Mzee wa Upako amchana live TB joshua

Mzee wa Upako amchana live TB joshua

Kazi mnayo nyie waamini mambo ya kufikirika tu ambayo huwezi kuthibitisha kabisa. Ila nawahakikishia kuwa hakuna aliye sahihi katika imani yake kama mtaanza kuchunguzana.
 
Shetani yupo kwenye kampeni. Watu wa Mungu wawe makini wasimpe shetani nafasi.
 
Asijilinganishe na Tb joshua kwanza tb joshua anatimiza maandiko ,yakobo 1:27 dini iliyo safi kuwajali wenye mahitaji
Yy Lusekelo anakunja noti za kutunzwa
 
Wache wafu wazike wafu wenzi wao........ sisi yetu macho maana tukisema tusije pigwa ban buree na JF twaipenda...... maana sisi twajua mtume wa mwisho ni nani hawa wengine ........opppssss nimeropoka tena

Hao wa mtume wa mwisho wanamiminika kwa TB Joshua kila siku na wanapewa misaada ya kila aina.TB Joshua ni mtu wa Mungu hakika asiye na makuu
 
Sasa hapo ni shida tayari,wao wenyewe wanaanza kutoleana siri,kama ni kweli wachungaji wana magumashi,fulani fulani basi hata yeye hayuko salama sana,yeye kaweza kutoa siri au tuseme kaweza kusema aliyosema na yeye basi mtu/mchungaji hapahapa nchini mikoani,waumini wake au hata washirika wake wanajua magumashi yake,mambo ya kuzua ugomvi kurusha mawe uswazi na unaishi nyumba ya vioo,tusubiri mtasikia tu.
 
Hivi jamani tumesahau ni miaka michache mzee wa upako alianzisha tifu na Kakobe,mwenzako kwa kutumia neno lile kukaa kimya nako ni hekima hivyo alimpuuza,baadaye kidogo akawatukana maaskofu eti wapenda mwaliko wa rais Ikulu kwa ajili ya chai na kupiga picha.Kama walivyotangulia kusema wengine toa kwanza boriti kwenye jicho la mwenzio.Sisi kwetu tunawahesabu ninyi nyote ni watumishi wa Mungu mnaoleta ujumbe wa Mungu kwa staili tofauti 1Kor 3:5-9 Phil 1:18
 
Hawa wote ni free masons, wanamuwakilisha shetani, biblia huwaita manabii wa uongo, ambao wanatenda miujiza hata kutekemsha moto kutoka mbinguni mbele ya macho yenu.hebu soma hii nukuu "Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. (MT. 24:5 SUV)". Yohana anaonya pia "Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. (1 YOH. 4:1 SUV)". Kipimo pekee ni biblia, epuka mapokeo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tanzania mijitu mijinga inatapeliwa wenzao wanapata pesa tu.yao yanakufa maskin
 
Sijawahi kumuamini lusekelo hata siku moja hvyo namchukulia kama watu wa kawaida.

Na watu wa kawaida hawajawahi kuacha kuwasema watumishi wa MUNGU vibaya yani watatfuta sababu yoyote tu ya kwenda kinyume naye hata kama hawajui undani wake ni ngumu kwa giza kuikubali NURU na haya yamekuwepo tokea enzi


[h=1]Mathayo 11 : 18-19[/h]11.18 Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.
11.19 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.

wataunda zengwe tu ilikukuweka ugly na hizi ndio roho zilizo wajaza negativity.
 
Huyu ni mchungaji utapeli wake ni ngazi ya uchungaji lakini Joshua ni next level, yeye ni nabii. Nabii anapashwa kuwa na uwezo kuona mambo yatakayotokea kabla hayajatokea. Je uwezo huu Joshua anao? Au ndo hizo za kuwasiliana na CIA, wanamtonya halafu yeye anatangaza?

Huyo jamaa sijawahi kumwamini hata siku moja.

Tiba

Hahahaa haaaa
Tell them na ukiona ana jealous ujue kabeba roho nyingine coz watumishi wa kweli wenye Roho wa Mungu hawapingani...na bado
Ile ni deepest watahangaika mwishoni wataenda kuwa delivered km wachungaji wengine
Lusekelo hugusi na hatakaa aguse ile level
 
  • Thanks
Reactions: Kbd
mleta uzi ...
yamkini haya yaliyomo ndani ya uzi wako ni mawazo yako binafsi... na kama sivyo basi ungetuwekea clip ili nasi tumsikie yawezekana hukumnukuu vema..
PILI; kuyatumia majina matakatifu katika marumbano yasio na tija ni hatari sana kwa mstakabari wa maisha yako mbeleni, majina matakatifu achilia mbali aliye libeba na tabia zake lakini lile jina usithubutu kulitumia visivyo narejea tena itakula kwako ...
majina yenyewe ni haya MCHUNGAJI (PASTOR), NABII(PROPHET) ASKOFU(BISHOP) na mengine mengi yafananayo na hayo
 
Lusekelo.
Anatunzwa Jamani Hikitu Kwangu Mi Ina Nichanganya Sana Kutunzwa Kama Msani Waumini Wote Hao Hatosheki Bado Mpaka Kutunzwa Mmh Hela Hufi Nazo Mchungaji Punguza Njaa Kali Eti Anaongea Ongea Mambo Sijui Umbea Umbea Wa Family Ana Maliza Akisema Haloo Watu Wanapita Wanaenda Mtunzaa Jamani Hapana Aiseh Hayo Sio Makanisa Yakiroho Hayo Ni Yakipesa Zaidi?
Lusekelo Achana Na Hayo Mambo Ya Kutunzwa Bana Unatia Aibu?
 
Sawa kabisa. Kwa nini asimuombe Mungu wake kusitisha machafuko yanayotokea Nigeria. Pia anaona raha gani kutoa utabiri wa maafa kutokea pasipo kutoa tahadhari ya kuzuia maafa hayo kwa kumuomba Mungu?

Ww umeelewa alichoandika Mtazamo au umejibu tu?
Soma tena.
 
Mungu atuongoze na kutuonyesha njia sahihi. Kiukweli haya mambo ni magumu sana.

Magumu kwako kwa sbb hauna Roho Mtakatifu wa kukuongoza na kukuonyesha yupi ni mtumishi wa kweli na uupi sio, na kwa sbb tb joshua unamsikia kwenye vijiwe humfaham yy wala kazi zake
 
Back
Top Bottom