Biashara ya kushauriwa wakati fulani siyo nzuri sana. Unatakiwa ukafanye utafiti mwenyewe ili uwe na uhakika wa kitu unachoenda kukifanya.
Ungetembelea hayo masoko ya Dar ili kujua bei ya kuuzia pamoja na usafiri, halafu ungeenda huko Lindi ili kuangalia upatikanaji wa hizo nazi. Baada ya hapo unafanya sasa tathmini kuona kama hiyo biashara itakulipa, au la.
Ni biashara nzuri, hakikisha zimekomaa na kukauka vizuri, hakikisha hazinyeshewi na mvua kipindi unasafirisha, hakikisha umeongea na wanunuzi wa jumla / madalali kabla ya kuleta mzigo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.