Nahitaji msaada wa haraka, hasira zitaniumbua mimi

Nahitaji msaada wa haraka, hasira zitaniumbua mimi

Mdogo wangu Manka...

Mwenye nguvu sio yule anayepigana na wenzake akashinda,bali ni yule anayezishinda hasira zake pindi akikasirika....

Azimia kwanza kuacha pombe,kama ukishindwa basi punguza.
Mimi jambo likiniudhi huwa najiambia mwenyewe..."Usikasirike"halafu natabasamu.

Mimi pia nina hasira sana,ila sijawahi kuiruhusu ikaushinda utashi wangu mpaka nikafanya kituko.

Kulitambua tatizo ni chanzo cha kupata ufumbuzi,jitahidi sana kuzishinda hasira zako...

Nakupenda miss chagga .
Asante kaka . Nakupenda pia
 
Aisee, mnatakiwa mfanyie kazi anger management. Siku huzi kuna wataalamu wa kila fani. Pale MNH kuna wataalamu wazuri sana wa saikolojia na afya ya akili. Jaribuni kiwatembelea, wao wana njia nyingi za kufahamu shida iko wapi na jinsi ya kuwasaidia.
Dah...my ex kanitisha sana...
 
Hapana, ulabu cjafanikiwa kutumia bali kichapo wengi wamechezea, nilinusurika kula risasi baada ya kutembeza kichapo kwa wenzangu na kazi nkapoteza, sikuishia hapo nilizingua police station ya wilaya flan kisa mmoja kaniudhi nako nilipona kula mvua za kutosha...kwa ufupi hasira zimehatarisha maisha yangu japo tukiongea huwezi amin kama ninaweza kukasirika..
Hii kitu mbaya sana Elli79
Dear...mbona nakuogopa ghafla??

Sasa si utanichakaza sura jamani?
 
habari zenu wakuu.

ninatatizo kubwa la hasira nimejaribu kupitia thread za wengine walioomba msaada naona sijafanikiwa .. sasa naomba nijielezee mimi wanasema mficha maradhi kifo kiamuumbua.. naelekea kufa sasa sababu jana nimekasirika nimefanya mambo ya ajabu hapa nilipo mwili unauma kila mahali, natetemeka kama teja sababu ya kunywa pombe sana ..

kwanza nachukua muda kukasirika ila huwa nalipuka kama bomu, unaweza niudhi leo jambo kubwa ila kesho ukaniudhi kidogo nikakufanyia jambo kwanza huwezi elewa na mara nyingi hutegemei reaction ile kwa hiyo huwa nakuwa mshindi nakupa ngumi mateke kukutafuna nikibahatika ndani ya dakika mbili nakuta nimefanya tukio lakutosha..

wakati mwingine nalia sana na ukiniongelesha nalia kwa sauti kama napigwa aibu kwa mtoto wa kike.

nakunywa pombe sana ili nilewe nizime nilale lakini hili nina miezi 10 sijafanya japo jana nimelifanya tena na mimi nilishafanikiwa katika hili naona linanirudia tena...(japo akili yangu na nafsi yangu inaniambia bora kurudia kunywa pombe )
naombeni msaada nifanye nini napo kasirika ..
NB: nikikasirika huwa nashindwa kuongea na ukiona umeniboa naongea jua sijakasirika ila nikaa kimya kaa mbali na mimi... mpaka nawaza au bado na utoto utoto japo ni mkubwa.

asanteni
ITAKUWA NI STRESS TU,KWANI UMEOLEWA? ILI TUANZE TIBA SASA
 
toa basi kaushauri kidogo kabla sijakutafuta naomba
Una matatizo ya kisaikolojia,kuna mambo ukiwa mdogo hayakwenda sawa,usiogope ni matatzo ya kawaida,wataalam wa tiba hii wapo wachache nchi yetu ila ungebahatika umpate jamaa mmoja hivi ni psychologist wa International School of Tanganyika,anawahudumia watoto wapale,yuko poa sana kuna dada mmoja alimuhudumia vizur sana,au nipe muda kuna kituo kimoja hivi ntawauliza maana wana deal na psychotherapy,kama unaweza kuuliza sehem yoyote wana deal na masuala ya Psycho therapy,
 
Chakwanza unapokasirika km ulikuwa umesisima basi kaa chini hasira zitapungua pombe sio suruhu ya hasira pole kwa hali hiyo dada
 
Mwanamke hata uwe na hasira vipi_ wewe endelea tu maake hauna madhara...hata ukirusha ngumi haina madhara....mm mwanamke hata akinichoma na kisu huwa siumii..
Ushauri wangu...wewe endelea tu na hasira zako maake hazina madhara_ungekuwa na madhara...hapo sawa.!
 
Pole sana kwanza acha pombe dia mtoto wa kike na pombe sio vizuri .pili una marafiki wa kike aina gani? Jaribu kuwa na urafiki na watu ambao sio watumia pombe.

Pale unapokuwa moodless nenda kwa huyo rafiki na ukifika fanyeni vitu vya kukurudisha kwenye mood mnaweza kuangalia movie etc. Acha pombe dia . pole sana
 
Pole sana dada yangu, Mimi pekee ndo nina dawa ya hasira zako. Hata hivyo hatua ya kwanza kuwa karibu na Mungu kwa kusikiliza kwaya. Acha kuangalia tamthilia na Movie za kutisha, pendelea kuangalia Comedy na kusikiliza mziki wa Kufurahisha sio hii Miziki ya kuumizwa.

Tembelea marafiki, Achana na Pombe, na vileo vyote. Ukipata nafasi uwe unaenda kutembelea beach. Jitahidi kutojibizana na mtu. Jifunze kuwa Mvumilivu. Safiri kubadilisha mazingira. Kuwa mbali na watu wanaokutia hasira.

Uwe unanitumia PM nikupe ushauri nasaha zaidi.

Pole tena ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom