Naenda Tanga Kuoa

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,271
29,879
TANGA

Bora nikaoe Tanga, tena bint wa Pangani,
Yule anovaa kanga, na mitandio kichwani,
Aongea kwa kuringa, na lafudhi ya kipwani,
Awe na kauli njema, kwangu na kwa ikhwani.

Pangani nikimkosa, natafuta wa Handeni,
Niweze peleka posa, nioe niweke ndani,
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani,
Nitampenda kwa dhati, upendo toka moyoni.

Au nishuke Muheza, nikamsake mwandani,
Apate kuniliwaza, na uchovu wa kazini,
Najua hatanikwaza, kuniumiza moyoni,
Niliwazwe hasahasa, ili niwe wa thamani.

Au awe wa Lushoto, tena kule milimani,
Alozoea msoto, kupanda kushuka chini,
Azijua changamoto, zilizopo maishani,
Siku nikisema sina, asiende kwa jirani.

Au niende Korogwe, nimpate wa ubani,
Mchuzi atie ngogwe, nyanya chungu za mjini,
Nisemwe au nirogwe, sisikii na sioni,
Nitalia kwa makeke, akimtwaa fulani.

Wa Kilindi simpiti, na yeye namthamini,
Aweze kunidhibiti, ili nisitoke ndani,
Masham matashtiti, kwa udi pia ubani,
Katu asinisaliti, nikiwa na hali duni.

Ndugu zangu wa Mkinga, naomba nipokeeni,
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni.
Asiwe wa kujivunga, aishike sana dini,
Sio kama nabagua, natafuta mke mwema.

Au nibakie Tanga, nioe pale mjini,
Walipojaa nyakanga, wafundao wari ndani,
Panauzwa hadi shanga, sijui za kazi gani,
Kama nyumba nitajenga, hata kule mikanjuni.

Hapa sasa naishia, mawazo tele kichwani,
Wapi nitajipatia, mke yule mwenye shani,
Nipate kufurahia, raha ya ndoa ndoani,
Ila atokee Tanga, mjini au wilayani.

Cc : Mshana Jr
 
Jipange na kuolewa tanga siyo watu wema..!
 
Tatizo la Watu wa Tanga walio wengi wametawaliwa na uchawi na ushirikina! Na ndo maana pamoja Kwamba iko karibu na Dar lakini maendeleo hakuna! Natamani ndugu zangu utokee uamsho utakao pelekea kuona uchawi na ushirikina hauna faida zaidi ya hasara!
 
TANGA

Bora nikaoe Tanga, tena bint wa Pangani,
Yule anovaa kanga, na mitandio kichwani,
Aongea kwa kuringa, na lafudhi ya kipwani,
Awe na kauli njema, kwangu na kwa ikhwani.

Pangani nikimkosa, natafuta wa Handeni,
Niweze peleka posa, nioe niweke ndani,
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani,
Nitampenda kwa dhati, upendo toka moyoni.

Au nishuke Muheza, nikamsake mwandani,
Apate kuniliwaza, na uchovu wa kazini,
Najua hatanikwaza, kuniumiza moyoni,
Niliwazwe hasahasa, ili niwe wa thamani.

Au awe wa Lushoto, tena kule milimani,
Alozoea msoto, kupanda kushuka chini,
Azijua changamoto, zilizopo maishani,
Siku nikisema sina, asiende kwa jirani.

Au niende Korogwe, nimpate wa ubani,
Mchuzi atie ngogwe, nyanya chungu za mjini,
Nisemwe au nirogwe, sisikii na sioni,
Nitalia kwa makeke, akimtwaa fulani.

Wa Kilindi simpiti, na yeye namthamini,
Aweze kunidhibiti, ili nisitoke ndani,
Masham matashtiti, kwa udi pia ubani,
Katu asinisaliti, nikiwa na hali duni.

Ndugu zangu wa Mkinga, naomba nipokeeni,
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni.
Asiwe wa kujivunga, aishike sana dini,
Sio kama nabagua, natafuta mke mwema.

Au nibakie Tanga, nioe pale mjini,
Walipojaa nyakanga, wafundao wari ndani,
Panauzwa hadi shanga, sijui za kazi gani,
Kama nyumba nitajenga, hata kule mikanjuni.

Hapa sasa naishia, mawazo tele kichwani,
Wapi nitajipatia, mke yule mwenye shani,
Nipate kufurahia, raha ya ndoa ndoani,
Ila atokee Tanga, mjini au wilayani.

Cc : Mshana Jr
Hongera mkuu upo vizuri kwa utunzi wa mashairi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom