MIHAYO1710
Member
- Apr 7, 2018
- 22
- 59
“Kingdom True Anointing Standards: A RENAISSANCE”
Ni makala ndefu, kwa sababu hata watu wamedanganywa kwa kirefu! Uongo mkubwa unahitaji maelezo Makubwa!
Mwenye moyo na nguvu na asome!
AMANI NA SALAMA!
Mimi ni mzima wa afya, Karibu tujifunze!
**Kama umekuwa ukisikia habari za Mafuta ya Upako na Hujui Msingi wa Fundisho hilo, Nakusihi usome hapa, huenda ukaongeza kitu!
Kumekuwa na kutokuelewana na kupingana juu ya ‘MAFUTA YA UPAKO’ Lipo kundi linaloyatetea, kuyatumia na kuyauza hali kadhalika lipo kundi linalopinga kwa nguvu.
Mchuano huo umeleta mgawanyiko mkubwa, Msingi wa kutokuelewana huku ni kwamba sababu zinazotolewa na kila upande hazijitoshelezi kukata kabisa kiu ya waumini ili kuhalalisha au kuharamisha mafuta ya UPAKO!
Mimi kama Mwalimu, leo najitolea kukufundisha, kinaganaga asili, maana, maendeleo na uhalisia wa mafuta ya UPAKO kuanzia agano la kale, tamaduni za mashariki ya kati, mpaka katika kanisa la leo.
FUATANA NAMI KWA UTULIVU NA UVUMILIVU!
MAFUTA KATIKA AGANO LA KALE NA UTAMADUNI WA MASHARIKI YA KATI
Katika agano la kale, watu wa mashariki ya kati walikuwa na utamaduni wao juu ya mafuta, Utamduni huo upo na unanendelea mpaka sasa!
Mafuta yalikuwa na kazi kadha wa kadha, kama vile kutawadha wafalme, Kubarikia, KULAKI, kutibu magonjwa na udhaifu na matumizi ya kawaida ya jikoni kama ifuatavyo!
1. KUTAWADHA MFALME
Kumiminiwa mafuta kichwani ilikuwa ishara ya kusimikwa kwa mfalme. Mafuta yalipopakwa kichwani ilikuwa kiashiria cha kujiliwa na Roho ya Mungu na hivyo kuwa kama kibali cha kutawala kwa niaba ya Mungu!
Kwa hiyo mafuta yalitumika ‘symbolically’ kama ishara ya kushukiwa na Roho wa Mungu! (mafuta hayakuwa Roho, lakini yalikuwa ishara ya Roho Mtakatifu)
1Samweli 16:12-13 “Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, ‘Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye! Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka akaenda zake Rama.”
Umeona? Baada ya kumwagiwa mafuta hatua iliyokuwa inafuata ni kujiliwa na Roho wa Bwana!
Zaburi 89:20 (nimemwona Daudi, nimempaka mafuta)
Zaburi 92:10 “Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa mafuta mabichi.”
2. MAFUTA KWA AJILI YA BARAKA
Mafuta haya chimbuko lake ni Baraka alizokuwa anazitoa nabii Musa kwa makabila 12 ya waisraeli kabla ya kifo chake!
Kabila la Asheri ndilo lilifundishwa kufanywa hivyo
Kumbukumbu la torati 33:24-25 “Na Asheri akamnena, ‘Na abarikiwe Asheri kwa watoto! Na akubaliwe katika nduguze, na achovye mguu wake katika mafuta. Makomeo yako yatakuwa chuma na shaba, na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.”
Fundisho la mafuta ya upako kwa kiasi kikubwa limekita mizizi yake hapa! Watu wote ambao hupenda matumizi ya mafuta mara kwa mara hunukuu aya hiyo!
JE, SISI TUNATEMBELEA BARAKA ZA MUSA AU ZA KRISTO?
Watoto wa Ufalme wa Mungu, hawatembelei channel za nabii Musa pamoja na torati yake na tanzu na vipera vyake!
Waefeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo”
Kwa nini?
Sababu ni hii hapa chini
Wagalatia 3:24 "Sheria/torati ilikuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo aliye mwisho wa sheria”
Kwa hiyo maelekezo yaliyotolewa kwa kabila moja la Asheri katika Israeli hayawezi kuwa mwongozo kwa watoto wa agano jipya lililo bora zaidi!
Kwa maana imeadnikwa!
Waebrania 7:22 "Kwa kadiri hii, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo Bora zaidi"
Kwa hiyo mambo yote ya kipindi cha Musa yalikuja kupata ufafanuzi bora zaidi katika Kristo!
Yohane 1:17 "Kwa kuwa Torati ililetwa kwa Mkono wa Musa; Neema na kweli zilikuja kwa Mkono wa Yesu Kristo."
Kwa hiyo waacheni Waasheri waliomkataa Yesu waendelee kukanyaga mafuta ili wabarikiwe! Nyinyi Wanyakyusa, wasukuma etc hamna fungu kwa kabila la Asheri, ni bora kujiitiisha chini ya Kristo ambae Baraka zake hazina mipaka ya kikabila wala mataifa, na muhimu zaidi Baraka za Kristo haziji kwa kukanyaga mafuta!
Tena zama za Musa zilipita na iliwekwa wazi!
Luka 16:16 "Torati na manabii vilikuwepo mpaka Yohane; tangu wakati huo habari njema ya Ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa Nguvu."
Unakubali kuwa habari hizo unazozing’ang’ania ni zilipendwa?
Ndiyo maana Sauti kutoka mbinguni ilisikika Yesu akiwa amesimama na Musa na Eliya kwamba “Huyu ndiyo mwanangu mpendwa, msikieni yeye!”rejea Marko 10:2-4
Kushindwa kumsikia Kristo na kung’ang’ania desturi za kabila la Asheri ni upumbavu!
3. MAFUTA KWA AJILI YA KULAKI NA KUONESHA UPENDO
Kwa wayahudi ilikuwa kawaida kumpaka mgeni mafuta kichwani au miguuni kama ishara ya upendo wa dhati, kukaribisha na kulaki.
Rejea habari za mwanamke aliyemmiminia Yesu Marhamu kama kuonyesha pendo lake kwa Yesu kutokana na kusamehewa dhambi zake! (Luka 7:36-50)
4. MAFUTA YA KUHIFADHIA MAITI
Kwa wayahudi ilikuwa ni swala la kawaida kupaka mafuta ya manukato maiti !
Rejea hapa (Marko 16:1 na marko 14:8)
5. MAFUTA KWA AJILI YA DAWA.
Katika Mashariki ya kati tangu zamani za kale mafuta yalitumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali na udhaifu, na mpaka sasa mafuta hayo yapo na hutumika kwa kazi hiyo bila kuzingatia mipaka ya kiimani, wala kuhusishwa na upako!
Mafuta ya mzeituni yalitumika kuimarisha watu dhaifu, manusura wa vita na wakati mwingine majeruhi walipakwa mafuta hayo kwenye jeraha zao.
2Nyakati 28:14-15 “Basi watu wenye silaha wakawaacha wafungwa na nyara mbele ya wakuu na kusanyiko lote. Wakaondoka wale watu waliotajwa majina yao, wakawatwaa wafungwa, wakawavika kwa zile nyara wote wao waliokuwa uchi, wakawapa mavazi na viatu, wakawalisha, wakawanywesha, WAKAWATIA MAFUTA, wakawapandisha waliokuwa dhaifu miongoni mwao juu ya punda, wakawaleta Yeriko, mji wa mitende, kwa ndugu zao, kisha wakarudi Samaria.”
Hawa walikuwa manusura wa vita kati ya mfalme Ahazi wa Yerusalemu dhidi ya ufalme wa Shamu! Kwa hiyo mafuta pale yalitumika kama huduma ya kwanza!
Ndivyo ilivyo mpaka leo kwa watu wote, wapagani, waislam, wakristo, wayuda etc waishio mashariki ya kati, bado hutumia mafuta hayo kama dawa bila kuhusishwa na imani. Hata maeneo ya misikiti hapa Tanzania mafuta hayo huuzwa!
Tiba ya namna ile BWANA YESU alikuja kuizungumzia alipokuwa akieleza maana ya ujirani na jirani! (luka 10:29-37) kwamba Yule majeruhi alipakwa mafuta jeraha zake na msamaria mwema, kumbuka wasamaria walihesabika kama wapagani! Lakini kwa kuwa mafuta tiba hayakuhusishwa na imani, hata watu wa Samaria waliyatumia kama dawa! Kwa hiyo hayakuwa Mafuta ya upako, yalikuwa mafuta dawa!
Kwa sababu hiyo, Mafuta ya mzeituni yanatajwa kusaidia kutibu
vidonda vya tumbo,
Huduma ya kwanza kwa aliyekunywa sumu
Hutibu ugonjwa wa kusahahu
Ni msaada kwa wanaokojoa kitandani
Huua minyoo tumboni
Huongeza nguvu za kiume
Hupunguza lehamu (cholestro) mwilini
Tiba ya degedege
Hukausha majeraha
Huzuia kansa ya matiti
Pia hutumika kurefusha nywele
Hupunguza makali ya njaa
Hutibu mafua nk!
#Kumbuka, uponyaji na msaada huu wa zeituni hautegemei maombi wala nini, ni dawa kama Mseto ya malaria ilivyo!
Ukitaka ujue kabisa kuwa ni dawa kama dawa zingine, Hata dini ya kiislamu hutumia mafuta hayo hayo na kwa kazi hiyo hiyo!
Katika Quran, Mtume wao Mhamedi amaufia mzeutuni, mafuta yake na matunda yake!
Na mti (mzeituni) unaoinuka kutoka Mlimani Sinai, una mafuta, na ni furaha kwa wala. (Quran 23:20).
Pia mahala pengine Mtume Muhammad pia aliwaambia wafuasi wake:
“Kuleni mzeituni na mjitake mafuta pamoja nao, kwa maana ni kwa mti mzuri.”
Kwa hiyo, Mafuta hayo hayana uhusiano wowote na UFALME WA MUNGU, ni moja ya tiba za kienyeji kule mashariki ya kati!
6. MAFUTA KWA MATUMIZI YA JIKONI
Kama ilivyo leo, tangu zamani mafuta yamekuwa yakitumika kwa shughuli za jikoni na upishi kwa ujumla.
1Wafalme 17:10-16 (Eliya na Mjane wa Sarepta) Mafuta yale yaliyofanyiwa muujiza na nabii Eliya hayakuwa kwa ajili ya kutawadhia mfalme au dawa! Yalikuwa mafuta kwa ajili ya kuokea mikate na mapishi mengine ya jikoni!
TUREJEE KWENYE MADA!
AGANO JIPYA NA MATUMIZI YA MAFUTA
Katika agano jipya, hakuna kabisa matumizi ya mafuta katika maombi na maombezi! Wala huwezi kumpokea Roho mtakatifu kwa kumiminiwa mafuta kichwani asilani!
Na madhehebu yanayoendelea kufanya hivyo ni ishara ya eitha ujinga, ulimbukeni, kuiga tamaduni zilizopitwa na wakati au biashara kama wanavyopiga pesa wengine!
KWA NINI?
Katika agano la kale kila jambo lilifanyika kwa mafumbo na kama mfano! (1 Kor 10:11)
Uhalisia wa maana na picha kamili ya kila kilichokuwa kinafanyika katika agano la kale unadhihirika na kuwekwa wazi katika agano jipya!
KIVIPI?
Mjumbe wa agano jipya (Yesu Kristo) alipokaribia, michakato ya kupakwa ama kumwagiwa mafuta ili umpokee Roho Mtakatifu kama tulivyoona katika (1Samweli 16:12-13) ilikoma!
Na ndiyo maana mtangulizi wa Yesu kwa jina la Yohane Mbatizaji hakupakwa wala kumwagiwa mafuta na mtu!
Bali alijazwa Roho Mtakatifu tangu akiwa tumboni mwa mama yake! (Luka 1:15)
Au utasema huenda mama yeke Elizabeti alikunywa mafuta ya upako? Shauri yako!
Hali hii ilimaanisha kwamba liturujia ya kidini ya kupaka na kumwagia mafuta wafalme na manabii kwa ajili ya kujiliwa na Roho Mtakatifu ilikuwa ikielekea ukingoni kabisa!
YESU HAKUPAKWA MAFUTA!
Mbeba agano jipya hakuwahi kupakwa mafuta kwa maana ya kumwagiwa mafuta kichwani na raia yeyote, kama ilivyodhaniwa katika agano la kale, Pamoja na ukweli kwamba nabii Isaya alitabiri habari za masihi kupakwa mafuta katika Isaya 61:1, hata hivyo anaanza kazi kwa kusoma tu, na siyo kupakwa mafuta kabisa na kuhani!
Rejea Luka 4:16-22
Wayahudi walishtuka, alipowajulisha kuwa andiko lile limetimia wakati hawaoni mtu akimtia mafuta kwa macho yao! Ilibidi wafanye jaribio la kumuua kabisa, akawaponyoka!
KWA HIYO MAFUTA NI NINI KATIKA AGANO JIPYA?
Mafuta ni KISAWE cha Roho Mtakatifu! Roho Mtakatifu ana a.k.a nyingi! Mfano anajulikana kama kidole cha Mungu (luka 11:20 ufafanuzi wake ni mathayo 12:28)
Sijui sana kama unanielewa!
Labda, kwa mfano mimi Charles Mganda, nizae mtoto nimwite jina lake chumvi, je atakuwa chumvi kweli? Ndivyo ilivyo kwa Roho Mtakatifu, jina jingine ni kidole cha Mungu lakini pia jina jingine ni MAFUTA!
USHAHIDI UKO WAPI?
Soma hapa kwa uangalifu na utulivu zaidi!
1Yohane 2:20, 27
20 “Nanyi mmepakwa MAFUTA na Yeye aliye mtakatifu, nanyi mwajua yote.”
27. Nanyi, MAFUTa yale mliyoyapata kwake, yanakaa ndani yenu, Wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; Lakini kama MAFUTA yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo. Na kama YALIVYOWAFUNDISHA, kaeni ndani yake”
*Hapa tunapata mambo mawili muhimu sana!
Kwanza, Mafuta halisi hayapakwi nje, bali yanakaa ndani kama ilivyokuwa ahadi ya Yesu kumtuma wake Roho Mtakatifu kwamba atakaa ndani yetu hata milele! (Yohane 14:15-17 Roho Mtakatifu, atakaa ndani yenu)
Na Warumi 8:11 “Lakini ikiwa Roho wake yeyealiyemfufua Yesu ANAKAA NDANI YENU, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.”
Umeelewa dhana ya MAFUTA kukaa ndani?
Pili, Mafuta yanafundisha! Fikiri kiungwana, unaweza kupaka mafuta au kukanyaga au kunywa ukapata hekima? Ukajifunza kitu? Sasa tumeambiwa hapo juu, mafuta yenyewe yakitufundisha hakuna haja tena ya kufundishwa kitu na mtu!
Huduma ya kufundisha katika agano jipya ni huduma ya Roho Mtakatifu! Kwa hiyo suala la muhimu ni kuwa na Roho mtakatifu kabla ya kujifunza wala kusoma chochote!
Yesu alisema hivi!
Yohane 16:12-13 (Roho Mtakatifu atawafundisha yote na kuwatia kwenye kweli yote)
ROHO MTAKATIFU NA MITUME
Katika hali ya uwazi zaidi, inayothibitisha kwamba agano jipya halihitaji mafuta ni Ujio wa Roho Mtakatifu!
Yesu aliwavuvia Roho Mtakatifu bila kulazimika kuwamwagia mafuta! (Yohane 20:22-23) waliambiwa pokeeni Roho Mtakatifu, hawakumiminiwa mafuta!
Na katika siku ya Pentekoste, Roho Mtakatifu aliwajilia wakiwa wamejifungia ndani ya nyumba! Hakuna kuhani wala nabii aliwamwagia mafuta ili wapokee upako wa Roho Mtakatifu! Aliwashukia tu! (Mdo2)
HATA MIZIGO YETU INAONDOLEWA NA MAFUTA
Bwana Wetu Yesu Kristo alitupa mwaliko wa kutuchukulia mizigo yetu!
Mathayo 11:28-30 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na MIZIGO, nami nitawapumzisha, Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.”
Hata hivyo, manabii wa zamani walijua na kutabiri kuwa mizigo na nira hiyo huweza kuondoka kwa MAFUTA halisi, ambaye ni Roho Mtakatifu!
Isaya 10:27 “Tena itakuwa katika siku hiyo, mzigo wake utaondoka begani mwako, Na nira yake shingoni mwako, Nayo nira itaharibiwa. Kwa sababu ya kutiwa MAFUTA!”
Au ninene kwa lugha za malaika ndiyo sikio lako litazibuka na kuelewa?
Mzigo wa kubeba dini moyoni na makandokando yake hauwezi kuondoka bila ya wewe kujiachilia kwenye MAFUTA halisi, ambaye ni Roho Mtakatifu!
KWA NINI WANAFUNZI WA YESU WALITUMIA MAFUTA?
Marko 6:12-13 “Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu. Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza.”
Yakobo 5:13-15 “Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi. Mtu wa
kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa, nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa Yule, na Bwana atamwinua; Hata akiwa amefanya dhambi atasamehewa.”
Wanafunzi wote wa Yesu walikuwa wayahudi wenyeji wa Israeli. Kama nilivyotangulia kusema kule juu, mafuta ya mzeituni ni dawa!
Kwa hiyo waliendelea kuwapaka baadhi ya wagonjwa mafuta, ‘SIYO YA UPAKO’
Haya huitwa matendo ya huruma na mtu atendaye hayo ana heri kubwa mbinguni!
Kwa mfano, Mtu akaja kuomba msaada wa maombi kwangu, akanieleza kwamba anasumbuliwa na choo kigumu, “constipation”
Nitamwombea mtu huyo kwa imani na ikiwezekana nitamshauri anunue mafuta ya samaki anywe kwa maana ni dawa iliyothibitishwa na mamlaka ya chakula na dawa kuwa inalainisha choo, zaidi naweza kumshauri kula matunda kwa wingi kama vile papai, nanasi, tikiti maji au tango kwa maana ni matunda kinara katika kulainisha choo !
Nikijifanya kuyaombea yageuke dawa nitakuwa naanza sasa kufanya comedy. Kwa sababu hayategemei maombi ili yafanye kazi!
KWA HIYO DAWA ZINARUHUSIWA?
Usijitie ujuaji wa kipumbavu! Usijifanye wa kiroho kuliko Roho Mwenyewe! Hata Paulo alimshauri kijana wake katika imani atumie mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo na magonjwa yaliyokuwa yakimpata mara kwa mara!
Soma mwenyewe hapa!
1Timotheo 5:23 “Tokea sasa usinywe maji tu, lakini tumia mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lako na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.”
*Akili duni za kilokole zinaweza kuhoji, ina maana Paulo alishindwa kumwombea tu Timotheo mpaka akamshauri atumie mvinyo kama dawa?
Ndivyo ilivyo, hata mimi huwa nameza “Omeplazzle capusule” kwa ajili ya vidonda vya tumbo, saa nyingine huwa natumia asali na kujiepusha na vyakula vyenye acidity!
Kivipi sijui kuomba? Sina imani? Utajaza mwenyewe! Maana dini zinawahabibu sana akili!
KWA NINI MIMI NILIPONA KWA KUTUMIA MAFUTA?
Kuna mama mtu mzima, tena afisa huko wizara ya afya aliwahi kuniuliza, kama MAFUTA hayo ni FEKI kwa nini yalinisadia nikapata nafuu ya tumbo langu?
Jibu: Mafuta hayo ni dawa ya magonjwa mengi kwa asili, ndivyo Mungu alivyouumba huo mmea! Kwa hiyo kilichokusaidia siyo Upako wa yale mafuta lakini ni ile dawa!
Dawa yoyote ya hospitali haihitaji maombi ili ifanye reactin kwenye mwili!
UFEKI WAKE
Ufeki wa mafuta haya ni pale yanapohusishwa na imani! Ikiwa ni hivyo basi hata waislamu wanatumia upako huo huo maana wao ndiyo huyatumia zaidi kwa matumizi mengi, ikiwemo kufukuza masheitwani!
NYONGEZA YA ZIADA
Yesu aliponya kwa namna na style mbalimbali!
Wengine alitengeza tope la udongo kwa mate yake wakapona (Yohane 9:6)
Wengine waligusa mavazi yake wakapona (Luka 8:44 na Mathayo 14:36)
Wengine aliwawekea mikono wakapona (Luka 13:13)
Wengine walipona kwa kusikiliza neno lake tu (Mathayo8:16-17)
Wengine walipona bila hata kukutana naye uso kwa uso (Mathayo 8:8-14)
Wengine waliambiwa tu wakajionyeshe kwa makuhani (Luka 17:11-19)
Wangine walipona bila hata kuomba waombewe, waliambiwa tu (Yohane 5:1-18)
Wengine aliwaambia wakanawe tu kama ilivyokuwa kwa Naaman (Yohane 9:1-41)
Alitembea juu ya maji
Alifufua wafu
Alilisha watu maelfu kimiujiza na kufanya mambo mengi zana hata mengine hayakuandikwa!
KWA UPANDE WA MITUME
Wengine walipona kwa kugusa mavazi na leso za Mtume Paulo tu (Matendo ya Mitume 19:11-12)
Wengine walisimama karibu na kivuli cha Petro tu, na kupona (Matendo ya Mitume 5:12-16)
HATA HIVYO IKO HIVI
Mwisho wa yote Yesu aliwaamuru wafuasi wake kufanya yote hayo hata zaidi KWA JINA LAKE! (Marko 16:14-18, kwa jina langu watafanya ABC)
KWA HIYO?
Kupona kwa kugusa pindo, kivuli ni imani na ufunuo maalumu wa mgonjwa, siyo fundisho!
Baadhi ya miujiza, ni sehemu ya huduma katika ofisi ya kinabii, na ni nadra kufanyika mara kwa mara! i.e kutengeneza tope la mate ni ufunuo wa kinabii, siyo fundisho! (kwa sababu nahisi muda si mrefu litatokea kanisa la kuponya kwa mate)
Baadhi ya miujiza ilikuwa ni kuthibitishwa uungu wake!
NAJUA UMESHACHOKA SANA KUSOMA MAKALA NDEFU! NIISHIE HAPA KWANZA!
TAFAKARI, CHUKUA HATUA!
Ufalme wa Mungu njoo!
Kama hujampa Yesu Kristo maisha yako,
Hii ni fursa kwako kufanya hivyo, Karibu katika Ufalme wa Mungu
Umebarikiwa Milele!
KUMBUKA
#Shetani Anaogopa mtu anayejua kitu!