Pre GE2025 Tanga: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
4,012
13,796
Tanga.jpg

HISTORIA YA MKOA WA TANGA
Mkoa wa Tanga ni moja kati ya mikoa 31wenye eneo la 27,348 km² na upo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania ukipakana na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki na mikoa yaTANGA Morogoro, Manyara na Kilimanjaro. Mpaka upande wa kusini unafuata mto wa Mligaji. Mkoa wa Tanga unaunganisha sehemu za pwani pamoja na milima ya ndani kama Usambara.

Tanga inasemekana imeanzishwa na wafanyabiashara Waajemi katika karne ya 14 baada ya kristo, Baada ya kuanzishwa kwa ukoloni wa Kijerumani (DOA) mji ulikuwa makao makuu ya mkoa wa Tanga.

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Tanga ni 2,615,597; wanaume 1,275,665 na wanawake 1,339,932.

Pia, soma: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

MAJIMBO YA KIUCHAGUZI
Mkoa wa Tanga una jumla ya majimbo 12 ya kiuchaguzi. Majimbo haya ni;
  • Tanga Mjini
  • Muheza
  • Pangani
  • Korogwe Mjini
  • Korogwe Vijijini
  • Handeni Mjini
  • Handeni Vijijini
  • Kilindi
  • Lushoto
  • Mkinga
  • Mlalo
  • Bumbuli
HALI YA KISIASA
Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa ambayo kwa kiwango kikubwa nafasi za uongozi katika ngazi za serikali za mitaa, udiwani na ubunge zinashikiliwa na Chama cha Mapinduzi CCM ambapo hali hiyo ilisababishwa na uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu 2020.

uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 uliwapitisha bila kupingwa wagombea wa CCM huku mikoa mingine ambayo wagombea wake walipita bila kupingwa ni Katavi, Ruvuma na Njombe

Katika uchaguzi wa serikali za mitaa watia nia wa nafasi za uongozi katika nafasi hizo kutoka vyama vya upinzani walienguliwa kwa madai ya kukosa sifa za kugombea nafasi hizo na hivyo kupelekea kuondoa ushindani katika uchaguzi huo na kuacha wagombea wa Chama tawala CCM kupita bila kupingwa.

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu 2025, inatarajiwa kuwepo kwa mabadiliko na uimarishwaji wa demokrasia ili kutoa nafasi kwa vyama vyote kushiriki kikamilifu kwa uhuru na haki katika uchaguzi huo ili kutoa fursa kwa wananchi wote wenye mitazamo na milengo tofauti kugombea nafasi hizo.

MATOKEO YA UCHAGUZI 2020
Haya ni Matokeo ya idadi ya kura walizopata wagombea katika majimbo ya uchaguzi yaliyopo mkoa wa Arusha.

Jimbo la Uchaguzi la Handeni Mjini: Wagombea walikuwa watano. Mngatwa Twaha Said wa ADC alipata kura 310, Kwagilwa Reuben Nhamanilo wa CCM alipata kura 15,241, Andrew James Stima wa CHADEMA alipata kura 296, Sonia Jumaa Magogo wa CUF alipata kura 6,713, na Bakari Makame Semndili wa TLP alipata kura 31. Mgombea aliyeshinda ni Ndugu Kwagwilwa Reuben Nhamanilo wa CCM.

Jimbo la Uchaguzi la Handeni Vijijini: Wagombea walikuwa watatu. Doyo Hassan Mohamed wa ADC alipata kura 3,890, Sallu John Marko wa CCM alipata kura 94,900, na Bashiri Ally Muya wa CUF alipata kura 4,183. Mgombea aliyeshinda ni Ndugu Sallu John Marko wa CCM.

Jimbo la Uchaguzi la Kilindi: Wagombea walikuwa wanne. Maimuna Said Kassim wa ADC alipata kura 18,528, Kigua Omari Mohamed wa CCM alipata kura 61,777, Gadson Habibu Jaston wa CHADEMA alipata kura 1,388, na Tinker Abusheikh Mdimu wa CUF alipata kura 643. Mgombea aliyeshinda ni Ndugu Kigua Omari Mohamed wa CCM.

Jimbo la Uchaguzi la Korogwe Mjini: Wagombea walikuwa wanne. Bahati Hamadi Chirwa wa ACT-Wazalendo alipata kura 304, Alfred James Kimea wa CCM alipata kura 16,969, Wynjones Clarence Mwakolo wa CHADEMA alipata kura 2,116, na Amina Jumaa Magogo wa CUF alipata kura 1,497. Mgombea aliyeshinda ni Ndugu Alfred James Kimea wa CCM.

Jimbo la Uchaguzi la Korogwe Vijijini: Wagombea walikuwa watano. Juma Iddi Gao wa ADA-TADEA alipata kura 1,810, Pili Mohamedi Majeshi wa ADC alipata kura 1,157, Timotheo Paul Mnzava wa CCM alipata kura 48,078, Aminata AS Saguti wa CHADEMA alipata kura 12,092, na Magogo Hassan Jumaa wa CUF alipata kura 1,339. Mgombea aliyeshinda ni Ndugu Timotheo Paul Mnzava wa CCM.

Jimbo la Uchaguzi la Lushoto: Wagombea walikuwa wanne. Mwajabu Athumani Dhahabu wa ACT-Wazalendo alipata kura 1,163, Habani Omari Shekilindi wa CCM alipata kura 20,799, Mbelwa Walter Germano wa CHADEMA alipata kura 4,089, na Mshangama Ismail Abdi wa NCCR-Mageuzi alipata kura 3,246. Mgombea aliyeshinda ni Ndugu Habani Omari Shekilindi wa CCM.

Jimbo la Uchaguzi la Mkinga: Wagombea walikuwa wanne. Rehema Ally Mohamedi wa ACT-Wazalendo alipata kura 4,025, Kitandula Dunstan Luka wa CCM alipata kura 19,808, Bendera Jumaa Ally wa CHADEMA alipata kura 1,733, na Nuru Awadh Bafadhili wa CUF alipata kura 9,285. Mgombea aliyeshinda ni Ndugu Kitandula Dunstan Luka wa CCM.

Jimbo la Uchaguzi la Mlalo: Wagombea walikuwa watatu. Emmanuel Laurent Mnkai wa ACT-Wazalendo alipata kura 1,671, Shangazi Rashid Abdallah wa CCM alipata kura 46,632, na Shekiondo Amiri Mohamed wa CHADEMA alipata kura 2,803. Mgombea aliyeshinda ni Ndugu Shangazi Rashid Abdallah wa CCM.

Jimbo la Uchaguzi la Muheza: Wagombea walikuwa watano. Jamila Ally Mwakilachile wa ACT-Wazalendo alipata kura 1,223, Mwana FA Hamis Mohamed wa CCM alipata kura 47,578, Yosepher Ferdinand Komba wa CHADEMA alipata kura 12,038, Juma Peter Nindi wa CUF alipata kura 362, na Mhina Peter Mhina wa UDP alipata kura 194. Mgombea aliyeshinda ni Ndugu Mwana FA Hamis Mohamed wa CCM.

Jimbo la Uchaguzi la Tanga Mjini: Wagombea walikuwa wawili. Ummy Ally Mwalimu wa CCM alipata kura 114,445, na Mussa Bakari Mbarouk wa CUF alipata kura 7,497. Mgombea aliyeshinda ni Ndugu Ummy Ally Mwalimu wa CCM.

YANAYOJIRI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

JANUARY

FEBRUARY
  1. Mwenyekiti CCM Tanga: Tumeshuhudia uchaguzi wa CHADEMA wakitukanana, ni uthibitisho kuwa hawafai kupewa nafasi ya kuongoza nchi
  2. Tanga: CCM yachangia madawati Shule ya Sekondari Mgwashi
  3. Pre GE2025 Mwana FA asema atagombea tena ubunge wa jimbo la Muheza
  4. Tanga: Mjumbe wa kamati kuu UWT-Taifa achangia bati 40 kwa familia ya watoto yatima
  5. DC Muheza akabidhi Pikipiki 10 kwa UVCCM Tanga, ahamasisha Ushindi wa CCM
  6. Pre GE2025 Waziri Ridhiwani akabidhi hundi ya mil 730 kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu Muheza
  7. Pre GE2025 RC Dk. Batilda: Amewataka wananchi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura
  8. Mwenyekiti UWT Taifa: Lisu asiitishie serikali ya CCM "atulizane"
  9. Ummy Mwalimu awahimiza wakazi wa Tanga kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura
  10. Mwenyekiti kampeni ya 'Mama asemewe': Tupo tayari kuilinda nchi yetu kwa jasho na damu
  11. Mwenyekiti wa 'Mama Asemewe: Anayetaka tusishiriki katika uchaguzi kwa hoja zozote hana mapenzi na taifa letu
  12. Jiji la Tanga limepitisha rasimu ya bajeti ya Tsh. bilioni 25 kwa mwaka wa fedha 2025/2026
  13. Serikali yatoa bilioni 2.5 kuendeleza ujenzi hospitali ya Dtk. Samia Muheza
  14. Mwenyekiti CCM Tanga: Hakuna Elimu bila Ada sote tunalipiwa ada na Rais Samia
  15. Video: Mbele ya Rais Samia, Mbunge wa HandenI atangaza kuoga hadharani pindi mradi wa maji wa jimboni kwake utakapomalizika!
  16. Video: Samia Kings ( Chege, Madee na Ay) wakitumbuiza na kusema Samia mitano tena
  17. Rais Samia ashiriki kwenye uzinduzi wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga
  18. Serikali kuanza ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo)
  19. January Makamba: Kura za CCM uchaguzi Mkuu kuwa zaidi ya 90%
  20. ais Samia: Nilimpiga kikofi January leo namrudisha kwa mama
  21. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza kufanya uboreshaji wa daftari mkoani Tanga kuanzia Februari 13, 2025
  22. Rais Samia: Kwa wale wasiojua, baba yangu alikuwa mwalimu, kwa hiyo nayajua mazito ya walimu!
  23. Picha: Washiriki wa mafunzo ya waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki Tanga wakila kiapo kabla ya kuanza mafunzo
  24. Tanga: Afisa Mwandikishaji Handeni ataka waandikishaji wasaidizi kutunza siri za wananchi watakaojitokeza kujiandikisha
  25. Mkuu wa Wilaya ya Tanga akabidhi madaftari 1,000 yenye picha ya Rais Samia. Uchawa umefika kwa watoto wetu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom