Naenda Tanga Kuoa

Naenda Tanga Kuoa

Mimi naogopa kuoa Tanga kwasababu ya zile story za kupelekwa bafuni umebebwa mgongoni, ukakarishwa kwenye kigoda na ma%#£¥£ kwenye kososi.
Maji yana hiriki na viungo sasa nikifikiria hayo naona hiyo kitu siyo style yangu.
 
Ambiele Kiviele ,
Mkuu, karibu sana Tanga, uoe hutakaa ujute.

Binafsi, Poise, sijawahi kujuta, hata nusu sekunde kwa kuoa mke kutoka Tanga.

Nashukuru sana Tanga, kuwa Tanzania!!

Cc: emmyta na wanawake wengine wa Tanga wote heko kwenu kwa kunipeni mke mwema mliyemfunda vyema.
Hapa Nilipo Nipo Moto Na Totoz Za Tanga Acha Tuu
 
Ambiele Kiviele ,
Mkuu, karibu sana Tanga, uoe hutakaa ujute.

Binafsi, Poise, sijawahi kujuta, hata nusu sekunde kwa kuoa mke kutoka Tanga.

Nashukuru sana Tanga, kuwa Tanzania!!

Cc: emmyta na wanawake wengine wa Tanga wote heko kwenu kwa kunipeni mke mwema mliyemfunda vyema.

Daah. Shukrani sana Shemeji.

Japokuwa saa nyingine huwa nawashangaa sana wale wenye kuipa hila Tanga ila ndio hivyo huwa sina jinsi.

Barikiwa sana Shemeji yangu. Pia nawaombea kwa Allah azidi kuwasimamia.

 
TANGA

Bora nikaoe Tanga, tena bint wa Pangani,
Yule anovaa kanga, na mitandio kichwani,
Aongea kwa kuringa, na lafudhi ya kipwani,
Awe na kauli njema, kwangu na kwa ikhwani.

Pangani nikimkosa, natafuta wa Handeni,
Niweze peleka posa, nioe niweke ndani,
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani,
Nitampenda kwa dhati, upendo toka moyoni.

Au nishuke Muheza, nikamsake mwandani,
Apate kuniliwaza, na uchovu wa kazini,
Najua hatanikwaza, kuniumiza moyoni,
Niliwazwe hasahasa, ili niwe wa thamani.

Au awe wa Lushoto, tena kule milimani,
Alozoea msoto, kupanda kushuka chini,
Azijua changamoto, zilizopo maishani,
Siku nikisema sina, asiende kwa jirani.

Au niende Korogwe, nimpate wa ubani,
Mchuzi atie ngogwe, nyanya chungu za mjini,
Nisemwe au nirogwe, sisikii na sioni,
Nitalia kwa makeke, akimtwaa fulani.

Wa Kilindi simpiti, na yeye namthamini,
Aweze kunidhibiti, ili nisitoke ndani,
Masham matashtiti, kwa udi pia ubani,
Katu asinisaliti, nikiwa na hali duni.

Ndugu zangu wa Mkinga, naomba nipokeeni,
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni.
Asiwe wa kujivunga, aishike sana dini,
Sio kama nabagua, natafuta mke mwema.

Au nibakie Tanga, nioe pale mjini,
Walipojaa nyakanga, wafundao wari ndani,
Panauzwa hadi shanga, sijui za kazi gani,
Kama nyumba nitajenga, hata kule mikanjuni.

Hapa sasa naishia, mawazo tele kichwani,
Wapi nitajipatia, mke yule mwenye shani,
Nipate kufurahia, raha ya ndoa ndoani,
Ila atokee Tanga, mjini au wilayani.

Cc : Mshana Jr
Na mimi nina mpango wa kwenda huko mwakani, ukifanikiwa uje na mrejesho
 
Daah. Shukrani sana Shemeji.

Japokuwa saa nyingine huwa nawashangaa sana wale wenye kuipa hila Tanga ila ndio hivyo huwa sina jinsi.

Barikiwa sana Shemeji yangu. Pia nawaombea kwa Allah azidi kuwasimamia.

Maneno Yana Nyama Nyingi Sana Haya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom