Katika Misa ja Jumapili kama wiki mbili zilizopita Mzee wa Upako Mch Antony Lusekelo amechukizwa na tabia ya watu wanaojiita manabii, anasema, nashangaa kumsikia mtu akijiita nabii, akiweza kutabiri juu ya ndege ya malaysia Airline kupotea huku akishindwa kutabiri juu ya watoto wasio na hatia waliotekwa na Boko haramu tena kwenye nchi yake mwenyewe.
Anaendelea kusema hebu waangalie matendo makubwa aliyofanya Nabii Elisha, Elisha alikuwa na upako hata wa kuweza kujua kwamba kwa sasa nafatwa na maadui na hata kuwapofoa macho maadui zake.
Mzee wa upako anasema nashangaa kumuona TB Joshua yeye kushindwa kuwashikisha adabu Boko Haramu kama Nabii Elisha alivowashikisha adabu maadui zake.Mzee wa upako anaendelea kusema anachokifanya TB Joshua ni kununua habari hata kabla hazijatoka, kwa kuwapa fedha waandishi wa habari na CIA.
Mimi binafsi Nilikaa chini na kutafakari maneno yake na nimekiri kuwa watu hawa wanaojiita manabii ni wasanii, matendo yao hayafanani na Manabii kama Musa na Elisha lakini najiuliza swali ina mana tumeshindwa kabisa kuelewa usanii huu?, kila kukicha watu wanakimbilia kwa TB Joshua tena wengine wenye elimu kubwa za Masters na PHD lakini wanashindwa kufanya uchambuzi wa mambo hayo.
Karibuni wote tujadiri swala hili.