Mzee Kikwete kukemea Udini peke yake haitoshi tunataka Msimamo wako juu ya Mkataba mbovu wa Bandari

The Burning Spear

JF-Expert Member
Dec 23, 2011
3,445
8,300
Bila kupoteza mda waraka wa Maaskofu umemtoa Kikwete pangoni alikojificha siku nyingi.

Binafsi nimekuwa nikihoji uadilifu wa huyu mstaafu na faida yake kwa nchi pale mambo yanapokuwa yanaenda mrama amekuwa kimya sana.

Sasa tumemskia anakemea udini ambayo ni planned huko mara kwenye kanisa la wasabato.. maaskofu wamefanya makusudi maana jambo hili serikali inalichukulia lele mama

Lakini nilitegemea Kikwetele atoke mapema hata kabla ya waraka maana mambo yalishaonekana mapema kabisa . Tulisikia Dpw wanakuja.kujenga misikiti...

Ni mambo mengi sana ya hovyo yametendeka alikuwa kimya kwa mfano isue ya sukuma gang alikuwa wapi? naona ni.mwendelezo tu wa haya ya udini.

Pamoja.na kukemea udini sijasikia hoja yake ya msingi juu ya maktaba mbovu wa bandari ambao ndiyo chanzo Cha yote haya. Alipaswa atoe way foward siyo ngonjera na masimango.

Mpaka Maaskofu wanatoa waraka im.sure wamejirizisha pasipo shaka kwamba serikalii bado inataka muwaburuza wananchi kwenye uwekezaji huu.

Kwa hiyo atoe maoni yke tumsikie
 
Hiyo hawezi kuja maana facts, hard facts zitamuaibisha! Hard facts negate his stand!

Christians should both be active in politics but also careful not to equate Christianity with their political positions.

Timothy Keller
Those who avoid all political discussions and engagement are essentially casting a vote for the social status quo. American churches in the early 19th century that did not speak out against slavery because that was what we would now call ‘getting political’ were actually supporting slavery by doing so. To not be political is to be political … Nevertheless, while believers can register under a party affiliation and be active in politics, they should not identify the Christian church or faith with a political party as the only Christian one

 
Bila kupoteza mda waraka wa Maaskofu umemtoa Kikwete pangoni alikojificha siku nyingi.

Binafsi nimekuwa nikihoji uadilifu wa huyu mstaafu na faida yake kwa nchi pale mambo yanapokuwa yanaenda mrama amekuwa kimya sana...
Ni kweli kabisa. Ilibidi atoke mbele kama ilivyofanya TEC na kusema bilaunafiki wala kujifichaficha kwamba, ANAUPINGA mkataba au ANAUUNGA MKONO..!! Full Stop.
 
Bila kupoteza mda waraka wa Maaskofu umemtoa Kikwete pangoni alikojificha siku nyingi.

Binafsi nimekuwa nikihoji uadilifu wa huyu mstaafu na faida yake kwa nchi pale mambo yanapokuwa yanaenda mrama amekuwa kimya sana...
Weledi gani kwa Kikwete?
 
Hapa mmeshaleta udini kwenye hili Sasa kila dini isimame upande wake tuone Nani mshindi.
 
Ni kweli ukisemacho, kwamba, uwekezaji ni muhimu, ILA, SI KWA MIKATABA YA KILOFA KAMA HUU WA DPW. Weka msimamo wako wazi, unapinga au unauunga mkono mkataba wa DPW na TZ kama ulivyo sasa?
Huu mkataba hata chifu Mangungo angeukataa
 
Bila kupoteza mda waraka wa Maaskofu umemtoa Kikwete pangoni alikojificha siku nyingi.

Binafsi nimekuwa nikihoji uadilifu wa huyu mstaafu na faida yake kwa nchi pale mambo yanapokuwa yanaenda mrama amekuwa kimya sana...
Aliyemwandikia hiyo hotuba ndiye alimwingiza chaka zaidi ingawa yeye ndiye mwenye mawazo hayo hayo!

Nilimsikiliza mwanzo mwisho sikumuelewa mantiki yake ya msingi!

Eti dini na siasa!

Tangu lini samaki na maji vikatenganishwa?

Ama Tec kukemea mkataba wa mangungo wa kubadilisha nchi kwa shanga za kiunoni ndiyo imekuwa dini na siasa?

Matamko yote yaliyotolewa na viongozi wa dini kutetea maslahi ya jimii katika awamu zote za tawala zilizopita leo kayasahau isipokua kwa awamu hii pekee?

Ndiyomaana watu wengi wanasema kaidhalilisha sana hadhi ya maRais wastaafu!

Hakujifunza kwa wenzake Nyerere na Mkapa namna walivyokuwa na turufu ya kuingilia mambo ya kiTaifa hasa inapotokea Serikali iliyopo madarakani "inalikoroga"!

Jana nilimsikia akisema: ..." aah mimi nimestaafu"...!

Tangu lini Rais mstaafu anastaafu kwa mambo muhimu ya kiTaifa!

Hizo 80% ya mishahara ya Rais aliyepo madarakani wanazoendelea kulipwa na maupurupu mengine hadi kufa, huwa ni kwa ajili gani labda?

Kimantiki busara za Rais huwa hazistaafu kwa kushauri masuala muhimu ya Taifa.

Mimi naona Samia mwenyewe angelifungia kibwebwe kulimaliza suala hili, mbona ni rahisi sana tu?

Kwa sababu wote ambao yeye anawategemea kusimama kwenye mimbari waweze kuuzima moto huu uliowaka, hawakubaliki katika jamii, ama hoja wanazokuja nazo ni mfu hazijengi, zinazidi kumharibia kadri siku zanaposonga mbele.
 
Back
Top Bottom