akapokonywa akaja kulelewa na bibi kwa mtindo huo nilipata ndugu zangu wawili nao kama mimi hawakuwajua baba zao
Nikamaliza Darasa la saba nilifaulu kwenda sekondari ambayo ilikuwa mbali kidogo na nyumbani, Bibi alikuwa anauza pombe ndio napata mahitaji na mimi namsaidia kuuza mahindi ya kuchemsha kwa kutembeza tukipata hela tunagawa za shule na mahitaji ndani,
Kiukweli watoto aliozaa bibi hawakuwa na msaada kwake alizaa watoto saba, kila mmoja alikwenda kutafuta maisha baadhi walileta wajukuu kuishi pale na wajukuu wawili wakaleta vitukuu kulikuwa na mjomba mlevi sana yeye alikuwa mtu wa kunywa na kupigana sana, mwaka **** mjomba aliishia jela kwa mauaji ya mtoto wa dada yake
Alimpiga sana kisa alimtuma dukani akapoteza hela alimpiga tukishuhudia na hakuna mtu alisogea coz mjomba alikuwa anaogopwa hata na bibi alishawahi kumshikia kisu huku tunaona, ila kipigo kile kilizidi coz mtoto wa mamdogo alimshitaki kwa bibi kuwa usiku anamfanyia mambo mabaya, kukawa na kuzozana baina yao yakaishia chumbani uko ndio baadae kumtuma akapoteza hela
Usiku tumelala mwenzangu akaanza kukoroma sana ikabidi tuamshane akaanza kukohoa damu kufika hospital amefariki ndio mara ya kwanza kujua kifo ni nini kwa mtu unayeishi naye kufariki
Ma mdogo kuja kukawa na kesi ndio ilipelekea mjomba kufungwa.
Hayo mambo yote yanatokea bibi naye akaanza kuumwa sana kipindi hicho sikujua mama alipo maana hata mtaani alitoweka sikumuona tena kwa kipindi kirefu, Wakati bibi anaumwa mdogo wangu wa mwisho naye alikuwa mgonjwa sana, huyu siku zote alikuwa mgonjwa sababu alikuwa na Sickle Cell kwa hio nyumba ikawa na watu wawili wagonjwa,
Baada ya msiba watu waliondoka pale, hakukubakia hata na ndoo ya mchele wala zile hela zilitolewa sikuziona, upande wa baba wa marehemu walikuja na vitu vingi sana, mamdogo alitoka mjini na watu wamemsindikiza walikuja na vitu vya kula. Msiba ulija watu wengi sana, na watu hao tena ndugu walichota vyakula wakaenda navyo makwao hela sijui ziliishia mikononi mwa nani lakini mwisho wa siku mimi na bibi tulibaki chumbani tumekaa kitandani hatuna chakula hatuna pesa, nakumbuka kuna ndugu nilimuomba pesa kidogo alinijibu baba zenu wako wapi watafuteni baba zenu
Hii iliuma sana sidhani kama kuna mtoto huwa hatamani kumjua baba yake au kusaidiwa na baba yake hata aweje au maskini kiasi gani mimi huyo baba hata sikuwa namjua wakati huo
Nimetembeza sana mahindi, nimebeba mizigo midogo midogo, nimeuza sana maji ili nipate hela ya chakula na matibabu ya bibi na mdogo wangu
Maisha yangu kimasomo yalikuwa ya hovyo sana siku zote wa mwishoni uko laura ningesoma saa ngapi, nikiwa form two sijui ilianzaje lakini ulianza utani wa kuitwa jina baya sana ****.
Naomba hili usiliweke kisa tu habari za mamangu zilianza tena kuwa mdomoni mwa watu, kipindi hicho mamangu alikuwa kama changudoa mitaa fulani mbali kidogo alikuwa amedhoofika sana, nilkwambia ilipita kipindi kirefu sijamuona kisha akarudi mitaa hiyo
Nakumbuka siku moja usiku wakati natoka stendi nilitembea mpaka mitaa hiyo ili japo nimuone, I missed her i loved her na nilikuwa najiuliza sana kama aliwahi ata kunikumbuka au kunifikiria, mimi sikuwahi kumsahau, baadae ikaanza kuwa mazoea natembea mpaka huko nakaa sehemu namuangalia wakati mwingine nalia peke yangu kisha narudi nyumbani ambako watu wote wananitazama, Laura sikuwa hata na miaka 18
Siku moja nilienda baada ya kama wiki tatu kupita sikumuona sehemu ambayo alipenda kukaa, nilipata wasiwasi sana nikaenda mpaka eneo lile nikamuulizia, maneno magumu sana kusikia ni huyu *** ameanza kulalwa na vitoto sasa apate stimu,
Nilijiskia vibaya kujitambulisha kuwa mimi ni mtoto wake, Wakanionyesha sehemu ya nyuma ya nyumba kuna kijibanda amelala umo amejisaidia hajiwezi wametelekeza hapo, sikuweza kufanya chochote nilikufuru kwa mara ya kwanza nilikufuru kwanini nimepewa mama wa hivi katikati ya mamilioni ya wanawake wanaojitambua kwanini mimi nipewe kama huyu, lakini ndiyo picha ya mwisho ya mama kunitazama usoni na kutabasamu, coz alifariki wiki moja baadae
NitaENDELEA...