Mzee wa Upako amchana live TB joshua

Mzee wa Upako amchana live TB joshua

Dhambi hii anayo ifanya lusemelo itammaliza mwenyewe,kila nabii aliyekuja alikuja na unabii wake hawakufanana,nashangaa kitu kimoja kazi wanayofanya ni moja ya MUNGU anamkashifu nini acha wanao ponywa kupitia TB Joshua MUNGU anyanyuliwe,na wanao ponywa kupitia Lusekelu MUNGU ainuliwe pia ,wewe umewahi kutabiri nini kikatokea, hivi CIA wanauwezo wakujuwa kuwa ndege itapotea tena ya Nchi flani ,hivi CIA wanaweza kujuwa kuwa msanii flani marekani atakufa,hivi CIA wanaweza juwa kuwa kunakiongozi mkubwa wa Nchi flani atakufa ,hao ni CIA Wanaweza kumpa TB Joshua nguvu ya kum ombea asiyezaa apate Mtoto tena amtabirie kuwa atapata Mtoto wa jinsia gani na pia CIA anaowahonga wanampanguvu ya kuponya watu ambao wameshindikana kwa Kansa na magonjwa sugu .naimani CIA wa TB Joshua ni MUNGU aliye hai na Jina la MUNGU libarikiwe AMEN
 
hii ni vita ya sadaka, enzi ya babu wa samunge sadaka zilipunguwa sana kwenye haya makanisa ya ndombolo, na babu alipigwa vita hasa.

nadhani sasa adui yao mpya ni tb joshua maana scoan wana agents Tanzania sasa hivi, inawezekana mafungu ya 10 yamepunguwa ndio hasira zote hizi.

huyu mzee wa upako anayetunzwa pesa jukwaani utazani muimbaji wa ngwasuna anapata wapi credibility ya kunyoshea wengine vidole?


Mungu atuongoze na kutuonyesha njia sahihi. Kiukweli haya mambo ni magumu sana.
 
Wanaacha Kuhubiri Neno La Mungu Wanatumia Muda Mwingi Kusemana. Hakuna Aliye Mkamilifu Chini Ya Jua, Nashangaa Hao Wanaojihesabia Haki Nakuona Wengine Wamepungukiwa Utukufu Wa Mungu.
 
Katika Misa ja Jumapili kama wiki mbili zilizopita Mzee wa Upako Mch Antony Lusekelo amechukizwa na tabia ya watu wanaojiita manabii, anasema, nashangaa kumsikia mtu akijiita nabii, akiweza kutabiri juu ya ndege ya malaysia Airline kupotea huku akishindwa kutabiri juu ya watoto wasio na hatia waliotekwa na Boko haramu tena kwenye nchi yake mwenyewe.

Anaendelea kusema hebu waangalie matendo makubwa aliyofanya Nabii Elisha, Elisha alikuwa na upako hata wa kuweza kujua kwamba kwa sasa nafatwa na maadui na hata kuwapofoa macho maadui zake.

Mzee wa upako anasema nashangaa kumuona TB Joshua yeye kushindwa kuwashikisha adabu Boko Haramu kama Nabii Elisha alivowashikisha adabu maadui zake.Mzee wa upako anaendelea kusema anachokifanya TB Joshua ni kununua habari hata kabla hazijatoka, kwa kuwapa fedha waandishi wa habari na CIA.

Mimi binafsi Nilikaa chini na kutafakari maneno yake na nimekiri kuwa watu hawa wanaojiita manabii ni wasanii, matendo yao hayafanani na Manabii kama Musa na Elisha lakini najiuliza swali ina mana tumeshindwa kabisa kuelewa usanii huu?, kila kukicha watu wanakimbilia kwa TB Joshua tena wengine wenye elimu kubwa za Masters na PHD lakini wanashindwa kufanya uchambuzi wa mambo hayo.

Karibuni wote tujadiri swala hili.

Unataka 'tujadiri' if not tujadili nini kiongozi maana sikupatipati..
 
One might ask why a nation like Nigeria that has a world class Prophet like T.B Joshua and other great Men of God known worldwide continue to experience bombings and killings of all sort, perpetrated by some extremist group in their country?,

Why can’t God use T.B Joshua to end the crisis in his own land
just as HE has been using the Prophet to do greater things in the life of many and other nations all over the world?But let us not be quick to forget that since the start of the present crisis in Nigeria, T.B Joshua has remained persistent in exposing the mind of God concerning the situation of terror presently facing the nation.

Prophet T.B Joshua has continued to advice the nation on how to handle the Boko-Haram crisis for peace to return to the land but, unfortunately, those in the higher authorities in the country, neither take him, his advices nor his prophetic declaration serious;all of his words where ignored and swept under the carpet.

It was in Prophet Elisha’s reign that there was a great famine in Samaria, where Parents were using their Sons for meal to survive and yet, Elisha could not do anything about it until the king recognized the God of Elisha (2King6). When a nation ignores Gods voice, such nation will keep on prolonging her crisis and keep fighting the wrong battle that may even consume them at the end.

In a battle of warfare everyone has his or her own role to play, the Prophet can’t do what is meant for the Soldier likewise, the Soldier cant do what is meant for the Prophet. The Crisis in Nigeria is a battle between light and darkness, you cannot fight darkness with darkness, you need light to fight darkness and this is why the nation needs to seek counsel from the Prophet to handle their present situation.

The killing and arrest of key leaders of the Boko-Haram sect and other extremist group will not guarantee the end of terrorism and militancy in Nigeria; only peaceful negotiation and Gods intervention can stop this act of terror in Nigeria. Let the leaders be united, throw sentiment away and seek for counsel from the Prophet; never say we are in a modern world and Prophets are not needed.

The God who raised a Prophet like T.B Joshua in this modern age has reasons for doing so; and the Prophet has shown his genuine willingness to help the nation.
The nation should take note that most of those International nations fighting terrorists and advocating for no negotiation with terrorists; are not fighting this extremist group in their own soil, neither are they fighting them in their territory and also, the terrorist they are fighting are not their citizens but foreigners.But the Nigeria case is a fight between the Government and some group of citizens brainwashed to fight their people due to some unclear motives. And the Government should not close its eyes to the fact that some of the politicians and security personnel are Sympathetic to this extremist group which is also very dangerous to the territorial integrity of the nation if immediate actions are not taking to invite all parties involved to a negotiation table to end the act of terror.

The more a nation ignores God’s instructions, the more the evil plans of the devil will continue to strive in that Land. First get the terrorist to drop their arms through a peaceful negotiation and God will take control of the rest. God loves sinners but hates sin; that is, He loves thieves, killers, homosexuals, kidnappers and terrorists but hates the spirit behind their misconduct. The battle is not a fight against flesh and blood but evil spirits therefore; our neighbors are not the enemies but evil spirit.
you are 100% correct sir,the problem with people criticizing Prophet T.B. Joshua is that they do not know that a prophet is there to serve GOD as a Go-between information Agent,he is there to explain the unfoldind issues of GOD before them as they are not entitled to such a power of a Prophet granted by GOD.They want Prophet to fulfill their wishes as the way they want while GOD is not like that.
 
Na masanja mkandamizaji anataka kuwa mchungaji.

Hata mimi nataka kua mchungaji, hii ndio biashara inayolipa kwa sasa. hadi hapo wajinga watakapo erevuka.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Nani alikwambia imani inahusiana PhD au Masters? Elimu yenyewe ya bongo ya vitini na tests??
Shida moja ni kuwa mnatumia ulimwengu wa mwili kwa mambo ya kiroho, hamtakaa muelewe mtaishia kubisha na kukashifu tu. Hivi hujui hata Yesu walimuita msanii nyakati zake? Sasa kama Yesu aliyeponya watu akafufua mpaka wafu walimuita msanii, unachoshangaa kwa TB Joshua ni nini? Hivi huyo mzee wa upako yeye kipi hasa cha kumuamini nacho ikiwa anakashifu watu wanaofanya kazi kama yake? Ni vema kujua, nyakati hizi shetani yuko very busy na wenye tamaa za mali na wavivu wa kufikiri. Nenda kiroho utaelewa ikiwa ni kweli au la.

umenena yaliyo ya kweli
 
Lakini kumbuka elimu hii ya Dunia ndio inayotupa maarifa hata ya kufanya kazi ya mungu ndio mana Dini zote zina waasa watu wasome elimu ya duniani ili kupata maarifa zaidi

Kama hivyo ni kweli, ni kwanini dini fulani haiwapi uhuru "watumwa" wake wakahamia dini nyingine? Mtu akihamia dini nyingine anatangaziwa adhabu ya kifo.
Anachofanya mzee wa upako ni aina flani ya wivu tu. Kama TB Joshua ananunua habari CIA na zinamlipa kwanini nayeye asinunue? Au yeye hapendi pesa? Na kama angekuwa hapendi pesa ni kwanini anapohubiri kwenye tv, screen yote yamejaa maandishi ya watu kumchangia kwa namba za MPesa, Tigopesa, Airtel money, CRDB cimbanking, NMB cimbanking, Zapmoney......?
 
Katika Misa ja Jumapili kama wiki mbili zilizopita Mzee wa Upako Mch Antony Lusekelo amechukizwa na tabia ya watu wanaojiita manabii, anasema, nashangaa kumsikia mtu akijiita nabii, akiweza kutabiri juu ya ndege ya malaysia Airline kupotea huku akishindwa kutabiri juu ya watoto wasio na hatia waliotekwa na Boko haramu tena kwenye nchi yake mwenyewe.

Anaendelea kusema hebu waangalie matendo makubwa aliyofanya Nabii Elisha, Elisha alikuwa na upako hata wa kuweza kujua kwamba kwa sasa nafatwa na maadui na hata kuwapofoa macho maadui zake.

Mzee wa upako anasema nashangaa kumuona TB Joshua yeye kushindwa kuwashikisha adabu Boko Haramu kama Nabii Elisha alivowashikisha adabu maadui zake.Mzee wa upako anaendelea kusema anachokifanya TB Joshua ni kununua habari hata kabla hazijatoka, kwa kuwapa fedha waandishi wa habari na CIA.

Mimi binafsi Nilikaa chini na kutafakari maneno yake na nimekiri kuwa watu hawa wanaojiita manabii ni wasanii, matendo yao hayafanani na Manabii kama Musa na Elisha lakini najiuliza swali ina mana tumeshindwa kabisa kuelewa usanii huu?, kila kukicha watu wanakimbilia kwa TB Joshua tena wengine wenye elimu kubwa za Masters na PHD lakini wanashindwa kufanya uchambuzi wa mambo hayo.

Karibuni wote tujadiri swala hili.

TB Joshua aneni yatokayo kinywani kwake ila anachoambiwa na roho mtakatifu awezi kukulupuka kama lusekelo au kumjibu lusekelo kwa kuwa lusekelo anaongea anayoambiwa na mkwewe.roho wa MUNGU ni tofauti na roho wa shetani.TB JOSHUA ajahambiwa haongee kuusu boko haramu pindi roho wa MUNGU atakapo mruhusu ataongea.hata manabii wa zamani walikuwa wanahamlishwa na roho wa MUNGU na si kwa matakwa yao na pindi waombapo shida fulani uongozwa na roho jinsi ya kufanikishwa.upayukaji wa lusekelo ni wa kibinadamu yeye aongozwi na roho wa MUNGU na roho wa MUNGU awezi kuongea maneno ya kukashifu hapo ni pepo mchafu alimwingia anene hayo
 
Lakini kumbuka elimu hii ya Dunia ndio inayotupa maarifa hata ya kufanya kazi ya mungu ndio mana Dini zote zina waasa watu wasome elimu ya duniani ili kupata maarifa zaidi

Pia ukumbuke kuna kikomo cha ufahamu wa mambo ya dunia katika kung'amua mambo ya kiroho. Kuna mazingira bila nguvu za kiroho hufanyi chochote, hapo ndo unapoona kikomo cha uwezo wa kidunia.
 
Ukiona mtumishi wa Mungu anaacha kufanya kazi yake ya msingi ambayo ni kueneza neno la Mungu; na badala yake anaongelea na kukosoa watumishi wengine muogope kuliko njaa…
Ameeen! Yeye ni nani hata athubutu kumhukumu TB Joshua? Mie jamani na Ukatoliki wangu mpaka kifo kitutenganishe. Mungu wangu na miujiza yake naipatia huku huku niliko.
 
Back
Top Bottom