Kwa uelewa wa kawaida usio wa "elimu ya bongo ya tests na kukaa vitini" kama ilivyotamkwa hapo juu, sidhani kama tuliowengi tumeyasoma mawazo ya mtoa mada na kwenda zaidi ya kutoa hoja zetu. Suala la TB Joshua kuwa nabii huku maafa makubwa yakitokea ndani ya nchi yake mwenyewe bila hata kuyazuia ama kutabiri kuwa yangetokea nadhani ndo ilikuwa hoja ya Mzee wa Upako kujustify unabii hewa wa TB Joshua na wengine wenye jina la nabii. Lakini kwa upande wa pili wa shilingi, mzee wa "Upako" amesahau kuwa yeye mwenyewe yuko katika kikaango kilekile kwa watu kuanza kulizungumzia hata jina lake na maana halisi ya neno UPAKO kama ni sahihi ama la na humaanisha nini. Kwa uelewa wangu wa kawaida (wa kushika Biblia na vitabu vingine vya dini kwa matukio), neno "upako" limetokanana na kile kinachoaminika kuwa ni nguvu za Mungu kwa namna alivyowavuvia ama kuwapaka mafuta (anointment) watumishi wake ambao kwa neno jingine huitwa "Manabii" (prophets). Kama yeye pia si mmoja wa manabii ama wale wanojiita jina hilo ningeona ni busara kama angefafanua hilo kwanza kisha akaanza itupia mawe nyumba ya jirani yake. Ni upako upi huo ambao yeye anao na wengine wameukosa??? Hoja ya kutoweza kuzuia maafa ndani ya nchi yake na hata sehemu nyingine nje ya eneo lake, hazimfanyi TB Joshua kutokuwa nabii kwani hata Yesu pia hakuzuia baadhi ya mambo yasitokee bali kuyaacha yatimie kwani ilikuwa ni sehemu ya mpango wa Mungu kuonesha utukufu wake mf. kusalitiwa na Yuda (alilijua mapema), kifo cha Lazaro, mateso na hata kifo chake n.k vyote hivi alivijua lakini hakuvizuia (nisiulizwe juu ya kutekwa kwa mabinti wa kinaijeria kama ni mpango wa Mungu ama wa Boko kharam). Siwezi sema kati ya hawa wawili yupi ni nabii wa uongo ama la kwani kumtaja mmoja kati yao ni ku-take side ama kujipa 'unabii' wa aina yangu hivyo suala la nani alitabiriwa ni wa uongo ama la ninaliacha kwenu. Mzee wa Upako anasahau kuwa yeye pia ni nabii ukiachilia kuwa hajiiti jina hilo (kutolitumia haina maana siye) kwani a "PROPHET is a person who is believed to have a special power which allows them to say what God or a god wishes to tell people, especially (not necessarily) about things that will happen in the future". Yeye pia huwatabiria watu kuwa watakuwa matajiri, kupona magonjwa yao na mengine makubwa in no time na kwa shuhuda za "wanae" kama awaitavyo, yale aliyoyasema yali/yametimia tena double-double kama si zaidi ya hapo, hivyo ni nabii pia. Kazi ya nabii ni "kuyatimiza yale anayoagizwa na aliyemtuma (be it God or a god of its own kind) na si kufanya chochote ili watu waone kuwa amefanya". Uwezo wa kuyafanya hayo yote hutoka kwa aliyemuagiza na si vile apendezwavyo yeye vinginevyo hata Yesu angetengeneza makontena ya mikate kumuonesha shetani kuwa anaweza. Mimi napita tu!