Bora nikaoe Tanga

TASLIMA

JF-Expert Member
Jul 23, 2019
3,014
3,572
BORA NIKAOE TANGA

Bora nikaoe Tanga, tena binti wa Pangani,
Yule anovaa kanga, na mitandio kichwani,
Aongea kwa kuringa, na lafudhi ya kipwani,
Awe na kauli njema, kwangu na kwa ikhwani.

Pangani nikimkosa, natafuta wa Handeni,
Niweze peleka posa, nioe niweke ndani,
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani,
Nitampenda kwa dhati, upendo toka moyoni.

Au nishuke Muheza, nikamsake mwandani,
Apate kuniliwaza, na uchovu wa kazini,
Najua hatanikwaza, kuniumiza moyoni,
Niliwazwe hasahasa, ili niwe wa thamani.

Au awe wa Lushoto, tena kule milimani,
Alozoea msoto, kupanda kushuka chini,
Azijua changamoto, zilizopo maishani,
Siku nikisema sina, asiende kwa jirani.

Au niende Korogwe, nimpate wa ubani,
Mchuzi atie ngogwe, nyanya chungu za mjini,
Nisemwe au nirogwe, sisikii na sioni,
Nitalia kwa makeke, akimtwaa fulani.

Wa Kilindi simpiti, na yeye namthamini,
Aweze kunidhibiti, ili nisitoke ndani,
Masham matashtiti, kwa udi pia ubani,
Katu asinisaliti, nikiwa na hali duni.

Ndugu zangu wa Mkinga, naomba nipokeeni,
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni.
Asiwe wa kujivunga, aishike sana dini,
Sio kama nabagua, natafuta mke mwema.

Au nibakie Tanga, nioe pale mjini,
Walipojaa nyakanga, wafundao wari ndani,
Panauzwa hadi shanga, sijui za kazi gani,
Kama nyumba nitajenga, hata kule mikanjuni.

Hapa sasa naishia, mawazo tele kichwani,
Wapi nitajipatia, mke yule mwenye shani,
Nipate kufurahia, raha ya ndoa ndoani,
Ila atokee Tanga, mjini au wilayani.
 
Ukweli ninakwambia, unakoelekea utajutia,
Presha kujitaftia, kaburi kulisogelea,
Ndoa sio yakukimbilia, kichwa kichwa kuingia,
Punguza matarajio, mke hatafutwi hivyo.

Dunia imebadilika, sio kama zaman kabisa,
Utu umehadimika, upendo umepoa kwa sasa,
Pesa inathaminika, uthariti umezoeleka,
Punguza matarajio, mke hatafutwi hivyo.

Sijui niseme nini, ili kukusaidia,
Uwazapo raha za ndoani, kumbuka machungu pia,
Unaitajika umakini, ni mengi utapitia,
Punguza matarajio, mke hatafutwi hivyo.

Najaribu tu
 
Wamekusikia wanakusubiria
BORA NIKAOE TANGA

Bora nikaoe Tanga, tena bint wa Pangani,

Wanawake wa kitanga ni aina ya wanawake wenye kukidhi vigezo vizuri vya wastani vinavyopendwa na wanaume wengi.

Mwanamke wa kitanga;

-anajua kumsikiliza Mwanaume

Hakosi kuwa na adabu na heshima kwa Mwanaume

Umaridadi na usafi ni hadhi zao

Anajua kupika

Anajua huba

Anajua kumsitiri Mwanaume

Anajua mambo ya kitandani.

Anajua ukarimu kwa ndugu wa mume na
majirani.

Anaelewa lugha ya kuluzu

N.k.
 
Ukweli ninakwambia, unakoelekea utajutia,
Presha kujitaftia, kaburi kulisogelea,
Ndoa sio yakukimbilia, kichwa kichwa kuingia,
Punguza matarajio, mke hatafutwi hivyo.

Dunia imebadilika, sio kama zaman kabisa,
Utu umehadimika, upendo umepoa kwa sasa,
Pesa inathaminika, uthariti umezoeleka,
Punguza matarajio, mke hatafutwi hivyo.

Sijui niseme nini, ili kukusaidia,
Uwazapo raha za ndoani, kumbuka machungu pia,
Unaitajika umakini, ni mengi utapitia,
Punguza matarajio, mke hatafutwi hivyo.

Najaribu tu
Hongera mkuu, haya mashairi mie siyaelewi tangu shule huko.
 
Back
Top Bottom