Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,021
- 2,478
I. UTANGULIZI
Aya ya 19(2) katika Katiba ya Tanzania (1977) inaizuia serikali kujitenga na ubaguzi wa kidini na kuhimiza usawa wa kidini kwa kutumia maneno ifuatayo:
"Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi."
Katika mipaka ya nukuu hii, tunaunga mkono onyo la Rais Mstaafu, Jakaya KIkwete, katika kupinga tunu hasi za udini, usiasa, ukabila, urangi, na ukanda. Yaani, tunapinga ubaguzi wa kidini, ubaguzi wa kisiasa, ubaguzi wa kikabila, ubaguzi wa kirangi, na ubaguzi wa kikanda.Udini ni tabia ya kukweza dini yak dhidi ya dini baki, usiasa ni tabia ya kukkweza itikadi ya chama chako dhidi ya itikadi za vyama baki, ukabila ni tabia ya kukweza kabila lako dhidi ya makabila bako, urangi ni tabia ya kukweza rangi yako ya ngozi dhidi ya rangi baki za ngozi, na ukanda ni tabia ya kukweza kanda yako dhidi ya kanda baki. Zote ni ni tunu hasi dhidi ya ustawi wa watu na mslahi ya pamoja katika Taifa.
Pia tunaungana naye katika kupigania tunu chanya zifuatazo: tunu ya kujitenga na udini, tunu ya kujitenga na usiasa, tunu ya kujitenga na ukabila, tunu ya kujitenga na urangi, na tunu ya kujitenga na ukandaa. Yaani, tunapigania tunu chanya za usawa wa kidini, usawa wa kisiasa, usawa wa kikabila, usawa wa kirangi, na usawa wa kikanda.
Tunu chanya za usawa wa kidini, usawa wa kisiasa, usawa wa kikabila, usawa wa kirangi, na usawa wa kikanda zinawezekana kwa sababu ya tunu mtambuka zinazozalisha umoja wa kijamii, yaani tunu mtambuka ya utu, tunu mtambuka ya uzalendo kwa nchi, na tunu mtambuka ya uraia wa Tanzania.
II. AINA NNE ZA WATANZANIA ALIOWAONGELEA KIKWETE
Lakini, kama watanzania wakiulizwa waseme wako katika upande gani wa kila tunu iliyotajwa hapo juu watagawanyika kwenye makundi 16 yafuatayo:
Wito wa KIkwete ni kwamba tupiganie ujenzi wa Taifa lwenye watu walio kwenye aina ya 16 pekee. Hakuna mtu mwenye akili timamu anayepinga wito huo.
Hata hivyo, KIkwete aliongelea tunu mbili pekee, yaani tunu ya usawa wa kidini na tunu yausawa wa kisiasa, zinazozaa makundi manne ya watu.
Hivyo, kwa jili ya kuboresha alichokisema Kikwete kuhusu tunu hizi mbili, tunapenda kujadili watu walio kwenye makundi hayo manne pekee, kama mchoro ufuatao unavyoonyesha.
Kutokana na mchoro huu, ni wazi kwamba, kadiri maamuzi ya kidini na maamuzi ya kisiasa yanavyohusika , kuna Watanzania wa aina nne, kama ifuatavyo:
- Watanzania wenye udini na wenye usiasa kila mahali na kila wakati. Hawa wanakweza dini zao dhidi ya dini baki, na kukweza itikadi zao za kisiasa dhidi ya itikadi baki. Huu ni mseto wa tunu mbili hasi.
- Watanzania wenye udini na wasio na usiasa kila mahali na kila wakati. Hawa wanakweza dini zao dhidi ya dini baki, lakini hawakwezi itikadi zao za kisiasa dhidi ya itikadi baki. Huu ni mseto wa tunu hasi na tunu chanya.
- Watanzania wasio na udini na wenye usiasa kila mahali na kila wakati. Hawa hawakwezi dini zao dhidi ya dini baki, lakini wanakweza itikadi zao za kisiasa dhidi ya titikadi baki. Huu ni mseto wa tunu hasi na tunu chanya.
- Watanzania wasio na udini na wasio na usiasa kila mahali na kila wakati. Hawa hawakwezi dini zao dhidi ya dini baki wala kukweza itikadi zao za kisiasa dhidi ya itikadi baki. Huu ni mseto wa tunu chanya.
Hivyo, tunafikiri kwamba, KIkatiba na kisheria, onyo la Rais Mstaafu, Jakaya KIkwete, kuhusu alichokiita "tunu ya kujitenga na dini" pamoja na "tunu ya kujitenga na usiasa," linapaswa kutazamwa katika mipaka ya ukuta unaotenganisha maisha ya kidini na maisha ya kisiasa, uliopo kwa mujibu wa ibara ya 19(2) Katiba ya Tanzania.
III. MAANA YA UKUTA WA KIKATIBA UNAOTENGANISHA DINI NA SIASA
Tunapendekeza kwamba, ukuta wa KIkatiba unaotenganisha maisha ya kidini na maisha ya kisiasa ni kama dhana ya "semi-permeable membrane," tuliyoisoma kwenye bayolojia ya seli.
Yaani, ni ukuta wenye milango inayoruhusu vitu vilivyoko upande mmoja kupenya na kwenda upande wa pili, lakini inakataza vitu vilivyo upande wa pili kupenya na kuingia upande wa kwanza.
Ukuta wa kikatiba unaotenganisha dini na siasa unayo milango kama hiyo pia. Unawaruhusu watu walioko upande wa dini kusukuma mlango na kuingia upande wa serikali, lakini unawakataza watu walioko upande wa serikali kusukuma mlango na kuingia upande wa dini.
Hivyo, makuhani wanaweza kugombea udiwani, ubunge na urais, kama sheria za makanisa yao haziwakatazi. Mfano mzuri ni Askofu Gwajiboy ambaye ni Mbunge wa Kawe kupitia CCM.
Pia wanaweza kuzikosoa sera za serikali kwa niaba ya waumini wao. Lakini serikali haiwezi kuanzisha dini rasmi ya Taifa wala kuzikosoa sera za ndani ya taasisi za kidini, isipkuwa pale zinapokiuka katika ya nchi.
Hivyo, ukuta wa kikaiba unaotenganisha maisha ya kidini na maisha ya kisiasa, ni mwongozo kwa serikali kuhusu tunu ya kujitenga na ubaguzi wa kidini na kujinasibisha na tunu ya usawa wa kidini, ambao unatokana na tunu mtambuka zilizotajwa hapo awali.
IV. NAFASI YA TUNU MTAMBUKA KWENYE TEOLOJIA YA UKOMBOZI
Hata viongozi wa dini, ambao kimsingi ni wanateolojia, wanatuhimiza kuzienzi tunu mtabuka. Mwaka 1973, Profesa Gustavo Gutierez Merino wa Peru, huko Amerika ya Kusini, aliandika kitabu "A Theology of Liberation: History, Politics, and Salvation," kwa ajili ya kufafanua ukweli hii.
Tunaambatanisha kitabu kizima hapa chini baada ya kunukuu baadhi ya kauli zake muhimu kwa Tanzania ya leo hapa chini....
Profesa Merino anasema yafuatayo kuhusu tunu ya mshikamano:
“An essential clue to the understanding of poverty in liberation theology is the distinction, made in the Medellín document 'Poverty of the Church,' between three meanings of the term 'poverty': real poverty as an evil—that is something that God does not want; spiritual poverty, in the sense of a readiness to do God's will; and solidarity with the poor, along with protest against the conditions under which they suffer.”
Profesa Merino anasema yafuatayo kuhusu tunu hasi ya ubaguzi na tunu chanya ya usawa:
“The denunciation of injustice implies the rejection of the use of Christianity to legitimize the established order.”
Profesa Merino anasema yafuatayo kuhusu tunu chanya za utu, uhai, chakula, makazi, afya, elimu, na uhuru wa kujieleza, kwa upande mmoja, na kwa uoande mwingine, tunu hasi za unyonyaji, ukosefu wa ajira, kusigina hadhi ya utu, na utumwa.“In the final analysis, poverty means death: lack of food and housing, the inability to attend properly to health and education needs, the exploitation of workers, permanent unemployment, the lack of respect for one's human dignity, and unjust limitations placed on personal freedom in the areas of self-expression, politics, and religion.”
Aidha, Profesa Merino anasema yafuatayo kuhusu tunu chanya ya kutumia miwani ya historia ya jana kuitazama historia ya kesho, na tunu hasi ya ukuta unaotenganisha malimwengu ya kidini na malimwengu ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii.
“There are not two histories, one profane and one sacred, 'juxtaposed' or 'closely linked.' Rather there is only one human destiny.”
“History is no longer as it was for the Greeks, an anamnesis, a remembrance. It is rather a thrust into the future.”
Kwa hiyo, kuhusu Teolojia ya Ukombozi wa Rasilimali za Watanzania Wanyonge Dhidi ya Waarabu wa Dubai, Tamko la Maaskofu wa TEC juu ya Bandari zetu limegonga penyewe kwa wakati sahihi.
V. TAMKO LA MAASKOFU NI TAMKO LA KINABII
Wakati kauli za KIkwete zinaonekana kama zinaukandia tamko la TEC, huu ni waraka wa kinabii. Ushahidi wa hili umo kwenye maudhui ya Tamko, hasa zile nukuu za Misahafu, pamoja na mazingira yaliyouzunguka.
Kwa ujumla, tusisahau kwamba sababu zilizowasukuma Maaskofu wa TEC kuchukua hatua waliyoichukua ni nyingi kuliko zile walizozitaja kwenye tamko. Mifano ya sababu ambazo hawakuzitaja hizi hapa:
1. Hayati Magufuli alipiga marufuku makinikia kusafirishwa nje ya nchi, lakini leo marufuku hii imefutwa na kampuni ya kina Rostam Azizi inayoitwa Taifa Transport and Logistics Ltd ndiyo inasafirisha makinikia haya kutoka mikaoni hadi bandarini, kuyapakia kwenye meli hadi huko ng'ambo. Makao yake makuu yako Plot No. 77, Kipawa, Kiwalani Industrial Area, Dar es Salaam, Tanzania.
2. Rais Mstaafu KIkwete alimwahidi Rostam kile kiwanja cha Oysterbay, ilikokuwa POlice Officers Mess, kwa kuwa alitaka kuleta Wachina kujenga Supermarket kwa sharti kwamba wapewe Title Deed ya miaka 99. Mapatano yalikuwa kwamba, Rostam ajenga Kwota za Polisi kule Kunduchi, Pale Morocco, na Kuhamisha Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kukijenga pale Namanga kilipo sasa. Rostam kafanya haya yote kwa fedha yake ili apate uhalali wa kumilikishwa kiwanja cha Masaki. Ghafla Mwamba JPM akaingia Ikulu kabla Rostam hajakabidhiwa kiwanja hicho. Rostam akaambiwa, chagua moja: ama nikurudishie fedha zako au nikupe kiwanja kule Bagamooyo, lakini sio hapa Masaki. Rostam kwa unyonge akaomba arudishiwe fedha zake, Na Magufuli hadi anakufa aligoma kuzindua zile KJwota za Polisi kwa sababu ya hasira! Zimezinduliwa majuzi wakati wa uongozi wa Rais Samia.
3. Lakini, wakati hayati Magufuli alimnyima Rostam kile kiwanja cha Oysterbay, ilikokuwa POlice Officers Mess, kwa kuwa alitaka kuleta Wachina kujenga Supermarket kwa sharti kwamba wapewe Title Deed ya miaka 99, leo tunataka kutoa bandari zote 88 kwa miaka zaidi ya 99.
4. Wakati hayati Magufuli alikataa wazo la kuhamisha kituo cha Polisi cha Oysterbay hadi Namanga, japo akawa amechelewa, na hilo likatokea chini ya awamu ya Kikwete; alichukua hatua za haraka kuzuia michakato iliyokuwa ifuate. Alifanya hivyo mara tu baada ya kuingia ofisini. Leo Samia anataka kuhamisha Chuo cha Polisi cha Kigamboni na kukipeleka anakokujua yeye, ili KIgamboni awakabidhi Waarabu wa Dubai kwa miaka zaidi ya 99. Watalipa fidia kama Rostam alivyotaka kufanya wakati anahamisha kituo cha Polisi cha Oysterbay kutoka kule ufukweni hadi pale Namanga.
5. Mdogo wake Rostam, aitwaye Akram Aziz, alishtakiwa na kupokonywa bunduki 56 alizokuwa anamiliki kiharamu kwa ajili ya ujangili, lakini sasa amerudishiwa silaha hizo, na ujangili ni business as usual.
6. Akram Aziz aliposhtakiwa mwaka 2018 Mahakama ilitaka afungwe na kulipa faini kwa pamoja, lakni Nchimbi wakati huo akiwa waziri wa Mambo ya Ndani akacheza muziki wake adhabu ikawa either/or scenario. Zawadi yake ilikuwa ni bonge la "kitu" kule Boko. Sasa Nchimbi amerudishwa nchini, huenda, kwa ajili ya kuimarisha Timu Rostam.
7. Hakuna mwekezaji wa kigeni anayekanyaga Tanzania bila kwanza kwenda KUHIJI NA KUSUJUDU nyumbani kwa Rostam Aziz, na DP World wakiwemo, hata kama ametoa kauli ya kuwaruka juzi.
8. Wakati tunayafahamu haya yote, tumemwona Rostam Aziz ameketi na Rais Saimia huko Marekani wakisaini mikataba ya siri. Mpaka leo hatujaambiwa wakati sisi ndio wananchi wenye wenye nchi.
9. Haya tunayoyasema hapa, ni habari za wazi sana katika duru za vyombo vya ulinzi na usalama. Tatizo wakubwa kadhaa tayari wametekwa. Jana tuliulizwa kutoa maoni yetu kuhusu dhana kwamba IGP Camillius Wambura aliyewaweka kizuizini kina Dr Slaa anapaswa kujiuzuli. Tunasema hapana. Alitumwa. Kumwadhibu yeye ni sawa na kujaribu kuliua joka kubwa kwa kupiga mkia wake badala ya kugonga kichwa. Tunapaswa kugonga kichwa. Lakini kazi ya kugonga kichwa ni ngumu sana kiasi kwamba kunahitajika detonator kabambe. Ugumu wake uko hivi: Rais Samia amejilundikia "watu wake" kiasi kwamba tatizo la "collective thinking" sasa limezingira "makao." Just imagine the Topmost Three ndani ya "Eagles House" ni Wazanzibari. Rais ni Mzanzibari. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mzanzibari. Asilmia 21 ya ajira za Muungano ni za Wazanzibari. Mbarawa wa IGA Mzanzibari. Hamza Johari wa IGA Mzanzibari. Nchi imetekwa.
VI. HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
10. Kwa ufupi, tunachosema ni kwamba, Rais Mstaafu Kikwete afahamu kuwa yeye ndiye mwasisi wa Timu Rostam na kwamba Timu Rostam ni hatari kwa usalama wa Rais Samia, Usalama wa CCM na kwa usalama wa Taifa kwa ujumla. Ni timu ya watu wanaofanya uhaini wa kiuchumi. Lakini Maaskofu wa TEC sio hatari kwa usalama wa Taifa letu. Kikwete ajifunze kusoma alama za nyakati na kuchukua hatua sahiki. Kwa leo tunaishia hapo.
Dawati la Mama Amon
"Sumbawanga Town"
Sumbawanga.