Nahitaji msaada wa haraka, hasira zitaniumbua mimi

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,821
48,976
Habari zenu wakuu,

Nina tatizo kubwa la hasira nimejaribu kupitia thread za wengine walioomba msaada naona sijafanikiwa. Sasa naomba nijielezee mimi wanasema mficha maradhi kifo kiamuumbua.. Naelekea kufa sasa sababu jana nimekasirika nimefanya mambo ya ajabu hapa nilipo mwili unauma kila mahali, natetemeka kama teja sababu ya kunywa pombe sana.

Kwanza nachukua muda kukasirika ila huwa nalipuka kama bomu, unaweza niudhi leo jambo kubwa ila kesho ukaniudhi kidogo nikakufanyia jambo kwanza huwezi elewa na mara nyingi hutegemei reaction ile kwa hiyo huwa nakuwa mshindi nakupa ngumi mateke kukutafuna nikibahatika ndani ya dakika mbili nakuta nimefanya tukio la kutosha..

Wakati mwingine nalia sana na ukiniongelesha nalia kwa sauti kama napigwa aibu kwa mtoto wa kike.

Nakunywa pombe sana ili nilewe nizime nilale lakini hili nina miezi 10 sijafanya japo jana nimelifanya tena na mimi nilishafanikiwa katika hili naona linanirudia tena (japo akili yangu na nafsi yangu inaniambia bora kurudia kunywa pombe).

Naombeni msaada nifanye nini napokasirika?

NB: Nikikasirika huwa nashindwa kuongea na ukiona umeniboa naongea jua sijakasirika ila nikaa kimya kaa mbali na mimi... Mpaka nawaza au bado na utoto utoto japo ni mkubwa!

Asanteni..
===========

MADA HII IKIWA NA MAONI YA WANAJF IMESOMWA PIA KWENYE KIPINDI CHA JAMII LEO. TAZAMA VIDEO;
 
habari zenu wakuu.

ninatatizo kubwa la hasira nimejaribu kupitia thread za wengine walioomba msaada naona sijafanikiwa .. sasa naomba nijielezee mimi wanasema mficha maradhi kifo kiamuumbua.. naelekea kufa sasa sababu jana nimekasirika nimefanya mambo ya ajabu hapa nilipo mwili unauma kila mahali natetemeka kama teja sababu ya kunywa pombe sana ..

kwanza nachukua muda kukasirika ila huwa nalipuka kama bomu, unaweza niudhi leo jambo kubwa ila kesho ukaniudhi kidogo nikakufanyia jambo kwanza huwezi elewa na mara nyingi hutegemei reaction ile kwa hiyo huwa nakuwa mshindi nakupa ngumi mateke kukutafuna nikibahatika ndani ya dakika mbili nakuta nimefanya tukio lakutosha..

wakati mwingine nalia sana na ukiniongelesha nalia kwa sauti kama napigwa aibu kwa mtoto wa kike.

nakunywa pombe sana ili niliwe nizime nilale lakini hili nina miezi 10 sijafanya japo jana nimelifanya tena na mimi nilishafanikiwa katika hili naona linanirudia tena...
naombeni msaada nifanye nini napo kasirika ..
NB: nikikasirika huwa nashindwa kuongea na ukiona umeniboa naongea jua sijakasirika ila nikaa kimya kaa mbali na mimi... mpaka nawaza au bado na utoto utoto japo ni mkubwa.

asanteni


Utakuwa na ugonjwa wa ukichaa au kwa jina la Kizungu wanaita Bordeline Personality Disorder (BPD) nakushauri kama upo Bongo uende kwa Kitila Mkumbo yeye ana PhD ya psychology labda atakusaidia kidogo lkn ni ngumu sana kupata tiba yake hapa Bongo kwani hatuna hawa Wataalamu!

Wanasema hii inatokana na madhara ambayo uliyapata wkt ukiwa mtoto, labda ulibakwa au kuteswa kwa ujumla ulikosa mapenzi utotoni ambapo mtoto wa kawaida hupata ktk kwa Wazazi au Walezi vile vile kuna kurithi wengine hurithi huo ukichaa ulio nao hivyo angalia kwenye familia yako kama mna asili ya ukichaa basi hapo na wewe utakuwa umerithi na hapo hakuna kitu utafanya, ningekushauri usianzishe mahusiano ya kimapenzi ili kutokuwadhuru wengine, nilishwahi kuwa na Demu mwenye huo ukichaa, hivyo najua ninachokiongelea!
 
Utakuwa na ugonjwa wa ukichaa au kwa jina la Kizungu wanaita Bordeline Personality Disorder (BPD) nakushauri kama upo Bongo uende kwa Kitila Mkumbo yeye ana PhD ya psychology labda atakusaidia kidogo lkn ni ngumu sana kupata tiba yake hapa Bongo kwani hatuna hawa Wataalamu!
Nilishwahi kuwa na demu mwenye huo ukichaa, hivyo najua ninachokiongelea!

Wanasema hii inatokana na madhara ambayo uliyapata wkt ukiwa mtoto, labda ulibakwa au kuteswa kwa ujumla ulikosa mapenzi utotoni ambapo mtoto wa kawaida hupata ktk kwa Wazazi au Walezi vile vile kuna kurihti wengine hurithi huo ukichaa ulio nao hivyo angalia kwenye familia yako kama mna asili ya ukichaa basi hapo na wewe utakuwa umerithi na hapo hakuna kitu utafanya, ningekushauri usianzishe mahusiano ya kimapenzi ili kutokuwadhuru wengine!
hapo naweza kuelewa sasa nifanyaje ?
 
hapo naweza kuelewa sasa nifanyaje ?


Inategemea kwa kawaida hauna Tiba hasa inapokuwa kama umerithi kwa maana ni genetic yaani iko kwenye genetic code yako, hivyo unaweza tu kuishi nao, ndiyo maana nakushauri ujichunguze kama ni kweli una hiyo basi usianzishe mahusiano (kimapenzi) na mtu, na jaribu tu kukubali hali halisi na kuishi nayo!
 
Pole sana!

Hilo tatizo lilianza lini?

Au ulikuwa nalo tangia utotoni?

Kama limeanza ukubwani kuna kitu kinapelekea uwe hivyo kama kunyanyaswa kihisia.

Pia kutokujihusisha katika kufanya tendo la ndoa inaweza kupelekea mtu kuwa na vihasira uchwara vya hapa na pale.

Tendo la ndoa huondoa hasira kama hauamini mtafute umpendaye uone siku mbili utarudisha marejesho hapa.
 
toa basi kaushauri kidogo kabla sijakutafuta naomba
Kwanza una stress, unahitaji kuwa na mtu karibu sana, aonyeshe mapenzi na ukaribu hata usipokuwa nae awe karibu ki mawasiliano, mengine mpaka tukionana lakini ulienae ameshindwa kucover hiyo nafasi.
 
Pole mumy, kila mtu ana njia Yake ya kuhandle situations (hasira, stress, depression etc)... Ila hatua ya kwanza ya kuhandle situation ni kujua point ya reaction yako... uzuri wewe unajijua ukikasirika unafanya vitu gani...sasa ni vema ukajiepusha na mazingira ya kukutia hasira though wakati mwingine Huwezi kuepuka inatokea tuu bila kutarajia... Pole
 
Back
Top Bottom